Heshima sana wanajamvi,
Mosi unatakiwa kujua majukumu ya Waziri wa Utumishi na Utawala bora.
Kifupi sana hii wizara pamoja majukumu yake ya kusimamia utumishi lakini pia kuna huu utawala bora.Utawala bora maana yake ni pamoja na kuisimamia TISS & TAKUKURU.Hii ni moja ya Wizara nyeti kweli kweli.TISS imo kila mahali kuanzia uraiani,majeshi yote ya Ulinzi na Usalama & mashirika yote ya umma na sehemu zote nyeti.TISS ina jukumu la kuwatafuta na kuwapachika wale maJAJI wa kuchonga.
Wizara hii tunaweza kusema pasipo shaka ndio utoa DIRA namna ya uendeshaji nchi kuanzia teuzi nyeti mbali mbali.Kifupi kabla haujateuliwa hawa jamaa wanakuwa na record zako zote.
Nafikiri huyu Mwamba kilichomwondoa pale ni mambo mawili.
Moja zipo tuhuma kwamba yeye na Majaliwa waliachiwa mambo yote ya ulinzi na usalama huku Bi Mkubwa akijishughulisha na masuala madogo madogo.Tuhuma hizi zilitolewa na yule Mwamba aliyetandikwa risasi nyingi lakini Mwenyezi Mungu akamnusuru na umauti.Dogo akitumia ukaribu baina yake na Bi Mkubwa (Mama Mkwe) alijikuta akipitiliza na Wazee wa nchi wakashauri ni vyema akaondolewa mara moja.
Waziri wa Utawala Bora ndiye aliyeshauri kesi ya yule Mwamba ipelekwe Mahakamani kwakuwa kuna ushahidi wa kutosha tena usioacha mashaka mashaka.File lilipopelekwa Wizara ya yule Waziri mtoa macho likapata baraka zote.Baada ya kesi kuunguruma Mahakamani mambo ya PGO na kina Kingai yakaonekana hovyo kabisa kesi haina mashiko.Ikabidi muhimili uliojichimbia zaidi kutumia njia ya mkato (MAJAJI MICHONGO) kuepeka aibu.
Majaji Michongo wamejitahidi sana tena sana kuibeba JAMHURI na wengine kupandishwa cheo lakini kila hatua au kadri siku zinavyosonga mbele KESI ya UGAIDI inazidi kukosa uhalali wa kuendelea kuwepo Mahakamani.Mawakili wa Serekali wamepewa msaada wote ikiwemo kusaidiwa na Majaji Michongo lakini wapi !.
Kesi ipo kwasababu inatafutwa njia nyingine ya kujisafisha ikiwemo kutumia watu wapuuzi kama Zitto wamuadae Mwenyekiti aingie mkenge kama Ndugai mambo yaishe.Ni suala la muda tu Mwamba atakuwa huru huku jina lake likizidi kutakaswa na heshima yake ikizidi kupaa.