Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Unataka kusema kwamba SGR na Stigler Gorge hakutaka watu wapande?
Ninadhani upandishwaji wa madaraja kwa wakati ilikua msukumo zaidi kutoka kwa mkuu wa nchi.
Mchengerwa alikua mtekelezaji tu wa maelekezo kutoka kwa mh. Rais.

Hata awamu iliyopita sio kwamba Mkuchika hakua na uwezo wa kupandisha madaraja kwa wakati bali alitii maelekezo ya mamlaka iliyokua imemuweka
 
Rasmi sasa maoni ya watumishi walio wengi wanaona kumleta Mhagama Utumishi anakuja kuwadidimiza na sera mbovu alizokuwa nazo kipindi cha Mwendazake kama vile kikokotoo

Wamemuomba mama angembakiza Mchengerwa kwani amekuwa waziri aliyekuwa anawasikiliza watumishi kwani kipindi kifupi sana watumishi waliokuwa hawajapanda madaraja walipanda wote bila upendeleo pia malimbikizo ya watumishi yalikuwa yameanza kulipwa

NB: Mhagama umeanza kutiliwa mashaka na watumishi kwamba ni mmoja wa waliokandamiza watumishi

Jirekebishe au upewe wizara nyingine
 
Kwa maoni yangu huyu alipaswa pia apumzishwe hakufaa kurudi kwenye kikosi.

Nadhani kapewe nafasi ya mwisho, ataaamua mwenyewe hatma yake, either apige kazi vizuri aendelee au avurunde apigwe chini.

Kwa sasa anatakiwa ashughulikie na azitatue kero za watumishi ili wawe na Imani na Serikali yao.
 
Mama chonde chonde, nakuomba tena kwa kusisitiza sana, mrejeshe Mohammed Mchengerwa Wizara ya Utumishi. Huyo bwana hapo alikuwa smart sana na alijitahidi sana kushughulikia na kutolea ufafanuzi kwa ufasaha kabisa masuala ya kiutumishi.

Huyu kipaza sauti uliyemleta utumishi naomba arudi huko kwenye sera na siasa nyingine. Mhagama ni mpiga mayowe tu na hawezi kujenga hoja, atasababisha uchukiwe bure na watumishi.

Mchengerwa ni smart sana ambaye ameanza vizuri, hupaswi kumkatisha tamaa kwa kupeleka huko.

Yule anatakiwa Utumishi au TAMISEMI. Very smart

Mwisho rekebisha jina la Wizara ya Gwajima hasa pale kwenye Wanawake na Jinsia hapajakaa vizuri maana neno jinsia linatisha sana

Kazi iendelee!!
Naunga mkono hoja jamaa aliweza sn hii wizara
 
Ishu ni fadhila sio professionalism kwa sasa😅 kwahio jiandaeni kuitwa Sukuma Gang!
 
Mh. Rais kwakumuondoa Mchengerwa umetukosea sana watumishi wa Nchi hii... Ndani ya Muda mfupi aliohudumu katka UTUMISHI mambo mengi yalibadirika na watumishi walifurahi.. Sasa huyu Mwanamama uliemleta hatufai ata bure sijui ninani aliekushauri utuletee Huyu.. Huyu Muhagama ni Bendera fuata upepo tu kwanza uyu nahisi nae ni Sukuma Gang tunakuomba utuondolee uyu Muhagama uwezo wake ni mdogo sana hana ushawishi wa kuwaagiza maafisa Utumishi miungu watu kwenye maofisi... Mh Rais tunakuomba sana Muhagama ni Big No
HR's wote walishika adabu
 
Huyu mheshimiwa alifiti Sana na ailitenda haki kwenye ile wizara, Rais wetu mpendwa unaesikiliza wananchi wako tunakuomba, tunakusihi mrejeshe huyu mheshimiwa kwenye ile wizara, huyu mwingine mpeleke kwingineko. Tunakuomba Sana Rais wetu.
Aliweza sn hiyo wizara sema bibi ushungi sijui anawaza nini?
 
Kweli Mhe Mchengerwa amesemewa na kupiganiwa sana kwenye makundi mengi juu ya kubadirishwa kwake Wizara. System na Mamlaka zitakuwa imesikia na itapima faida na hasara za kufanya mabadiriko ndani ya muda mfupi na haitakuwa mara ya kwanza. Mnakumbuka yule aliepata msituko na kushindwa kusoma Kiapo na hivyo kushindwa kuapa Uwaziri Ukayeyuka.

Hata hivyo kuna mazuri na sio mazuri kwa Uongozi wa Pamoja na kulinda Hadhi na Staha za Viongozi wa Nafasi Zingine katika Muundo za Serikali baada au pamoja na Wizara ambazo Mawaziri na Viongozi katika Nafasi Hizi zingine hawanabudi kuzingatia katika kutoa kauli/ matamshi mbele ya Umma ,Wananchi, au na Watumishi. Unaweza ukawa unawafurahisha Wanaokusikiliza lakini unawaondolea Imani na kupokelewa kwa Viongozi Wengine.

Ningeweza kutoa mifano ya kauli hizo tata lakini nitakuwa nina mlenga Kiongozi husika Moja kwa Moja. Mhe Mchengerwa kuna Kauli alizitoa zinavutia na kupendwa na Watumishi lakini wakati huo huo zinabomoa taswira ya Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Idara/ Taasisi hata kama zipo sawa kisheria na kanuni za kiutumishi. Ngazi mbalimbali za serikali zinafanya kazi kwa Consultation na Mawasiliano ya Ndani Kimaandishi na sio kutoleana Decree Kadamnasi.
 
Bora Mchengerwa alikuwa anawapigania sana watumishi.

Lkn alikabiliwa na VITA ya MAJUNGU na FITINA kama kawaida wapiga majungu ndani wana nguvu sana.

Kama unataka udumu na upande basi jifunze kupiga majungu na fitina.

Hii tabia aliikemea wazi wazi Mhe. Mchengerwa lkn wanachama wa majungu na fitina wakajibu mashambulizi dhidi yake.
Hii tabia inapaswa ikemewe vinginevyo ni hatari kwa ustawi wa taifa.

sasa kila mmoja akiwa mpiga majungu na fitina tutasonga kweli?!
 
Tunataka Mchengerwa arudi! Mtu anafanya kazi vizuri mnamtoa! Kweli ngozi nyeusi Bado tuna safari ndefu! Hivi huyu jenista sijawahi ona la maana alilofanya, bungeni alikuwa ni mama wa kuwawekea wenzake mapingamizi.....taarifa spika,.....taarifa! Leo wanamuweka Wizara nyeti inayodeal na watumishi! Bure kabisa!
 
Huyo maza ana kazi maalumu ya kudhibiti ongezeko la mishahara, kikokotoo kurudishwa na hapandi mtu daraja.
 
Mchengerwa Smart Sana
Alianzisha utaratibu wa App ya Mtumishi unawasilisha Kero yako moja kwa moja na unajibiwa (e-mrejesho, e- Malalamiko)
Mkuu naomba link ya hiyo app,nina mengi yananiandama.
 
Mama chonde chonde, nakuomba tena kwa kusisitiza sana, mrejeshe Mohammed Mchengerwa Wizara ya Utumishi. Huyo bwana hapo alikuwa smart sana na alijitahidi sana kushughulikia na kutolea ufafanuzi kwa ufasaha kabisa masuala ya kiutumishi.

Huyu kipaza sauti uliyemleta utumishi naomba arudi huko kwenye sera na siasa nyingine. Mhagama ni mpiga mayowe tu na hawezi kujenga hoja, atasababisha uchukiwe bure na watumishi.

Mchengerwa ni smart sana ambaye ameanza vizuri, hupaswi kumkatisha tamaa kwa kupeleka huko.

Yule anatakiwa Utumishi au TAMISEMI. Very smart

Mwisho rekebisha jina la Wizara ya Gwajima hasa pale kwenye Wanawake na Jinsia hapajakaa vizuri maana neno jinsia linatisha sana

Kazi iendelee!!

Naunga mkono hoja, Mohammed Mchengerwa is the best of the best kiukweli..
Huyo bwana ni kiongozi mzuri sana..

Mungu ajalie, Mama Samia amrudishe Utumishi kwa kweli..

Mchengerwa ni kati ya Mawaziri bora kabisa ambao bila shaka hata kidogo wanamsaidia sana Mh. Rais..

Mama yetu Rais wetu Mh. Samia, tunakuomba sana jamani, mrudishe huyo Mh Mchengerwa Utumishi..
 
Back
Top Bottom