Jeshi letu la Polisi na vyombo vingine vya Usalama vimeonesha udhaifu mkubwa mno katika azma yao ya kuzuia Maandamano ya Amani kupinga mkataba wa Bandari, kudai Katiba Mpya na Uhuru wa kuishi kwenye maeneo ya asili.
Polisi wamekodoa macho Mbeya huku Dunia nzima watu wameandamana kwa kuvaa nguo maalumu nyeupe zenye ujumbe mahususi!
Ninanaona watu wa kila kada, siasa, dini, wasanii, wasomi wakiandamana USA, Russia, SA, Kenya, Tanzania, UK, Singapore, Ufilipino, Kenya, Israeli, Rwanda, Uganda, Bennin, Ugoslavia, Moldovia, Italia, Zambia, Msumbiji, Namibia, Comoro, Morocco, Dubai, Quatar, Brazili na Sweden. Naendelea kufuatilia. Ujumbe huu utakuwa umeenda mbali sana maana vyombo vya habari vya Kimataifa vinafuatilia kwa karibu sana tukio hili kama DW, VoA, BBC, Al-Jazeera na ABC.
Walioandaa haya Maandamano pokeeni maua yenu. Hii ni akili kubwa mno.