Kuanzia uhuru mpaka leo hii mchango wa Waislamu katika harakati za mapambano umeenda ukipungua sana.
Wakati wa uhuru Waislamu walikuwa active sana mstari wa mbele katika harakati za uhuru pamoja na Nyerere. Watu wengine kama
Mohamed Said wanafikia mbali hata kusema Waislamu ndio walikuwa engine ya mapambano na kina Nyerere walikuwa body tu.
Waislamu waliendelea kutoa mchango mkubwa wa changamoto dhidi ya utawala hata na mapambano ya kuboresha haki hata baada ya uhuru kupitia watu kama kina Bibi Titi Mohamed.
Harakati za mapambano ya haki ziliendelea tukiwashuhudia watu wenye majina makubwa na maarufu Waislamu kama wakina Maalim Seif, Aboud Jumbe, Zitto Kabwe, Professor Safari, Said Arfi, Prof Lipumba, Uamsho, CAG Assad, Salum Mwalimu mpaka Fatma Karume.
Hata hivyo ni wazi mchango wao umekuwa ukienda ukipungua, kuwa vuguvugu na wakizidi kujitambulisha na kujiweka karibu na serikali zaidi mpaka leo wamekuwa watetezi wakubwa wa serikali au wasiotaka kuikosoa tena.
Sasa hivi majina makubwa walio active wamebaki wachache sana kama Sheikh Ponda tu.