Nini kinaendelea kuhusu Novena ya Mtakatifu Ritha wa Kashia? Mbona imebamba sana?

Nini kinaendelea kuhusu Novena ya Mtakatifu Ritha wa Kashia? Mbona imebamba sana?

Nikikumbuka enzi hizo nilivyokuwa mkatoliki konki kijana wa madhabauni Hadi nikanunua kitabu cha mawaridi ya sala ili kilasiku niwe nasali hizo novena natamani kujitandika makofi, akili ilipofunguka niligundua dini ni ubatili na utapeli mtupu sawa na Imani za kishirikina, wanaosali hizo novena hawana tofauti na wale mapoyoyo wavaa kobasi wanao amini kwenye majini.
NB: Hao jamaa wanaonaje wakiunganisha nguvu kwenye hizo novena wawaombe Hao watakatifu washushe gari za mwendo Kasi za kutisha? Taifa litawaweka kwenye vitabu sahihi vya historia, vinginevyo hawatakuwa na utofauti na wale wafuasi wa kinjekitile walio amini watapambana na mkoloni kwa kutamka Tu maji maji
Hicho kitabu kina hizo novena?? Jina lake linaitwaje?
 
Sio sahihi kusema hivyo, hospitali zinajengwa na Wakatoliki ambao wengine ni wakwepa kodi, mafisadi na hata wauza dawa za kulevya, mfano Colombia Pablo Escobar alivyojenga.
Acha hizo tunazungumzia hospitali ambazo ndugu zako na wewe mnatibiwa hapo hapa Tanzania ,

1.Bugando Medical centre-Mwanza
2.St.Francis referral hospital -Morogoro
3.Peramiho regional hospital -Songea

4.Ndada referral hospital -Mtwara
 
Sijawahi kutibiwa katika hizi Hospitali wala simjui ndugu yangu aliyewahi kutibiwa huko.
 
Mimi nina ushuhuda wangu ni wa mwaka huu!Kuna mtu mmoja katika kampuni fulani alifanya fitna nikashindwa kuendelea kampuni X.ilikuwa ni kipindi kigumu sana kwangu na nikipindi ambacho niseme nilihitaji sana kazi.Nilianza kusali NOVENA YA Mt Ritta ,mtakatifu Joseph,Mt Padre Pio.Nilikuwa nasali novena na sala za maombi ya kawaida mama yangu pia alikuwa aniombea katika hili.Baada ya kusali sana ikapita kama miezi miwili hivi mama akaniambia ameota nipo kwenye interview na hr wako anaoekana yupo----- hapa alinitajia wadhfa wa hr huyu.Jamani kuna siku nikapigiwa simu niende interview maana niliapply sehem tofauti tofauti.Kufika kwenye interview yale mama aliyoniambia niliyakuta vilevile nilishangaa sana.Nilifanya ile interview na ile kazi nikaipata.Hata baada ya kummuliza hr niliwezaje kupita ilikuwa ni muujiza sababu application zilikuwa karibia 800.Ndugu zangu Mungu yupo na anasikia maombi yetu,nilifunga na kusali kwa miezi mitatu Watakatifu wa Mwenyezi Mungu waliweza kunisaidia kuniombe na kuwasilisha sala yangu!
 
Asante mkuu! Ya kwangu iko tofauti kidogo na ya kwako! Mimi nilifanya interview kwenye kampuni moja, nikafanya ya kwanza nikifanyishwa na team leader wa hicho kitengo nikatoboa vizuri sana! Akanipeleka kwa mtu mwingine nako nikatoboza sasa huyu wa mwisho ndiye akatoa comments zake kwamba huyu bwana yuko vizuri sana atatusaidia mno tumpe kazi. Kumbe team leader yeye akawa na wasiwasi kwamba naweza kuchukua nafasi yake baadaye maana kwenye interview mwenyewe alipwaya sana! Akanifanyia fitina na kufuta ile interview, kumbe huku nyuma nilishapewa taarifa kwamba bwana umefanya vizuri mno kwenye hiyo interview wakati wowote utaitwa! Subiri nitaitwa subiri na wewe mpaka kesho! Basi bwana nikamfungia Novena ya kumhoji Mungu kulikoni hiyo nafasi nimeikosa? Kabla hata sijamaliza siku ya 9, yule team leader akatumbuliwa! Kwenye Novena hiyo nilimhoji Mungu mambo mawili (1) Je, hiyo nafasi nimeikosa kihalali? (2) Kama kuna fitina ya mtu unanipa ishara gani? Tumwache Mungu aitwe Mungu! Kwa wanaobeza wao waendelee tu!
 
Asante mkuu! Ya kwangu iko tofauti kidogo na ya kwako! Mimi nilifanya interview kwenye kampuni moja, nikafanya ya kwanza nikifanyishwa na team leader wa hicho kitengo nikatoboa vizuri sana! Akanipeleka kwa mtu mwingine nako nikatoboza sasa huyu wa mwisho ndiye akatoa comments zake kwamba huyu bwana yuko vizuri sana atatusaidia mno tumpe kazi. Kumbe team leader yeye akawa na wasiwasi kwamba naweza kuchukua nafasi yake baadaye maana kwenye interview mwenyewe alipwaya sana! Akanifanyia fitina na kufuta ile interview, kumbe huku nyuma nilishapewa taarifa kwamba bwana umefanya vizuri mno kwenye hiyo interview wakati wowote utaitwa! Subiri nitaitwa subiri na wewe mpaka kesho! Basi bwana nikamfungia Novena ya kumhoji Mungu kulikoni hiyo nafasi nimeikosa? Kabla hata sijamaliza siku ya 9, yule team leader akatumbuliwa! Kwenyw Novena hiyo nilimhoji Mungu mambo mawili (1) Je, hiyo nafasi nimaikosa kihalali? (2) Kama kuna fitina ya mtu unanipa ishara gani? Tumwache Mungu aitwe Mungu! Kwa wanaobeza wao waendelee tu!
Ubalikiwe sana mtumish

BWANA anawapenda watu kama wewe tena anawatafuta sana Yohana 4: 23-24
 
Back
Top Bottom