Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Wale walikuwa waislamu wewe na mohamed said mnapotosha mpate huruma ya Umma.
Wwe ndio unapotosha ambacho hufahamu ni kwamba walikua wanakamata kamata kila anayekatiza ile mitaa kwa ile wiki nzima na kuendelea sasa wangejuaje dini ya mtu kijiweni?? Kuja kuconfirm 1/3 ni wakristo ikabidi watenganishwe hata mahakama ili wakristo waende kivukoni huko wakapewe dhamana ila waislam wakaenda kisutu wakamyimwa dhamana. Na haya mambo yamekuwa documented so kaconfirm ndio uje kubisha humu.

Nachokiona watu humu hawana uelewa wa kilichotokea so mnacomment kwa hisia tu bila facts

Anyway naomba unisaidie unapokamata watu kariakoo pale unawezaje kujua huyu ni muislam hyu ni mkristo kwa MACHO??

Nasubiri jibu

Cc Hammaz
 
Sasa kosa lao lilikuwa lipi?? Unajua inaonekana unachangia bila kujua story nzima.

Embu niambie hapa kosa lao lilikuwa lipi?? Kwenda kudhamini wenzao waliokamatwa msikitini ule usiku?? Kwani polisi walishindwa nini kuzuia maandamano kwa kuwaita masheikh kuwatuliza kama wanavyoitaga Wanasiasa kuwazuia wamachinga au bodaboda wakiandamana??

Embu naomba uniambie kosa lao ni lipi?? Au ni hearsay ya Yule padri?? Na kwanini wasipelekwe mahakamani tu hadi wapigwe risasi kuua?? Rubber bullets hazikuwepo??

Mnanishangaza
 
Kabla hatujaenda mbali,wewe ulishawahi kukamatwa na police ukawekwa ndani ikihitajika dhamana kutoka kwa jamaa zako?
 
Mtoto wa watu Akwilina nae aliingia kwenye 18 za hao hao polisi.
 

Acha Ujinga, Taifa gani alilojenga? na udogo wa Taifa la Nigeria ni nini?
 

Mohamed Said ww Ni mmoja wa waisilamu ninaowakubali sana hapa jukwaani, pamoja na kuwa na imani tofauti na ww lakini huheshimu sana michango yako iliyoshena ustaarabu mwingi na elimu tele.
 
waweza nifafanulia huo 'u-con-artist' wake ili niweze kuelewa upande wako?
Umekwisha msoma na kumuelewa aliyoandika?
Kama huna uwezo wa kuchambua maandishi kama hayo, nitakachokiandika mimi hakiwezi kuwa na msaada wowote kwako.
 

KADA WA CCM KWENYE UBORA WAKO
 
Ngoja nikuambie kitu.
Hawa watu, Sudan wapo. Egypt, wapo, Pakistan, wapo. Hata Saudi penyewe wapo na kote huko hushikishwa adabu zao.

Huyu mzee hapa ka-'thrive' kweli kwa taarifa zake za upindishaji na kuwapata watu wanaomwona kama mtaalam sana. Ukimsoma vizuri utaona katika maandishi yake yoote, ni ya kupindishapindisha taarifa na kutafuta majina makubwa kuhalalisha anayoyaandika ili watu waamini anachoandika.

Akishabanwa na uongo wa maandishi yake unapogunduliwa, utaona anasogeza au anabadili msimamo kiaina. Siku hizi imembidi akubali uongozi wa Mwalimu Nyerere tokea huko nyuama. Ukimsoma alivokuwa akiandika juu yake huko mwanzo, tadhani Mwalimu hakufanya kazi yoyote katika uongozi wa kuleta Uhuru wa Tanganyika.

Anasimulia hadithi za kuambiwa na kuziongeza chumvi anavotaka yeye ili kuchota akili za watu wanaomtegemea katika upindishaji wa habari nyingi.

Akibanwa kwenye udini anaoutumia kwa maslahi ya kujijengea jina, utamwona akiruka na kukataa kuwa yeye huko hayupo. Ndio maana mimi namwita ni tapeli aliyekubuhu.

Misingi ya kidini anayoisimamia, ndiyo hiyo hiyo anayomlaumu Mwalimu Nyerere kuibaini na kuiondoshea mbali mapema kabisa; na ndio sababu kuu ya yeye na wanaomkubali huyu mzee kumchukia Mwalimu Nyerere. Na kama hali ile waliyoitaka, ya dini na siasa ziambatane isingestukiwa kungali mapema, nchi hii sasa hivi ingekuwa ni tofauti sana na ilivyo sasa.

Maajabu ni kwamba bado wanayo matumaini kwamba siku moja hali hiyo inawezekana kuletwa hapa Tanzania!
 
Kabla hatujaenda mbali,wewe ulishawahi kukamatwa na police ukawekwa ndani ikihitajika dhamana kutoka kwa jamaa zako?
Mkuu twende kwa hoja mambo personal hapa hayana nafasi whether nimewahi kaa selo au lah haibadilishi ukweli kuwa kwenye kamata kamata za polisi huwezi tambua mkristo na muislam kwa macho.

Kwa taarifa tu ninao watu naowafahamu takribani kumi ni wakristo na waliwekwa ndani kwa kesi ya mwembechai so naongea kitu nachofahamu sio kuhisi au kubahatisha.

Sass naomba wewe unieleze ukikamata wati kariakoo utajuaje nani mkristo nani sio??nisaidie hapa
 

Hivi wewe ni muislamu? Swali la kwanza tungeanzia hapo
 

Kwa hali hiyo ni maana hupo tayari kufahamu ukweli
 
Umekwisha msoma na kumuelewa aliyoandika?
Kama huna uwezo wa kuchambua maandishi kama hayo, nitakachokiandika mimi hakiwezi kuwa na msaada wowote kwako.
hizi ni kauli za mtu anayejua fika hawezi shindana na mtu kwa hoja stahiki maana yeye nishazisoma hoja zake ila wewe mpk sasa hujaweka hoja zako wazi kuthibitisha upungufu wa hoja zake.
hata kama ni kweli huyo mzee ni 'con-artist' hakuna mtu mwerevu atakayekuamini kwa namna hii
 
ArIeN,
Huyu Kalamu hana moja alijualo katika hii mada.

Namwekea taarifa nyingi zimsaidie yeye kuelewa bahati mbaya anapandisha hasira na kutoa kejeli.

Mimi licha ya kuwa naandika historia ya wazee wangu na nimeishi ndani ya historia hii nimefanya utafiti na kuandika kitabu kizima sasa kipo mwaka wa 20 kinasomwa na kinakwenda toleo la 4.

Haya yote bado hayajamtanabaisha amebaki na ghadhabu na ukaidi.
 
Basi baki humo humo kama ulimwelewa yeye, kwani kuna shida gani.
 
Tunatofautiana upeo & fikra mzee...tuvumiliane tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…