Nini hasa kilijiri mpaka Luteni Jenerali Imran Kombe akauliwa na Askari Polisi?

Nini hasa kilijiri mpaka Luteni Jenerali Imran Kombe akauliwa na Askari Polisi?

Huyu Mzee nakumbuka ilikuwa siku ya jumapili nilikuwa kituo cha tax sokoni moshi mjini. Tumetulia tunapiga stori zetu kusubiri abiria mara tukaona Nissan patrol nyeupe inapita mwendo kama wa 5km hivi mdogo mdogo. Tukasema hayo ndio maisha wenzetu wanayafurahia. Dah! Baada ya muda kupita taarifa zinatufikia kuna jambazi White kauwawa na ndio alikuwa na lile Nissan, wengi watu wa moshi tulioiona ile Nissan kabla ya tukio tulipagawa, sababu White alikuwa ni kijana na anajulikana sana na watu wa pale Moshi, na yule aliekuwa na ile Nssan alikuwa anaonekana sababu vioo vilikuwa wazi na havina tinted. Wengi tuliposikia White kapigwa risasi kwenye ile Nissan tulijua kwamba yule Mzee kaibiwa gari na White na ndio akawahiwa kupigwa risasi.
 
Mambo kama "Corridors of Power" au KITENGO na kadhalika ni masuala mazito sana.

Uzito huja baada ya mtu kukiuka misingi ya kuwepo masuala hayo mawili.

Kwenye viambaza vya utawala yaani "Corridors of power" kuna mambo mengi sana yanotendeka na sio tu yawahusu wanasiasa.

Mambo haya yanahusu uwezo ulo juu ya masuala kama maisha binafsi, familia na hata ushirikiano baina ya nchi jirani.

Maeneo hayo mawili yaani viambaza vya utawala na sehemu ya Kitengo vinashiba chakula kinachotoka kwenye taarifa kama za ujasusi ndani ya dini, hadhara na hata duru za Freemason.

Ujasusi barani Afrika umebobea sana kwenye hayo maeneo matatu na kila code inatumika hapo.

Nafikiri serikali ililipa fidia ya 600 milioni ambayo mahakama kuu chini ya jaji Mchome iliamuru zilipwe na mjane wa marehemu Roseline na mwanae Sheila sasa wanaishi kwa amani ingawa wamemkosa mzee Kombe.

Mwenyezi Mungu airehemu roho ya Marehemu Luteni Jenerali Imrani Kombe shujaa wa vita vya Kagera vya kumng'oa nduli Amin.
 
Ilijulikana Kuwa aliuawa na waliomuua Kwa Kuwa wauaji walikosea target Mke wa Marehemu aliekuwa Na Mumewe wakipeleka Migomba shambani alifanikiwa kujificha asionekane wakati wanamtafuta na alifanikiwa Kwa Kuwa alikuwa ameshiriki Mafunzo Mengi ya namna ya kujilinda aliyokuwa amepitia wakati Mumewe akiwa Mnene wa Kijitonyama otherwise tungekuwa tunasema kauawa na wasiojulikana

Mke alitambua mpaka force number Za wahusika bila ya wao kujua na ndie alikuwa shahidi muhimu kwenye Mimbar Za Mahakama!

Wauaji wanadai walimuua Kwa kufananisha gari yake na gari iliyoibiwa japo hapakuwa na taarifa zozote zilizowahi kurepotiwa Kuwa kuna gari imepotea

Hata Kama gari iliibiwa na Mwizi Mwenye Umri zaid ya Miaka 60 Baada ya kustaafu aliwazidi Mbio Za kumdhibiti Baada ya kushuka kwenye gari na kuanza kukimbia hadi wakaona Waache gari waliyokuwa wanaitafuta na kuanza kumimina Risasi 14 kwenye kifua kutokea Nyuma na inaonekana risasi hizo zilipigwa umbali wa mita zisizozidi 10 kutokana na kipenyo ( matundu) kwenye Mwili wa Marehemu Kuwa madogo

Mahakama ilithibitisha Pasi na Shaka Kuwa aliuawa Kwa makusudi ndio sababu wauaji walihukumiwa kifo, kitendawili kimebaki sababu zipi zilipelekea akauawa?

Mkuu heshima yako.

Mimi nafikiri baada ya Ladwa kusema kwamba kulikuwa na 1.5 millions tayari kwa atakaewezesha kukamatwa kwa jambazi wa gari hilo na gari yenyewe kugombolewa, basi motive ya hao jamaa wa DSM ilikuwa ni kumkamata na kumuua huyo jambazi haraka iwezekanavyo.

Hivyo hapo misingi ya kipolisi kiutendaji ikawekwa pembeni.

Fedha ni shetani sana na khasa kwa wale wenye tamaa na uroho.
 
Wakuu wa jukwaa hili, ni takribani miaka 22 sasa imepita tangu Mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Usalama, Meja Jenerali Imran Kombe alipouwawa na askari polisi mkoani Kilimanjaro.

Mengi yamezungumzwa, je ni nini kilitokea na kujiri mpaka 'deep state' ikaamua kumnyamazisha aliyekuwa boss wao?

Karibuni kwa mjadala wakuu, kama hujui basi usilete masihara.

nenda uganda kilicho mfanya kama huyo umekijua
 
Mtu ambae anakimbizwa Na akapigwa Risasi akijaribu kukimbia Sio rahisi kupigwa Risasi ya kifuani Kwa mbele

Ukisikia story Kuwa alipigwa Risasi Kwa mbele maana yake inatengenezwa Mazingira ionekane alikuwa anakabiliana nao wakaona wamuwahi

Yule Mama hakuwa target no. 1

Huwezi kuanza kufanya jitihada Za kuficha ushahidi kabla ya kufanya uhalifu

Kwanz unafanya uhalifu then unaficha ushahidi kwenye kuficha ushahidi inawezekana ukachemka kutokana na Mazingira Na extent ya uhalifu uliofanya
Tuna watu hatari sana humu jf
Kwa lugha na matamshi yao wanajitambulisha ni akina nani wao
Shikamoo jf
 
Doh! Kama ali surrender na bado wakamweka chuma it means aliwekwa za kifuani Sasa!

Kumbe alikuwa na mgombea wake mfukoni, ndio kilicho mcost. Ila hapo kuna utata kidogo huyo Che nka angeweza vipi ku injinia hiyo kitu wakati na yeye ndio alikuwa anaanza kuingia ofisini? Kwangu Mimi Naona hiyo 95 mzee wa kiraracha alikuwa ana connection kwenye system kuliko huyo Che nka..sasa aliwezaje kuamuru mtu aondolewe wakati hakuwa na mizizi kule?
Kwani sponsor alikuwa nani wakati ule si mzenji ?
 
Vipi kuhusu President Slim wa nchi jirani kuhusika katika mauaji.

Kombe akiwa DG wa Idara, alikuwa anajua kinachoendelea kuhusu mipango ya Slim kutaka kufanya mapinduzi nchini mwake.

Kombe aliwashauri Marais wale wasipande ndege moja wakiwa wanatoka Dar Es Salaam lakini wakawa wabishi, kilichowakuta kila mmoja anajua.

Hivyo kuna wanaoamini Slim alimfanyia faulo Kombe ili kupoteza ushahidi, na ukizingatia Kombe alishapoteza kuaminiwa na wakuu wake, hivyo ikawa kazi rahisi kwa Slim kufanya yake.
Hii nayo ni kona ambayo unaweza toka nayo na ika sound
Ila duh ... hatari sana haya mambo
 
Ukiwa kwenye baadhi ya idara lazima ujue maisha yako yote umeapa kutumikia serikali na sio yeyote yule. Sio kabila lako.

Kama kweli marehemu alihusika kupeleka siri kwa mzee wa kiraracha basi alikuwa msaliti. Wababe wa biashara za hatari wanawaita 'rat' wasaliti wa namna hiyo.
Kiraracha ni nini ?
 
Back
Top Bottom