Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Heshima sana wanajamvi,

Mosi unatakiwa kujua majukumu ya Waziri wa Utumishi na Utawala bora.

Kifupi sana hii wizara pamoja majukumu yake ya kusimamia utumishi lakini pia kuna huu utawala bora.Utawala bora maana yake ni pamoja na kuisimamia TISS & TAKUKURU.Hii ni moja ya Wizara nyeti kweli kweli.TISS imo kila mahali kuanzia uraiani,majeshi yote ya Ulinzi na Usalama & mashirika yote ya umma na sehemu zote nyeti.TISS ina jukumu la kuwatafuta na kuwapachika wale maJAJI wa kuchonga.

Wizara hii tunaweza kusema pasipo shaka ndio utoa DIRA namna ya uendeshaji nchi kuanzia teuzi nyeti mbali mbali.Kifupi kabla haujateuliwa hawa jamaa wanakuwa na record zako zote.

Nafikiri huyu Mwamba kilichomwondoa pale ni mambo mawili.
Moja zipo tuhuma kwamba yeye na Majaliwa waliachiwa mambo yote ya ulinzi na usalama huku Bi Mkubwa akijishughulisha na masuala madogo madogo.Tuhuma hizi zilitolewa na yule Mwamba aliyetandikwa risasi nyingi lakini Mwenyezi Mungu akamnusuru na umauti.Dogo akitumia ukaribu baina yake na Bi Mkubwa (Mama Mkwe) alijikuta akipitiliza na Wazee wa nchi wakashauri ni vyema akaondolewa mara moja.

Waziri wa Utawala Bora ndiye aliyeshauri kesi ya yule Mwamba ipelekwe Mahakamani kwakuwa kuna ushahidi wa kutosha tena usioacha mashaka mashaka.File lilipopelekwa Wizara ya yule Waziri mtoa macho likapata baraka zote.Baada ya kesi kuunguruma Mahakamani mambo ya PGO na kina Kingai yakaonekana hovyo kabisa kesi haina mashiko.Ikabidi muhimili uliojichimbia zaidi kutumia njia ya mkato (MAJAJI MICHONGO) kuepeka aibu.

Majaji Michongo wamejitahidi sana tena sana kuibeba JAMHURI na wengine kupandishwa cheo lakini kila hatua au kadri siku zinavyosonga mbele KESI ya UGAIDI inazidi kukosa uhalali wa kuendelea kuwepo Mahakamani.Mawakili wa Serekali wamepewa msaada wote ikiwemo kusaidiwa na Majaji Michongo lakini wapi !.

Kesi ipo kwasababu inatafutwa njia nyingine ya kujisafisha ikiwemo kutumia watu wapuuzi kama Zitto wamuadae Mwenyekiti aingie mkenge kama Ndugai mambo yaishe.Ni suala la muda tu Mwamba atakuwa huru huku jina lake likizidi kutakaswa na heshima yake ikizidi kupaa.
Mama alianza vizuri na aliungwa mkono tukashangaa ghafla bin vuu, mbowe na ugaidi na hii kesi ndio imefanya Rais achukiwe mchengerwa alifanya poor calculation aisee ya hii kesi ambayo ilifanya Hadi Rais asiitwe kwa Biden, ni heri ifutwe maana ni aibu tupu.
 
Alifanyaje kwani huyu mchengerwa Mimi nilikuwa namuona smart sana
Yeye bado kijana sana ile Wizara ni kubwa haihitaji sifa za kijinga, ndiyo maana hiyo Wizara alikuwa akipewa Mzee Mkuchika, mwanajeshi mstaafu na mkongwe wa system

Kuwa Waziri wa Utawala Bora maana yake unasimamia Idara ya Usalama wa Taifa, ile "Utumishi" huwa inawekwa tu kuficha kazi ya msingi kabisa ya Wizara hii, kuratibu shughuli zote za watu wasiojulikana na Takukuru, makesi ya kusingiziasingizia

Sasa ingetokea watu wakaanza kuuawa katika mazingira yanayoashiria uhusika wa serikali kama enzi za Magufuli, basi shutuma moja kwa moja zingeelekezwa kwa Rais na mkwe wake; tayari Mchengerwa anahusika kwa kiasi kikubwa na kesi ya uongo dhidi ya Freeman Mbowe, keshamwingiza Mama Mkwe wake matatizoni

Kwa hiyo kumtoa Utumishi/Utawala bora ni kumwokoa na dhahma huko mbele ya safari maana Mama Mkwe muda wake wa Urais utapita, Mchengerwa angebeba madhambi yote ya Mama Mkwe wake kama kina Sabaya, Ndugai, Polepole, Kabudi, Makonda na wengineo wanavyobeba madhambi ya Magufuli
 
Si busara Mkwe wa Rais kuongoza Wizara inayosimamia Usalama wa Taifa; tayari huyu Mchengerwa alishamwingiza mama mkwe wake kwenye kesi ya mchongo ya Freeman Mbowe

Mchengerwa, Mkwe wa Mama Samia ndo Makonda na Sabaya wa Awamu ya 6
Pia yasemekana amekuwa anavuta mpunga sana kwa wawekezaji wanaotaka kuuingiza mtaji nchini kwa ahadi ya kuwaunganisha na Rais
 
Wakati watu wakipitea wakati wa magu nani alikuwa wizarani hapo? Aamewajibikaje?
 
Watapanguana sana,ila laana ya JPM itawatafuna wanafiki na wauaji wake taratibu.

Muda utaongea...
 
Wakati watu wakipitea wakati wa magu nani alikuwa wizarani hapo? Aamewajibikaje?
Mkuchika, sasa inategemea na hulka ya waziri husika pia, Magufuli alikuwa na kikundi chake cha kupoteza watu, wazee kama akina Mkuchika walipohoji wakapigwa na maradhi yasiyojulikana hadi leo...ndiyo maana unaona Mama anamteua tu kama Waziri asiye na Wizara Maalum ili kumfuta machozi na kumsaidia apate huduma za matibabu zinazogharimikiwa na serikali
 
Sio kumfuta machozi bali hakuna kijiji kikakosa wazee
 
Mkuchika, sasa inategemea na hulka ya waziri husika pia, Magufuli alikuwa na kikundi chake cha kupoteza watu, wazee kama akina Mkuchika walipohoji wakapigwa na maradhi yasiyojulikana hadi leo...ndiyo maana unaona Mama anamteua tu kama Waziri asiye na Wizara Maalum ili kumfuta machozi na kumsaidia apate huduma za matibabu zinazogharimikiwa na serikali
Dah nchi hii ina mambo mengi sana nyuma ya pazia plus umafia
 
Uyo wazir aliewekwa sasa ni mchumia tumbo hatari, yeye anachojua ni kutetea maslahi ya CCM tu
 
Huyu kuondolewa pale imeniuma sana.Anyway serikali ya wanyonge ishapitwa na wakati
 
Back
Top Bottom