Nini kilimpata Rais Magufuli akiwa anahutubia Ruangwa?

Nini kilimpata Rais Magufuli akiwa anahutubia Ruangwa?

Katika Lugha adhimu ya Kiswahili huwa hatuna neno la ' alikuwambia ' kama uliloliandika hapa bali tuna neno sahihi la ' alikuambia ' sawa? Jiimarishe Kwanza katika kuijua vyema Lugha ya Kiswahili na ukiona umeshaijua basi unaweza ukarudi tena Kwangu An Eagle a.k.a BRAINIAC ili niweze sasa kukujibu hayo Maswali yako ya Kitoto kama siyo ya Kipuuzi uliyouliza.
Jifunze kwanza kuandika vizuri kabla ya kujitia umajinuni wakati huna ndala mguuni.
 
Kwa elimu yangu ya ngumbaro na intelijensia ya kawaida kabisa ya kuzaliwa, huo mwanga ni kama reflection nahisi aliyekua anachukua video alikua kwenye gari au sehem kuna kioo.

Imeendelea kubaki hivyo na inaonekana ipo upande wa mchukua picha na sio kitu kilichokua kikitoa mwanga upande wapili.

Bado hii video haitoi jibu la taharuki inayoendelea, kuihusisha na ushirikina ndio kunazidi kuongeza tatizo.
The Monk himself
 
Hee! Unataka kutuambia moshi huo ni mlipuko wa battery ya ndani kwa ndani? Na kuwa ni sababu ya kusimama chini ya high voltage electric wire?
Kama ni hivyo hili jambo ni internal sabotage yaani "kikulacho ......"
Kwani watakuwa hawajui battery haitaki mvutano huo?
Aisee
 
Aliyekua anachukua video kwenye tv yake alikua kawasha na flashlight.

Ndiyo hiyo inatoa reflection ambayo baadhi ya watu wanadai ni radi. Which means ni uongo hakukua na radi.

Kuhusu moshi. Alikua anahutubia akiwa kwenye gari. Siyo jambo la ajabu gari kumalfunction na kuvuja moshi. Pengine ndiyo kilichotokea. Ila hii assumption nina asilimia nayo chache.

Ya hicho kimweku kinachodaiwa ni radi ninaamini ni flash ya simu kwa asilimia mia.

Mtu wa hivi hua hafi kama watu wanavyotaka.


Kwenye Radi Upo sahihi Mkuu.

Ila kwenye Moshi hapo kidogo kunaukinzani.

Unajua JPM ameuona huo moshi na akasema kabisa kuwa ni mambo ya wazee wa Luangwa.

Bahati mbaya Mchukua Kamera akaondoa haraka huku watu wakisogezwa
 
Huyo aliyeihariri hii clip ana lake jambo. ndiyo maana ameishia hapo na hakuweka mpaka mwisho. Inwezekena lilikuwa tukio la kawaida kabisa lakini kwa sababu mhariri clip alitaka kufikisha ujumbe kwa waamini nguvu za uchawi basi akaondoa sehemu zilizofuata.

Hajaihariri bali kaleta sehemu ndogo ya alichorekodi. Mpaka sasa nilikuwa naona hili suala toka lianze jana kama ni hadithi ya kuzua hivi, lakini kwa taharuki iliyopo kwenye jamii hata mimi naanza kupata mashaka. Nilikuwa naichukulia kama upotoshaji mwingine wowote wa mitandaoni na sisi wengine kutumia kama sehemu ya kufikisha changamoto zetu, lakini kwa sasa naona ni zaidi. Nadhani sasa ni muda muafaka wa serikali kujitokeza na kusema kulikoni.
 
Hasira za korosho hizi, Rais bado ana maadui wengi Mno. Ni vyema hili suala la korosho likaangaliwa kwa undani zaidi kuepusha majanga zaidi.

Naona Mh. Rais alikiri kabisa kuuona moshi na ukiangalia vizuri unaona Mh. alikuwa na hofu fulani, hata walinzi walianza kama kupanic kwa kujihami kwa kuimarisha ulinzi na kuanza kuwasukuma wananchi waliohudhuria eneo hilo.

Ni vyema serikali iangalie namna ya kumalizana na hao wazee wa huko ruangwa (Hapa Waziri Mkuu itabidi aonane nao, kidogo watamsikiliza) , kwani siku zote kurudia kosa ndio kosa, wawe na moyo wa kusamehe.
Kwanza haijathibitishwa kama Rais ni mgonjwa,
Pili hata kama ni mgonjwa, kwa nini tukimbilie kwenye ushirikina? Kwani watu hawaumwi?
 
Huo moshi sijui[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]Hao jamaa wanataka kumrestisha Jembe letu wale kichapooo[emoji35][emoji35][emoji35]
Hapo ndio huwa mwisho wa mabomu na risasi, kichapo utapiga raia wasio na hatia waket wenyewe wanakuchora tu.
 
Itafika mahala mikutano ya vijiji kwa vijiji njiani haitokuwepo zaidi ya wilayani au kwenye makao makuu ya mikoa.
Ziara nyingine za utekelezaji wa majukumu zitafanywa na Wakuu wa Mikoa na Wilaya,nguvu zaidi itaongezwa kwenye ufuatiliaji.

Hapo ndio tulipokuwa tunahimiza utendaji wa mifumo.
 
Back
Top Bottom