Nini hatima ya Wakristo walio Zanzibar kwenye sherehe za Pasaka baada ya zuio la kula mchana wakati huu wa Ramadhan?

Nini hatima ya Wakristo walio Zanzibar kwenye sherehe za Pasaka baada ya zuio la kula mchana wakati huu wa Ramadhan?

Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.
Moyo wangu unaugua sana kwa sababu ya Jamii ya Wakristo wanaoishi katika visiwa vya Zanzibar.
Nawaza namna watakavyokula Pasaka. Ikumbukwe kuwa, Pasaka ndicho kilele cha Ukristo na kwa asili, Pasaka ni siku ya kuchinja na kula kusherehekea ukombozi wa Mwanadamu uliopatikana kwa Kifo cha Yesu Msalabani. Hivyo, kuzuiwa kula ni kuzuia maadhimisho ya kipasaka.
Si murudi kwenu Bariadi uko mkale iyo pasaka yenu
 
Sasa kama watu wa huko wanafurahia kuwagawa watu kwa misingi ya Dini.
Je,wanastahili kuteuliwa na kuchaguliwa kwenye nafasi za viongozi za Jamhuri...?

-Tukumbuke nchi ina wafuasi wa dini nyingi...
 
Nchi haina uhuru wa kula eti🤣🤣🤣 yaani unakula wenzio wakila🤣🤣🤣!
Kwani serikali Yao ni ya kidini??
Hii inamaana wanachuki mbaya na ukristo na hawana ustahimilivu kwa wengine!!
Kwakuwa bara wazenji wapo wengi tuu kwanini hii Sheria isitumike nahuku hususani tukijua amir jeda mukulu ni wakwao?? Jee, kutofanya hivyo si yuatenda dhambi??!
 
Hao jamaa huku Bara tunawakarimu ila ni wapuuzi na wabaguzi sana, Jumapili iliyopita pale Unguja Sheha kuna Kanisa kaenda eti punguzeni sauti watu wamefunga........ Jumapili ndiyo watanuna Zaidi
Tunapoelekea sio kuzuri, Mwisho wa siku utasikia wazanzibari wachomewa vibanda vyao Bara kwa kumaliza maeneo yao
 
Najua mnaoliza maswali Kama haya hampo Zanzibar,
Punguzeni chokochoko kwani Ramadan Zanzibar si tukio jipya na katazo la Kula hadharani si jipya.
Answar wanaowahi kumaliza mfungo kabla ya wengine wao huruhusiwa kula hadharani siku hiyo wakimaliza mfungo kabla ya nyie wengine??
 
Najua kama wana katiba yao...Lakini swali langu ni je,kuna mahala imenena kwamba Zanzibar ni dola Kiislam...?
Mkuu zanzibar imekuwa Chini ya Sultanite state Tangu miaka ya 800s ..

Mpka mwaka 1964 Ilipoungana na Tanganyika..
Miaka zaidi ya 1000s Zanzibar imekuwa ni Islamic state..

Na hata wareno "Portuguese" Walipofika East Africa mwaka 1498, where they found several independent towns on the coast, with Muslim Arabic-speaking elites.

While the Portuguese travellers describe them as "black Islamic Societies"..

Kasome Hiki journal..

Prestholdt, Jeremy. "Portuguese Conceptual Categories and the 'Other' Encounter on the Swahili Coast." Journal of Asian American Studies, Volume 36, Issue 4, 390..


Na usisahau kwamba zanzibar Ina sheria zake Licha ya kuwa Na Utamaduni wa Kiislamu kwa miala zaidi ya 1000s
 
Kama jaribu la kuvumilia jirani yako akila hadharani linakushinda utaweza kuvumilia ukiona upaja wa pisi kali? Jaribu dogo tu linateteresha imani yako.
😁😁😁😁😁😁 wapuuzi sana hawa
 
Kwani nani aliwaambia mkakae Zanzibar?Mnaambiwa Zanzibar ni Islamic state hamuelewi,kataeni muungano,acheni uchawa,fungukeni hamtaki mnaleta ushabiki,suluhisho ni katiba tu.Tukisema JKN alikuwa mnafiki na ndo chanzo ya yote haya mnamtetea haya sasa mm nitamkimbuka sana Oscar Kambona
Mimi nitamkumbuka Mtikila
 
lini ilikuwa Islamic state
Zanzibar Ilikuwa Chini ya Sultanite State..
Tangu miaka ya 800s mpaka 1964..

Lakini ilianza official kabisa kuwa Rely kwenye Muslim state ilikuwa ni miaka ya 1800s
Screenshot_20240329_095338_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom