Nini hasa kilijiri mpaka Luteni Jenerali Imran Kombe akauliwa na Askari Polisi?

Huyu Mzee nakumbuka ilikuwa siku ya jumapili nilikuwa kituo cha tax sokoni moshi mjini. Tumetulia tunapiga stori zetu kusubiri abiria mara tukaona Nissan patrol nyeupe inapita mwendo kama wa 5km hivi mdogo mdogo. Tukasema hayo ndio maisha wenzetu wanayafurahia. Dah! Baada ya muda kupita taarifa zinatufikia kuna jambazi White kauwawa na ndio alikuwa na lile Nissan, wengi watu wa moshi tulioiona ile Nissan kabla ya tukio tulipagawa, sababu White alikuwa ni kijana na anajulikana sana na watu wa pale Moshi, na yule aliekuwa na ile Nssan alikuwa anaonekana sababu vioo vilikuwa wazi na havina tinted. Wengi tuliposikia White kapigwa risasi kwenye ile Nissan tulijua kwamba yule Mzee kaibiwa gari na White na ndio akawahiwa kupigwa risasi.
 
Mambo kama "Corridors of Power" au KITENGO na kadhalika ni masuala mazito sana.

Uzito huja baada ya mtu kukiuka misingi ya kuwepo masuala hayo mawili.

Kwenye viambaza vya utawala yaani "Corridors of power" kuna mambo mengi sana yanotendeka na sio tu yawahusu wanasiasa.

Mambo haya yanahusu uwezo ulo juu ya masuala kama maisha binafsi, familia na hata ushirikiano baina ya nchi jirani.

Maeneo hayo mawili yaani viambaza vya utawala na sehemu ya Kitengo vinashiba chakula kinachotoka kwenye taarifa kama za ujasusi ndani ya dini, hadhara na hata duru za Freemason.

Ujasusi barani Afrika umebobea sana kwenye hayo maeneo matatu na kila code inatumika hapo.

Nafikiri serikali ililipa fidia ya 600 milioni ambayo mahakama kuu chini ya jaji Mchome iliamuru zilipwe na mjane wa marehemu Roseline na mwanae Sheila sasa wanaishi kwa amani ingawa wamemkosa mzee Kombe.

Mwenyezi Mungu airehemu roho ya Marehemu Luteni Jenerali Imrani Kombe shujaa wa vita vya Kagera vya kumng'oa nduli Amin.
 

Mkuu heshima yako.

Mimi nafikiri baada ya Ladwa kusema kwamba kulikuwa na 1.5 millions tayari kwa atakaewezesha kukamatwa kwa jambazi wa gari hilo na gari yenyewe kugombolewa, basi motive ya hao jamaa wa DSM ilikuwa ni kumkamata na kumuua huyo jambazi haraka iwezekanavyo.

Hivyo hapo misingi ya kipolisi kiutendaji ikawekwa pembeni.

Fedha ni shetani sana na khasa kwa wale wenye tamaa na uroho.
 

nenda uganda kilicho mfanya kama huyo umekijua
 
Tuna watu hatari sana humu jf
Kwa lugha na matamshi yao wanajitambulisha ni akina nani wao
Shikamoo jf
 
Kwani sponsor alikuwa nani wakati ule si mzenji ?
 
Hii nayo ni kona ambayo unaweza toka nayo na ika sound
Ila duh ... hatari sana haya mambo
 
Kiraracha ni nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…