Mvinyo mpya
JF-Expert Member
- Aug 24, 2013
- 3,816
- 9,308
Mlevi na mwizi anapendwa katika harakati za kutaka kumsaidiaKuna hao lakini kuna wengine unakuta hawana hivyo labda ni kijana mlevi, mwizi anapendwa kuliko wengine hujaona hiyo.
Mlevi na mwizi anapendwa katika harakati za kutaka kumsaidiaKuna hao lakini kuna wengine unakuta hawana hivyo labda ni kijana mlevi, mwizi anapendwa kuliko wengine hujaona hiyo.
Huyo mtoto Abbas Chota huenda ni michezo😂 kabla sijakua nilikuwa sielewi ila kwa sasa huniambii kitu. Hii dunia iacheni kama ilivyo. Watu ni waharibufu sanaUpo sahihi mkuu Kipindi cha ujana nimeishi Temeke Aziz Ally kuna hiyo familia Baba alikuwa mtu wa mfumo Mama ni mtu wa nyumbani wana watoto almost 6 ila kuna huyo mmoja wanamwita Abas Chotta alikuwa jambazi aliyekubuhu mpeleke kituo chochote siku 2 ni nyingi utamkuta kitaani kesharudi alikuwa ni kipenzi cha wazazi sema ndio hivyo Nakumbuka kuna wakati alikiri makosa akawa ustadhi safi akanunuliwa bajaji imuingizie kitu Huwezi amini aliuza ile bajaji kwa bei ya kutupa akarudi upya kwenye wizi kilichomkuta amekua kilema walimsukumia barabarani akagongwa na gari. Wazazi wakaja kufa Anagombea Urithi tu na ndugu zake
Hauwezi kuwa mlevi,mraibu wa drugs,kichaa,mwizi, halafu wazazi wakupende never
labda ni kimbola yao huwezi jua mana dunia huwa ina mengi sana na mengi yapo sirini kuyajua au tambua yaitaji kibali cha Mungu tu.
Na mara nyingi matoto matukutu ndio yanapendwa na mama zao.
Tabia mbaya kubagua watoto, iwe kwa mafanikio yao au vinginevyo.
Tabia yake kulingana na mtazamo wa mzazi wake.
Mara nyingi si rahisi kusema ni kwa sababu ya pesa, tabia au mafanikio. Wazazi ni binadamu pia, wanaweza kujenga ukaribu wa kihisia na mtoto fulani kutokana na historia ya maisha, mazingira aliyokulia, jinsi alivyokuwa karibu nao au hata namna anavyowahitaji.
Wakati mwingine mtoto anayesumbua au anayepitia changamoto ndiye anayekuwa karibu zaidi na mzazi kwa sababu mzazi anajisikia anapaswa kumlinda zaidi. Kuna pia suala la personality—mtoto mmoja anaweza kufanana sana na mama/baba katika tabia na hivyo bond kuwa kubwa bila wao hata kutambua.
Tatizo linakuja pale tofauti hiyo inapokuwa kubwa kiasi cha watoto wengine kujiona hawapendwi. Hapo inaweza kuacha majeraha ya muda mrefu ndani ya familia.
Kwa hiyo nadhani si kila tofauti ya ukaribu ni upendeleo, lakini upendeleo wa wazi kabisa unaweza kutengeneza ufa mkubwa sana kati ya ndugu.
Sio kwamba wanapendwa sana
Mzazi siku zote hupenda mtoto anaeleta maokoto nyumbani
Ila hao mnaosema watukutu, walevi, wezi tunaona wanapendwa na wazazi kwa sababu tunataka wachukiwe
Ila kiuhalisia watoto kama hao jamii imekua ikiwatenga hivyo mzazi ndio pekee anayeweza kumsikiliza na hata ingekua wewe ndio mzazi usingeacha kumsikiliza sababu jamii yote na ndugu huwa inawatenga watu kama hao
Ni kweli ukimpenda sana na kumpa kila anachotaka mtoto una muharibu.Mimi hua naona watoto wanaopendwa na wazazi huishia kuwa walevi, watukutu n.k. Maana nafikiri hua wanadekezwa na kupewa kila wanachotaka
Mimi ni mlevi na mama yangu ananipenda kuliko watoto wake wengine 7 hata wao wanajua
Najivunia mama yngu 🤣 sijui siku akifa na mimi nipo hai itakuaje😭Aise hongera sana meku. Mamas boy 🤣.
Upo sahihi mkuu Kipindi cha ujana nimeishi Temeke Aziz Ally kuna hiyo familia Baba alikuwa mtu wa mfumo Mama ni mtu wa nyumbani wana watoto almost 6 ila kuna huyo mmoja wanamwita Abas Chotta alikuwa jambazi aliyekubuhu mpeleke kituo chochote siku 2 ni nyingi utamkuta kitaani kesharudi alikuwa ni kipenzi cha wazazi sema ndio hivyo Nakumbuka kuna wakati alikiri makosa akawa ustadhi safi akanunuliwa bajaji imuingizie kitu Huwezi amini aliuza ile bajaji kwa bei ya kutupa akarudi upya kwenye wizi kilichomkuta amekua kilema walimsukumia barabarani akagongwa na gari. Wazazi wakaja kufa Anagombea Urithi tu na ndugu zake
Sio kweli toka mdogo tu
MakubwaaMimi binafsi kati ya watoto wangu watatu katika mama tofauti. Mtoto mmoja ninampenda sanaa kuliko wengine sababu alizaliwa na mwanamke ambaye nilimpenda sana basi automatically nikajikuta kumpenda sana mtoto. Wale wengine ndio hivyo tu kwasababu wananiita baba.
Dah hatari sana, akakuongezea zaidi sioWakati mwingine Mungu anakupa kibali tu, Mimi nilipata kibali kwa wazazi wote wawili, lakini sikuyachukulia poa mapenzi ya wazazi wangu.
Mwanzoni nilimuona Baba ananipenda na kuniamini japo sikujua sababu, Siku moja kulikuwa na kikao nyumbani na Mimi sikuwepo na hawakutilia maanani kuwa sipo, katikati ya kikao wakagundua kuwa sikuwepo, nikatafutwa kwa marafiki zangu jirani, nikapatikana kikao kikaendelea, Mchango nilioutoa kwenye hicho kikao kilimfanya mzee aende kubadili makaratasi yake ya urithi.