Nini kinafanya Wazazi walio wengi kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine?

Nini kinafanya Wazazi walio wengi kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine?

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
2,919
Reaction score
5,558
Sijui kama na wewe umeona, nimekuwa nikichunguza familia nyingi unakuta wazazi hasa wamama kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine.

Nachakushangaza zaidi sio kwamba ni kwa sababu ana mafanikio kiuchumi au tabia njema hapana ila unakuta huyo ndio anapendwa zaidi kuliko hata wale wenye tabia njema na uchumi mzuri.

Nisimalize yote nadhani na nyie mna mengi na mifano mingi zaidi ya kueleza.
 
Tabia yake kulingana na mtazamo wa mzazi wake.
 
Sijui kama na wewe umeona, nimekuwa nikichunguza familia nyingi unakuta wazazi hasa wamama kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine.

Nachakushangaza zaidi sio kwamba ni kwa sababu ana mafanikio kiuchumi au tabia njema hapana ila unakuta huyo ndio anapendwa zaidi kuliko hata wale wenye tabia njema na uchumi mzuri.

Nisimalize yote nadhani na nyie mna mengi na mifano mingi zaidi ya kueleza.
Mara nyingi si rahisi kusema ni kwa sababu ya pesa, tabia au mafanikio. Wazazi ni binadamu pia, wanaweza kujenga ukaribu wa kihisia na mtoto fulani kutokana na historia ya maisha, mazingira aliyokulia, jinsi alivyokuwa karibu nao au hata namna anavyowahitaji.

Wakati mwingine mtoto anayesumbua au anayepitia changamoto ndiye anayekuwa karibu zaidi na mzazi kwa sababu mzazi anajisikia anapaswa kumlinda zaidi. Kuna pia suala la personality—mtoto mmoja anaweza kufanana sana na mama/baba katika tabia na hivyo bond kuwa kubwa bila wao hata kutambua.

Tatizo linakuja pale tofauti hiyo inapokuwa kubwa kiasi cha watoto wengine kujiona hawapendwi. Hapo inaweza kuacha majeraha ya muda mrefu ndani ya familia.

Kwa hiyo nadhani si kila tofauti ya ukaribu ni upendeleo, lakini upendeleo wa wazi kabisa unaweza kutengeneza ufa mkubwa sana kati ya ndugu.
 
Sio kwamba wanapendwa sana
Mzazi siku zote hupenda mtoto anaeleta maokoto nyumbani
Ila hao mnaosema watukutu, walevi, wezi tunaona wanapendwa na wazazi kwa sababu tunataka wachukiwe
Ila kiuhalisia watoto kama hao jamii imekua ikiwatenga hivyo mzazi ndio pekee anayeweza kumsikiliza na hata ingekua wewe ndio mzazi usingeacha kumsikiliza sababu jamii yote na ndugu huwa inawatenga watu kama hao
 
Kuna hao lakini kuna wengine unakuta hawana hivyo labda ni kijana mlevi, mwizi anapendwa kuliko wengine hujaona hiyo.
Upo sahihi mkuu Kipindi cha ujana nimeishi Temeke Aziz Ally kuna hiyo familia Baba alikuwa mtu wa mfumo Mama ni mtu wa nyumbani wana watoto almost 6 ila kuna huyo mmoja wanamwita Abas Chotta alikuwa jambazi aliyekubuhu mpeleke kituo chochote siku 2 ni nyingi utamkuta kitaani kesharudi alikuwa ni kipenzi cha wazazi sema ndio hivyo Nakumbuka kuna wakati alikiri makosa akawa ustadhi safi akanunuliwa bajaji imuingizie kitu Huwezi amini aliuza ile bajaji kwa bei ya kutupa akarudi upya kwenye wizi kilichomkuta amekua kilema walimsukumia barabarani akagongwa na gari. Wazazi wakaja kufa Anagombea Urithi tu na ndugu zake
 
Back
Top Bottom