Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Ukitaka kuelewa kitu kwanza uwe neutral...ukiwa na notion ambazo ni basis kwako huwezi kupata somo na kuelewa.

Mbili.. Kuelewa uhusika wa huyo unayemtaja huwezi kuulezea kwakuwa huwa nyuma ya pazia kwakuwa nao wanaakili na wanafikiri kama wewe..

Tatu; unaweza kukubali kuwa miaka hyo kuliibuka vikundi vya mafunzo vya karate kila nyumba ya ibada lakin nikiuuliza nani ni intiator na progandist wa hyo kitu kuweza kuenea kila mahali ....hakika hutakuwa na jibu.

NNE; unaposoma kitu kutafuta ukweli angalia na historiography...nani kaandika hiko unachokisoma. Tafuta na wa upande ule wanasemaje kuhusu kitu hichohicho.

Tano; ukiweza kuwa na ufahamu wa kuunganisha dot utaweza kufahamu kujua nini kitatokea. Tutasema upo logical
 
Aroon,
Ukitaka uchangie vyema ungekisoma kitabu ukajua Prof. Njozi amesema kitu gani labda ungeelewa na sababu kwa nini serikali ikakipiga marufuku.

Kuchangia kitu ambacho hukijui si busara.

Hiki kitabu kipo hapa mtandaoni pdf.
Mpaka kimepigwa marufuku ,means kina biased sana , hivo kuleta uchochezi, siku zote waislamu ni watu wa kulalamika , hili swala LA machafuko ya mwembechai, hata Mkristo akilielezea ni tofauti na mwislamu , ushahidi ni kwenye Comment humu ,

Hivo hata hicho kitabu cha prof.njozi Muislamu lazima tu awe ame base upande wa Uislamu kuonesha Walionewa.

Niipongeze serikali kwa kukipiga marufuku.
 
Sio rumours mambo mengi yalikuwa yanaendelea
Mkuu nilitegemea as a great thinker ungeelezea walau kidogo ukweli huo ambao waislam walidai iundwe tume huru kuchunguza mauaji yale lakini hakuna tume yoyote hadi leo, badala ya kuwaita waislam kwa majina yote mabaya mngetumia muda huo kuainisha ubaya wao na walau ushahidi kidogo.
Nimefwatilia post zako kwenye uzi huu ila sijaona hata hoja ya msingi zaidi ya maneno ya kejeli kwa waislam tu, nakusubiri uje na hoja walau 2 ukiwa na ushahidi kuhusu tukio lile la KINYAMA dhidi ya waislam.
 
Chinchilla,
Inataka utulivu uelewe sababu ya tatizo lile.

Nimetoa mhadhara mzima Chuo Kikuu Cha Johannesburg kisha Islamic Propagation Centre International Durban na hiyo paper nimekuwekea hapo juu.

Bahati mbaya haijafasiriwa kwa Kiswahili.

Ukiisoma utapata majibu mengi na si lazima ukubaliane na mimi lakini utajua mengi.
 
Mauaji ya mwembechai yalikuwa ni kilele cha kilio cha waislamu juu ya ubaguzi dhidi yao wa siri na dhahiri katika nyanja nyingi hususan elimu na ajira serikalini, Serikali ya Mwalimu haikufanya vya kutosha kubridge gap kati ya Wakiristo waliokuwa na advantage kielimu toka wakati wa mkoloni. Hata shule za Kanisa ambazo Nyerere alitaifisha kwa hoja kwamba Watanzania wote wasome haikusaidia kwa sababu gepu la kielimu liliendelea. Na badala ya Nyerere kujenga shule mpya nyingi yeye alitaifisha zilizokuwepo ambazo bado ziliendelea kuwa chache na ndiyo maana watoto walikuwa wakifaulu primary school hawachaguliwi kutokana na uhaba wa shule za Sekondari.

Viwango na idadi ya waislamu chuo kikuu ilikuwa ni ndogo sana na serikali ya Nyerere na ya Mwinyi ambayo iliendelea kuwa under watch kali ya Nyerere kama Mwenyekiti wa CCM hadi mwaka 1990 haikuweza kuaddress tatizo hili.

Mkapa alivyoingia madarakani alikuta tatizo hili limefikia peak, mihadhara ilikuwa ni sehemu mojawapo tu ya waislamu kufikisha grievences zao kwa serikali.
Mkapa akaona atoe kile chuo cga TANESCO morogoro kuwapa waislamu ili kupunguza gepu na kilio hiki cga waislamu kuwa marginalized kwenye elimu.

Alipoingia JK akafanya kazi nzuri sana ya kujenga shule za kata kila nchi, kwa hiyo waislamu wakaweza nao kuaoma kwa wingi na pia JK akapandisha hadhi vyuo vya advanced diploma na kuvifanya vitoe digrii kwa hiyo katika mazingira haya huwezi kuwabagua tena waislamu.
Katika ishu ya teuzi, Kikwete alijirahidi kuteua teua na waislamu kwa wingi kidogo ijapokuwa wakiristo overall waliendelea kuwa wengi.

Alipoingia Magufuli, amejaribu kurudisga nyuma mafanikio haya ya kubalance demography za taifa katika utumishi wa serikali.Teuzi za Magufuli zinanuka Udini.
Proportiaonally ukiangalia idadi ya ma RAS, MaDAS, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wenyeviti wa Bodi Waislamu ni wachache mno kulinganisha na proprtion yao katika hii nchi.
Kitila mkumbo kabla hajaenda CCM aliandika makala juu ya hili akasema ni muhimu kwa kiongozi kubalance demography za kitaifa ktk utumishi wa serikali.
Magufuli aishukuru sana BAKWATA na Sheikh mkuu, hawa wamekuwa kama nguzo yake kuu katika kutuliza munkari wa waislamu, lakini kiukweli lazima ukweli usemwe Teuzi za serikali y awamu ya tano zinanuka udini.

Na kama akishinda uchaguzi ujao akaendeleza teuzi za hivi basi ajue matatizo mengi ya utawala wake kupigwa vita sababu mojawapo ni yeye kushindwa kubalance force za demography kwenye watu wa kumsaidia kazi. Akimarginalize watu ajue pindi anapohitaji force za kumuunga mkono anaweza asizipate na kibaya zaidi inajenga chuki kali kwa wananchi ambao wanahisi wanatengwa
 
Hahahahahahahahahahaah Ajuza acha utani wewe na karate wapi na wapi hahahahaahh daaah
Mazigazi,
Tufanye mjadala wenye staha.
Katika 1970s Faiza ni bint mdogo.

YMCA vijana wengi wanacheza karate pale wakifunzwa na Mawalla.

Dar es Salaam ndivyo ilivyokuwa miaka hiyo.

Hapakuwa na haja ya kejeli ungeuliza tu nasi tungekufahamisha kwa adabu.
 
Laudate,
Tatizo la jamii moja kukandamizwa Prof. Njozi kalieleza kwa ushahidi katika kitabu chake.

Ingekuwa bora mkakisoma kitabu kwanza ndipo mje hapa kuchangia.
 
Hizi akili za kuangalia majina kwenye teuzi na kuhitimisha kuwa huyu ni mkristo,na yule in muislamu ama mpagani ama myahudi in za kipuuzi.
Ni jambo LA ajabu na LA kipumbavu kuangalia watumishi kwa misingi hiyo ya hovyo.
Mkimaliza kuangalia kwa majina ya kiarabu na kizungu mtakuja kwenye ukanda na ukabila na mwishowe tutajikuta hatuna Taifa.
Acheni malalamishi ya hovyo
 

Laiti wanaoteua wangekuwa hawaangalii majina hoja yako ingekuwa na mashiko
Ila tatizo uko too naive kudhani kuwa mambo yapo tu kama yalivyo na kwamba hakuna ill intention yoyote katika teuzi zilizojaa UDINI
Hizi hoja zenu za Kipumbavu za kujifanya eti hamjali DINI za watu kwenye teuzi mbona inapokuja kwenye UKANDA hamzileti?, mbona watu wa KASKAZINI wakilalamika teuzi hamsemi kuwa siyo ishu?
NCHI HII INANUKA UDINI NA NI LAZIMA UPIGWE VITA ILI TAIFA HILI KILA MMOJA AWE NA HAKI YA KULITUMIKIA BILA KUBAGULIWA!.
Unazungumzia kuhusu Majina ya Kiarabu na Kizungu, unfortunately hiyo ni reality Waislamu wengi wanatumia majina ya Kiarabu na wachache mno wanatumia ya kikabila na wachache zaidi wanatumia ya Kizungu kwa hiyo ni rahisi kuwabagua kama mtu ana dhamira ya ubaguzi
 
Kipuyo,
Hapana hayo usemayo si sawa.

Unapojadili jitahidi sana kuwa mtulivu na jaribu uongozwe na lugha nzuri ya kiungwana kwani ukiwa unatuoa maneno ovyo unauchafua mjadala.

Tanzania dini kubwa ni mbili tu na ndizo tunapojadili tunaziangalia dini hizi mbili.

Katika nchi hii Waislam hawawezi kuwa wana malalamiko kuwa wanabaguliwa kwa misingi ya Uislam wao mtu akaja na hoja ya Wapagani na Wayahudi.

Hawa hawako popote katika suala hili katika nchi hii.
Hii mosi pili hapana haja ya maneno kama ''upumbavu.''

Tunaijadili hapa ni watu naamini wenye staha zao sasa isiwe kushiriki katika mjadala ndiyo ikawa sababu ya wao kutukanwa.

Tatizo la dini si la kupuuza.

Ikiwa Waislam wanasema kuwa wanabaguliwa si kitu cha kupuuza kwani hiyo ni fitna kubwa inayoweza ikavuruga nchi yoyote duniani.

Si busara tukajificha katika dhana mbona haijatokea?
Taifa halijengwi katika dhulma na ubaguzi wa aina yoyote.

Taifa linajengwa katika misingi ya haki.
Tanzania tatizo si ukabila bali ni dini.

Ipitie katiba ya Tanzania uangalie inasema nini katika suala hili.
Hili si suala la majina ya ''Kiarabu,'' wala ''Kizungu.''

Hili ni tatizo zito linalotaka ufumbuzi wa haraka.
 
Missile...
Haiwezekani kuielewa ahadi ya Nyerere katika haki na usawa kwa raia wote kama alivyoahidi wakati wa kudai uhuru, hadi usome hotuba yake aliyoitoa tarehe 10 Desemba, 1962 katika Bunge wakati Tanganyika inakua jamuhuri.

Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislam na Wakristo.

Nyerere alifanya hivi labda akijua kuwa ingawa yeye alikuwa Rais Mkatoliki lakini alipata uongozi wa Tanganyika kwa msaada mkubwa wa Waislam wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nyerere alikuwa na haya ya kusema:

''Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa.''

Hii ilikuwa kauli ya serikali ya kudhihirisha nia yake njema.

Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini na kuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwa serikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebisha hali hiyo.
 
unaweza ukaweka link?
 
kwenye hizo kashi kashi Mazinge alipona kweli?
 
Ngoja nikumbuke maana nilijikuta nipo Kibaha na nimepotezana na bibi yangu hata sielewi nilifikaje tu!!!
 
unasema kuna wapagani,then unaeleza tena wananchi wana dini,mbona unachanganya mafaili wewe
 
Ile video ya Afande anaamrisha piga yule ilikua inasikitisha sana
Alipiga vinara wote wa Yale maandamano walitumika maaskari wadunguaji yaani snipers wa Taifa...na ule huwa ni uamuzi wa mwisho pale maandamano yanapokuwa ni ya kiuhalifu na hata kuleta mauaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…