Issue za watu kupotezwa I don't think kama kuna mtanzania mwenye akili timamu ana support Hilo, na views nyingi za watu wa pwani hakuna mtu wa pwani mwenye roho hio ya kuteka watu,
Issue ya demokrasia na vyama, watu wanataka tu kiongozi anaejali, mfano kwetu hapa Tanga mbunge alikua ni mpinzani, Musa Bakari wa Cuf, then Akaja Ummy mwalimu, succession ilikua nzuri tu, Japo Tanga upinzani mkubwa ila Ummy ni one of our own, mapungufu yake ni mapungufu yetu, uchaguzi uliopita wakati kuna vurugu za Oct 29 watu wa Tanga hawakuandamana, ila kulikua na kifujo chetu wenyewe kwamba mbunge mpya watu hawamtaki ambaye alim replace Ummy CCM,
Mambo ya ukosoaji It depends, watu wa pwani ni conservative, heshima na adabu ni vitu vinavyopewa priority, hasa kwa watu waZima, Mzee anaweza kuwa anakosea ila akapewa heshima yake na hata kama anakosolewa basi kwa staha, siasa kama za Kina Mdude huwezi Kuta ni maarufu kwenye community zetu, ila watu kama Lissu, Zitto, OMO, Magufuli etc ni popular most of time sababu ukosoaji wao ni data driven most of time na sio personal.
Kuhusu Ufisadi na Uchumi kwa ujumla watu wanataka kuona matokeo, binafsi yangu I don't care viongozi wanalipana kiasi gani, wamekula kiasi gani, ila naangalia wamezalisha kiasi gani, na Mimi nimefaidika vipi. Kiongozi aliozalisha trilioni 10 na kujilipa bilioni 500 ni Bora kuliko anaezalisha trilioni 2 na kujilipa bilioni 100. Na mifumo kama hii utaiona kampuni zote kubwa, ingekua ni uwezo wangu Mimi nigewalipa hata mara 100 ya sasa as long as Uchumi ukue kwa kasi, so huku huoni watu wakilalamika sana sababu ya Viwanda, bandari, Bomba la mafuta etc. sasa hivi Tanga rent zipo juu, watu wanapata rent sawa na Dar, Hoteli hapa mjini zimejaa all the time that's why huoni upinzani mkubwa.