#COVID19 Nini hasa lilikuwa kosa la Hayati Magufuli kwenye ishu ya COVID-19 ?

#COVID19 Nini hasa lilikuwa kosa la Hayati Magufuli kwenye ishu ya COVID-19 ?

Kama mabeberu ni wabaya why alitumia pacemaker iliyotolewa uingereza?? Yaani kwanini atumie mashine ya mzungu kusukuma damu ilihali chanjo zao hatumii? Kwanini asingeacha kutumia moyo bandia Ili ategemee mitishamba imsaidie?
Kwani alisema wazungu ni wabaya na kila kitu chao?
 
Kosa la Mwamba Magufuli lilikuwa kuwaacha Watanzania waendelee kujitafutia chakula chao cha kila siku wao na familia zao badala ya kujifungia ndani. Sasa wako hai yeye ameenda zake ndio wanamsema vibaya. Lakini, Historia itamkumbuka!!
 
...
Piga hesabu ya fedha kiasi gani nchi kama ya Uingereza imetumia....kuagiza barakoa, na za chanjo kwa wananchi wake! Je tungeweza? kama tungefungua mabahasha yanayoambatana na Declaration of Emergency....?

Niongeze tu, nchi nyingi zilibidi zifanye jitihada za kutengeneza chanjo na barakoa zao wenyewe badala ya kuwa na madeni makubwa kutoka China ambayo ndio ilikuwa, inazalisha Barakoa pamoja na Vipima au vipimio vya Uviko 19.

Je, kiuhalisia leo hii tungeweza kutoa pongezi kwa Rais SSH? tuwe wakweli tungeweza?

Hizi kampeni za kumfanya Hayat Rais kuwa alikosea na hivyo apewe tuzo la kukosea ni dhahiri mna chuki. Ni dhahiri hayo aliyoyakataa ilifinya mirija ya Unyonyaji.


Aluta Continua

....
Mkuu mbona unadanganya? Tanzania mbona tulipokea fedha za mkopo kupunguza madhara ya COVID 19 kwenye uchumi? More so aliyepokea hizo pesa ni JPM Sasa kivipi unapotosha kuwa hatukukopa kwa mabeberu?


2. Pia Barakoa mbona zipo zilizokua zinatengenezwa humu ndani mpaka za vitambaa Sasa ni pesa Gani ingetucost kutengeneza Barakoa kiasi tukope?

3. Nani alisema chanjo ilikua gharama? Mbona zipo zilizokua zinanunuliwa na benki ya Afrika AfDB ama zilizokua zinatolewa msaada kma Astrazeneca n.k. nani aliyesema ingebidi tukope kupewa chanjo? Kama hujui chanjo zimepanda bei mwaka Jana mwishoni ilihali COVID 19 ilishapotea lakini kipindi COVID 19 ipo hot Wala hazikuwa na bei kiasi zitufilisi uchumi.

Tuache kupotosha watu
 
Kwani alisema wazungu ni wabaya na kila kitu chao?
Ndio.... Alisema kama wanatupenda sana mbona hakuna chanjo ya UKIMWI? Akahoji kwanini hakuna chanjo ya kansa? Eti Leo hii watupende sana watuletee chanjo??

Cha kushangaza yeye alikua anatumia moyo wa plastic ulionunuliwa uingereza!!
 
Mkuu mbona unadanganya?
Lipi?
Tanzania mbona tulipokea fedha za mkopo kupunguza madhara ya COVID 19 kwenye uchumi? More so aliyepokea hizo pesa ni JPM Sasa kivipi unapotosha kuwa hatukukopa kwa mabeberu?
Kwanza kabisaaaa Sijataja Beberu, hayo ni yako
Pili, nimesema haku declare a state of emergency ambayo ingefungua mabahasha yanayoambatana nayo kusokomezwa na mikopo migumu
Loan for Debt relief, hiyo tayari inatosheleza kuona alichokataa Hayat ungekuwa ni mlolongo mrefu wa madeni juu ya madeni...Yaani unapata mkopo wa kupunguza madeni....ndio kukubali mkopo wa kupunguza makali ya maambukizo? c'mon!!
2. Pia Barakoa mbona zipo zilizokua zinatengenezwa humu ndani mpaka za vitambaa Sasa ni pesa Gani ingetucost kutengeneza Barakoa kiasi tukope?
Usipindishe nilichosema, nimesema kwa kukataa kufungua mabahasha yanayoambatana na declaration of emergency ambayo yangetulazimu kupokea mabarakoa kutoka nje yangetufilisi. Na aliyedai hayo na kuyaita makosa ni mleta mada....
ni kupinga njia za kitaalamu kama kuvaa barakoa na njia hizi zilisaidia kwa kiasi gani sehemu nyingine
....kikubwa vile ni kuondoa woga uliotanda. wakati huo. Asante lakini kwa kuonyesha upindishaji na upotoshaji alioonyesha RNA kwa kukubali Barakoa zilikuwepo.
3. Nani alisema chanjo ilikua gharama? Mbona zipo zilizokua zinanunuliwa na benki ya Afrika AfDB ama zilizokua zinatolewa msaada kma Astrazeneca n.k. nani aliyesema ingebidi tukope kupewa chanjo?

Je unataka kudai hata zoezi la kutoa chanjo sio gharama? Agai sijasema popote ilibidi tukope kupata chanjo. Nime suggest, kufunguliwa kwa mabahasha yanayoambatana na Declaration of Emergency yangefungua mabahasha yakusokokomezewa madeni kwa kupokea bila shuruti hata dawa ambazo baadae zimekuja kujilikana hazina au hazikuwa na uwezo wa kupunguza maambukizi sembuse kupunguza vifo?
Kama hujui chanjo zimepanda bei mwaka Jana mwishoni ilihali COVID 19 ilishapotea lakini kipindi COVID 19 ipo hot Wala hazikuwa na bei kiasi zitufilisi uchumi.

Weka hapa Chanjo moja ina/ili kosti kiasi gani tufanye hesabu za harak haraka tuone kama hatukuweza kufilisika!
Tuache kupotosha watu
Mpaka hapo sioni umefikaje kudai mie ndie napotosha watu! Sijaona wapi umejibu kuhusu Mada ambayo nayo imekaa kunyanyasa na kupotosha ukweli! Mbona hivyo wewe Zitto?
 
Ni vizuri
Nikuulize Swali Unajua Russian Roullette...

Unachukua pistol unaweka risasi moja unazungusha ile cyclinder chamber alafu mnapeana zamu kila mtu kujipiga risasi kichwani...,

Hata ukibahatisha usipokufa lakini gamble kama hio ni hatari ukiendelea namna hiyo uwezekano mkubwa kuna siku utateleza....

Maana yangu ni kwamba kuna mambo hayawezekaniki (total lockdown especially kwa nchi kama Tanzania) LAKINI tahadhari haimaanishi Total Lockdown pekee bali kuwa serious na kuacha mzaha......; In Hindsight kilichofanyika huenda kilikuwa better option, ila sababu hatukujua reaction itakuwa vipi kwahio haikuwa busara ku-gamble na jambo hatari ingawa baada ya kupata more facts ndio inabidi tu-act accordingly ila kabla ya facts kwa mambo ya afya ni vema kuwasikiliza wataalamu na hapa kwenye hili wataalamu ni watu wa afya na sio wanasiasa
Umejirudi....Hayati hakuwa mwanasiasa-that is a fact. Hayat alisomea taaluma iliyogusa Virusi.-That is a fact.

Hayat alikataa masharti na mashinikizo ya wazungu-that is a fact. A Spade is a Spade We can sugarcoat and be politically correct but the end of the day....it will remain a cultural war!

Again, iwe ni Mungu, Iwe ni Wataalamu, iwe ni wanasayansi, Ukweli unabakia kuwa Mzungu sio Mungu, Mzungu sio mwanasayansi pekee, mzungu sio mtaalamu pekee katika dunia ya wengi. Madai yenu mara ni Mungu, mara wanasayansi, mara ni wataalamu does not negate the facts that you're conveying a message of "He defied Authority" and that Authority is only bestowed by God to his Choosen Children....someni mnayoandika...mmejaa kudai "Supremacy" over the like of the late President....in reality you just playing with words short of saying "He shouldn't have to mess with a White man"

I know for a fact, you cannot even refute my argument, because it will just chip on your ego and take away one thing you hold dearly in your chain of thoughts.....That you are Supreme. And by refuting you become less....Anathema will devour you!

That said...

Well, not here in Tanzania. Hatutaweza kusujudu na kukubali utumwa mamboleo, kama mnavyodai kwenye jumbe zenu....'Hatutakubali Kamwe litokee tena Afrika au Tanzania"

Aluta Continua
 
Kosa la Mwamba Magufuli lilikuwa kuwaacha Watanzania waendelee kujitafutia chakula chao cha kila siku wao na familia zao badala ya kujifungia ndani. Sasa wako hai yeye ameenda zake ndio wanamsema vibaya. Lakini, Historia itamkumbuka!!
Yaani makosa yake ndio yamekuwa mazuri kwa Tanzania na Jamii? I:ll take that any day
 
Ila kuna watu ni wajinga na wabishi.eti wazungu ni wazushi kwa hiyo haya mfano internet,magari,madawa na jf ungeziona wapi ?
Unashindana na mtu amekupa unaishi maisha ujawai kufikiria alafu unabisha utazani wewe ndio muundaji.
Huo ndio Upotoshaji wenyewe.
Madai yako kuwa Mzungu ndiye alietupa maisha kwamba Mzungu ndio Muumba....yaani unadai Mzungu ndio Mungu? mbona hamsemi waarabu ndio waliowafundisha herufi, mbona hamsemi wahindi ndio waliowafundisha Hesabu, mbona hamsemi mbinu nzuri na bora za Kivita mmezitoa Afrika Uchina?
Mbona hamsemi hayo madawa mnayotumia mnayatoa katika misitu yetu? Jitathmini,
 
Corona ilikuwa threat kwa watu wenye magonjwa nyemelezi, kwa hiyo alitakiwa kuwaambia watu endapo utajisikia hovyo wafike haraka hospitali kupata matibabu badala ya kuhimiza watu kutumia miti shamba kujitibu aka nyungu, badala ya kusema "hivi vi mafua fua lini viliuaga mtu wagoshaaa hiiii...."
Mbona Marekani na Nchi nyinginr ulaya zilikuwa zina shawishi kuwasha nyungu Kwenye chumba chako? Unajua ni Vyombo vingapi vilivyoanzishwa na teknoljia ya nyungu?

Huwezi ukaenda hospitali ukadai una Covid bila ya kuulizwa kama una mafua? au la au Una homa? Kikohozi? n.k msibadilishe lugha aliyotumia.

Mnabeza
 
Reaction ya JPM kwny gonjwa la Corona anastahiki alama zote I.e mia fil mia

Allah alimpa ilhamu ya hali ya juu sana …alipata ujasiri na uthubutu wa hali ya juu sana kuliko wasomi, watabiri na waganga na waganguzi

Kile chuma kilikuwa na flavor yake ya kipekee sana hata Julius angekuwepo kuna mambo angetakiwa ajifunze kwa yule Mwamba


nime miss sana zile hotuba za kutoka moyoni ambazo ndio hasa za Rais

Ma Rais wote walikuwa wanahutubia Hotuba za Ikulu kasoro John peke yake ndo alikuwa anatoa hotuba zake mwenyewe …hata Julius Hotuba zake nyingi zilikuwa zinehaririwa na yule Katibu wake Bibi wa Kiingereza
Watu waliendelea kuambukizwa na kufa kwa ugonjwa huo ambao pengine wasingepata na kufa.Mbinu alizotumia zilikuwa za hovyo sana kukubali watu wake wafe hadi kinga itaporejea.Ni jambo jema sana naye ilimuondoa ili aungane na wahanga wengine wa uamuzi wake wa ovyo
 
Corona ni hatari sana mkuu ,kama afya mgogoro unaweza usitoboe ikikukamata! Kinga ikiwa juu unaweza kuithibiti.

Kosa lake ni kutowaambia ukweli waTZ hasa wale wenye kinga ndogo na wenye magonjwa nyemelezi wachukue tahadhari hasa.
 
Ndio.... Alisema kama wanatupenda sana mbona hakuna chanjo ya UKIMWI?

That is a valid Question. Maswali hayo yanaulizwa leo hii na Jamii zilizoathirika ma Ukimwi. Maswali hayo yanaulizwa na Madaktari wengi, hata viongozi wengi Duniani...Kwanini?

na sababu kubwa ya kuiliza hayo ni muonekano wa hatua kubwa iliyopigwa katika utafiti wa Chanjo na madawa mengine ya kutibu magonjwa Sugu kama Ukimwi...Jiulize kwa nini teknoljia hiyo iliyotumika isitumike kwenye Virusi vingine kama virusi vya Ukimwi?

Mpaka sasa, Uwezekano wa Chanjo hiyo Upo....
Akahoji kwanini hakuna chanjo ya kansa?
Hata Joe Biden wa Marekani ameuliza hayo Kwanini? na Ametangaza kufikia miaka michache baaadae makampuni ya dawa yawe yamefanya hivyo, akiwa anamaana anajua Teknolojia ipo!

Eti Leo hii watupende sana watuletee chanjo??
Kweli kabisa, yaani watupende tu wakati historia inaonyesha Udhalimu na Uhasama dhidi ya wote wasiofanana nao?
Cha kushangaza yeye alikua anatumia moyo wa plastic ulionunuliwa uingereza!!
....Aisee, hoja yako ni nini haswa?
 
Watu waliendelea kuambukizwa na kufa kwa ugonjwa huo ambao pengine wasingepata na kufa.Mbinu alizotumia zilikuwa za hovyo sana kukubali watu wake wafe hadi kinga itaporejea.Ni jambo jema sana naye ilimuondoa ili aungane na wahanga wengine wa uamuzi wake wa ovyo
Aisee, sijui unatoa wapi Taarifa zako.

Tunajua haikuwa Corona peke yake, Tunajua haikuwa Papa, Tunajua haikuwa 'mungu' wa upande usioeleweka,.

Tufukue kaburi?
 
Nimekuja hapa kuthibitisha ujinga wa watanzania wengi tu.
Dk Uchwara Molleli ndio kakupa silaha.

Peke yako huna uthubutu huo.

ili uweze kuwatetea watu wako, huwezi kuwaita wajinga, kwa kipuuzi kama Daktari Molleli

Huwezi kuwaita watoto zako wajinga kwa kipuuzi, kamwe huwezi.

Jitathmini ndugu yangu.

Amani
 
Kosa lake ilikua kukosoa mbinu za kisayansi hicho tu basi. Ilikua wazi kuwa COVID 19 ilikua hatari zaidi kwa wazee au nchi zenye baridi kuliko huku kwetu so Kulikua hakuna haja ya kukejeli efforts za madaktari, mara sijui Barakoa hazifai, mara chanjo zimetumwa kutuua waafrika n.k. nakumbuka Hadi anamkejeli Askofu kuvaa Barakoa eti hamuamini Mungu!!

Kuna wakati Hadi alikataa uwepo wa COVID 19!! Mimi binafsi manusura nimpoteze Mzee wangu aliponea kwenye mtungi wa oxygen alafu nawasha Tv naskia JPM anasema "hakuna COVID 19 hapa Tanzania...." Hapo unategemea waliopoteza ndugu kwa changamoto hiyo watamuelewa?
Unajirudi, halafu unapotosha, huku unadanganya.

Weka ushahidi wa hayo maneno au kauli uliyonukuu....alisema wapi hayo..."hakuna covid- 19 Tanzania" wapi?
 
Kosa lake ni kujua ubeberu unaoambatana na mbiu zinazopigwa mara kwa mara na shirika la afya duniani kwamba ni biashara kuliko hali halisi. Mnatiwa hofu ya hatari kuliko ukweli halafu mnauziwa kila takataka kwa bei ya ajabu. Tena bidhaa hizo mara nyingi sivyo mnavyoelezwa ni feki productcs kuwapatia faifa za kutisha kwa ukubwa. Zaidi ya hapo lockdowns za corona bila shaka ilikua mbinu kuharibu uchumi wa nchi nyingi.
And then kuna njama kubwa magufuli aliitambua. Hapa tz kuna watu walishajiandaa eti kusambaza chakula kwenye lockdowns. Niliwahi kuwasikia eti wangejitolea nikacheka kimyakimya.
Hawa magaidi unaowasoma hawawezi kuliona hilo. Mirija yao ilifinywa nywiii! Kalas

Zaidi ya matusi na Kejeli hoja zao hazishiki, ndio maana wanazunguka zunguka kutafuta sababu za kubeza na kejeli.

Umenena.

Kwa lugha nyingine, Ujumbe wameupata.
 
Kosa lake ni kuwaharibia mchongo ambao walikuwa wanatakiwa kuongeza panic katika jamii kwa kuripoti vifo vya uongo na kujaza mkeka wa COVID-19 uonekane kila siku unaondoka na watu.

Na pia wao wakifanya hiyo kazi walikuwa na mafungu yao ya pesa ili wapate mgao.
 
Reaction ya JPM kwny gonjwa la Corona anastahiki alama zote I.e mia fil mia

Allah alimpa ilhamu ya hali ya juu sana …alipata ujasiri na uthubutu wa hali ya juu sana kuliko wasomi, watabiri na waganga na waganguzi

Kile chuma kilikuwa na flavor yake ya kipekee sana hata Julius angekuwepo kuna mambo angetakiwa ajifunze kwa yule Mwamba


nime miss sana zile hotuba za kutoka moyoni ambazo ndio hasa za Rais

Ma Rais wote walikuwa wanahutubia Hotuba za Ikulu kasoro John peke yake ndo alikuwa anatoa hotuba zake mwenyewe …hata Julius Hotuba zake nyingi zilikuwa zinehaririwa na yule Katibu wake Bibi wa Kiingereza
Julis alikuwa anatoa madini kichwani hakuwa akisoma. Sijawahi kumuona akisoma.
Kikwete na mkapa na mwinyi ndio mara nyingi walikuwa wakisoma.
 
habari jf , JPM aliamini corona itaendelea kuwepo na tutaishi nayo kama yalivyo magonjwa mengine ,kiuhalisia ndivyo ilivyo corona ipo na idadi ya watu waliopata chanjo ni ndogo sana na watu walishapata kinga asilia sasa hivi sio tishio tena .lakini bado watu wakiwemo madaktari wanalaumu approach yake kwenye ishu .

Swali langu ni lipi lilikuwa kosa lake ?

Je, ni kutoweka lock down ?

Je, ni kupinga chanjo ?

Je, ni kupinga njia za kitaalamu kama kuvaa barakoa na njia hizi zilisaidia kwa kiasi gani sehemu nyingine ?

Kwangu Mimi mnyonge mnyongeni katika hili alistahili tuzo .
Lakini akafa kwa Corona hiyo hiyo. Aliamini sana ushirikina kuliko science.
 
Back
Top Bottom