Nini kimesababisha mchango wa Waislamu katika harakati za siasa za mapambano Tanzania kuwa ukipungua ?

Nini kimesababisha mchango wa Waislamu katika harakati za siasa za mapambano Tanzania kuwa ukipungua ?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Kuanzia uhuru mpaka leo hii mchango wa Waislamu katika harakati za mapambano umeenda ukipungua sana.

Wakati wa uhuru Waislamu walikuwa active sana mstari wa mbele katika harakati za uhuru pamoja na Nyerere. Watu wengine kama Mohamed Said wanafikia mbali hata kusema Waislamu ndio walikuwa engine ya mapambano na kina Nyerere walikuwa body tu.

Waislamu waliendelea kutoa mchango mkubwa wa changamoto dhidi ya utawala hata na mapambano ya kuboresha haki hata baada ya uhuru kupitia watu kama kina Bibi Titi Mohamed.

Harakati za mapambano ya haki ziliendelea tukiwashuhudia watu wenye majina makubwa na maarufu Waislamu kama wakina Maalim Seif, Aboud Jumbe, Zitto Kabwe, Professor Safari, Said Arfi, Prof Lipumba, Uamsho, CAG Assad, Salum Mwalimu mpaka Fatma Karume.

Hata hivyo ni wazi mchango wao umekuwa ukienda ukipungua, kuwa vuguvugu na wakizidi kujitambulisha na kujiweka karibu na serikali zaidi mpaka leo wamekuwa watetezi wakubwa wa serikali au wasiotaka kuikosoa tena.

Sasa hivi majina makubwa walio active wamebaki wachache sana kama Sheikh Ponda tu.
 
Kuanzia uhuru mpaka leo hii mchango wa Waislamu katika harakati za mapambano umeenda ukipungua sana.

Wakati wa uhuru Waislamu walikuwa active sana mstari wa mbele katika harakati za uhuru pamoja na Nyerere. Watu wengine kama Mohamed Said wanafikia mbali hata kusema wao ndio walikuwa engine ya mapambano na kina Nyerere walikuwa body tu.

Waislamu wakiendeleza kutoa mchango mkubwa wa changamoto dhidi ya utawala hata baada ya uhuru kupitia watu kama kina Bibi Titi Mohamed.

Harakati za mapambano ya haki ziliendelea tukiwashuhudia watu wenye majinia makubwa Waislamu wakina Maalim Seif, Aboud Jumbe, Zitto Kabwe, Professor Safari, Arfi, Prof Lipumba, Uamsho, CAG Assad mpaka Fatma Karume.

Hata hivyo ni wazi mchango wao umekuwa ukienda ukipungua, kuwa vuguvugu na wakizidi kujitambulisha na kujiweka karibu na serikali zaidi mpaka leo wamekuwa watetezi wakubwa wa serikali au wasiotaka kuikosoa tena.

Sasa hivi majina makubwa walio active wamebaki wachache sana kama Sheikh Ponda tu.
Kwa sababu waislamu wanafaidi keki ya taifa kwa hichi kipindi
 
Kuna hii saikolojia ya hovyo kidogo bongo kwamba, awamu ambayo Rais aliyopo madarakani ni Muislamu, hamasa ya Waislamu kupambana na serikali inashuka sana automatically.

Huwa kuna kale kamtazamo ka chini kwa chini kwamba serikali ni yetu, hata kama kiuhalisia matatizo ya kiuchumi na kijamii yanamgusa kila mtu bila kujali dini. Hii complacency ndio inafanya sauti za kukosoa zionekane kama usaliti ndani ya jamii. Ni ujinga sana!
 
Blindfold of unseeing soul.
The bitter vigil of famine stricken hearth.
A brittle concord,shattered at the first tremor.
Kinship curdled into clannish venom.
 
Kwa sababu waislamu wanafaidi keki ya taifa kwa hichi kipindi
Siyo kweli.

Waislamu wenye akili wengi tu wapo na wanaunga harakati za mapambano,ingawa wajinga wajinga wanaotazama ukosoaji kwa uongozi huu ni kwa sababu ya dini yake yule bi mkubwa na siyo uwezo wake kama kiongozi...Hao hawakosekani.

Ila kusema waislamu wanapitia kipindi cha raha au kwamba wa-kristo walikuwa wanapitia kipindi Bora katika maisha enzi za magufuli kulinganisha na waislamu...huo ni uongo.

Ni mtu duni tu anayeweza kuwaza namna hiyo.

Sisiem hawana huo muda wa kuangalia dini. Wao wanakula kwa sababu ni sisiem,dini zenu hazina nafasi inapokuja swala la ulaji kwa Hawa jamaa.

Ninachoweza kukubaliana na wewe ni kuwa...Sasa hivi kiongozi aliye juu ameweka watu wengi sana wa kwao na hiyo siyo kwa sababu anawapenda sana ila sababu ni ya security yake. Anahisi akiweka watu wa kule ng'ambo usaliti unaweza kuwa mdogo sana kulibganisha na nyie vichogo.

Ila msoto wa wabara hauna dini tunapitia sote Katika Njia ya miiba.
 
Kuanzia uhuru mpaka leo hii mchango wa Waislamu katika harakati za mapambano umeenda ukipungua sana.

Wakati wa uhuru Waislamu walikuwa active sana mstari wa mbele katika harakati za uhuru pamoja na Nyerere. Watu wengine kama Mohamed Said wanafikia mbali hata kusema Waislamu ndio walikuwa engine ya mapambano na kina Nyerere walikuwa body tu.

Waislamu waliendelea kutoa mchango mkubwa wa changamoto dhidi ya utawala hata na mapambano ya kuboresha haki hata baada ya uhuru kupitia watu kama kina Bibi Titi Mohamed.

Harakati za mapambano ya haki ziliendelea tukiwashuhudia watu wenye majina makubwa na maarufu Waislamu kama wakina Maalim Seif, Aboud Jumbe, Zitto Kabwe, Professor Safari, Said Arfi, Prof Lipumba, Uamsho, CAG Assad mpaka Fatma Karume.

Hata hivyo ni wazi mchango wao umekuwa ukienda ukipungua, kuwa vuguvugu na wakizidi kujitambulisha na kujiweka karibu na serikali zaidi mpaka leo wamekuwa watetezi wakubwa wa serikali au wasiotaka kuikosoa tena.

Sasa hivi majina makubwa walio active wamebaki wachache sana kama Sheikh Ponda tu.
Waislam kama walivyo wafrika wengine wote ni wabinafsi Sana.
Nakumbuka kipindi Rais Magufuli alipoingia madarakani, Wasukuma woote ninaojua Mimi na Marafiki zangu walikuwa kama Malaika, hawakubali ukandamizaji anaifanya kwa raia, hawakubali Sera mbaya za uchumi wala ufisadi wake.
Mpaka wale wenye akili nilio amini wasomi yoote waliweka chini ya kapuni
 
Unawakumbuka Zitto Kabwe na Fatma Karume wa kipindi cha Magufuli?

Unaukumbuka moto wao kwenye kukosoa kila mpango wa Magufuli ikiwamo ununuzi wa ndege, bwawa la Nyerere na SGR!

Nakukumbusha tu, Hao jamaa bado wapo...
Nawakumbuka vizuri sana mkuu, ndio maana nashanga leo wamepotelea wapi!
 
Waislam kama walivyo wafrika wengine wote ni wabinafsi Sana.
Nakumbuka kipindi Rais Magufuli alipoingia madarakani, Wasukuma woote ninaojua Mimi na Marafiki zangu walikuwa kama Malaika, hawakubali ukandamizaji anaifanya kwa raia, hawakubali Sera mbaya za uchumi wala ufisadi wake.
Mpaka wale wenye akili nilio amini wasomi yoote waliweka chini ya kapuni
Hili ni tatizo kubwa sana kwa Waafrika. Sehemu nyingine duniani watu wanaunganishwa na class zaidi badala ya makabila na dini. Class struggle inapaswa kuwa muhimu zaidi kuliko makabila na dini zetu.
 
Nawakumbuka vizuri sana mkuu, ndio maana nashanga leo wamepotelea wapi!
Mkuu japo tunaogopa kuongelea udini kwenye siasa zetu ila huo udini upo na ni mkubwa...

Kama unakumbuka kipindi CUF ina mgogoro na Maalim Seif akahama, kila mtu alitarajia ataenda Chadema...

Maana kwa wakati huo ndio chama kilikua kimejipambanua kupambana na uovu...

Na Maalim akijulikana kama mpigania haki...

Unajua kwanini alienda ACT?

Fatma Karume pia baada ya kutoka CCM...

Mkuu nakuhakikishia wakati nyinyi wengine mnapambania haki bila kutazama tofauti za kidini au kijamii kuna wengine wana jicho tofauti.
 
Udini upo kiasi Tanzania hii ila watu wanaogopa tu kuongelea, Watanzania ni watu tusiopenda kukubali matatizo yetu kirahisi na kuyazungumza au kuyajadili kwa uwazi mkubwa.
 
Back
Top Bottom