Nini kinafanya Wazazi walio wengi kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine?

Nini kinafanya Wazazi walio wengi kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine?

Kinachopelekea upendo wa mzazi kuelekezwa kwa mtoto mmoja, ni utii.

Wazazi huwa wanapenda watoto wenye utii, ambao ukiwapa maelekezo wao watazingatia

Mimi nilipata bahati hiyo, lakini nilichojifunza ndugu wengine wanatengeza jealous wakiona unapendwa

Usipokuwa makini, unaweza kukutwa na jambo la Yusuph kwenye Biblia

Kama Mzazi, nimekataa kuwapenda watoto kwa upendeleo, nawapenda wote

Na yule ambaye naona ana changamoto ya utii/heshima, namnyoosha mapema kabisa ili wote uwapende kwa viwango vinavyofanana
Hongera mkuu ila kuna yule mmoja unampenda zaidi kidogo japo haipo wazi kwa sababu unatambua na hasa kwa experience yako ya nyuma.
 
Sijui kama na wewe umeona, nimekuwa nikichunguza familia nyingi unakuta wazazi hasa wamama kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine.

Nachakushangaza zaidi sio kwamba ni kwa sababu ana mafanikio kiuchumi au tabia njema hapana ila unakuta huyo ndio anapendwa zaidi kuliko hata wale wenye tabia njema na uchumi mzuri.

Nisimalize yote nadhani na nyie mna mengi na mifano mingi zaidi ya kueleza.
MAma yangu anawapenda watoto wa 3 mimi nilipendwa na baba yangu sana alipokufa nililia sana niliona ndio mwisho wangu sasa hivi nipo na yuda ambaye ni bi mkubwa na mayuda wenzake
 
Wakati mwingine Mungu anakupa kibali tu, Mimi nilipata kibali kwa wazazi wote wawili, lakini sikuyachukulia poa mapenzi ya wazazi wangu.
Mwanzoni nilimuona Baba ananipenda na kuniamini japo sikujua sababu, Siku moja kulikuwa na kikao nyumbani na Mimi sikuwepo na hawakutilia maanani kuwa sipo, katikati ya kikao wakagundua kuwa sikuwepo, nikatafutwa kwa marafiki zangu jirani, nikapatikana kikao kikaendelea, Mchango nilioutoa kwenye hicho kikao kilimfanya mzee aende kubadili makaratasi yake ya urithi.
Fafanua kwanini alibadilisha
 
Yeah hii naona inakuja automatically.
Mama yangu anatupenda wote ila.. baba alikua na love sana na watoto wa kike

Mama yangu ana love sana na watoto wa kiume

Mimi pia na watoto wa kiume wawili mmoja anamaliza standard seven mwakani

Nina bint yangu kafanana na mama angu nakapenda sana 2years age

Pia na kijana wa 1 years age huyu mzee wangu kabla hajafa alimpa jina la kimila kama mbarikiwa/ mteule / mrithi wa ukoo
 
Mimi ni mhanga wa jambo hilo na mpaka leo limeniathiri kisaikolojia.
Nimezaliwa last born lakini tangu utotoni mama alikua anampenda sana kaka yangu tunayefuatana nae kiasi kwamba nilikua najisikia vibaya but BABA was on my side!! (APUMZIKE KWA AMANI). Kilichotokea tangu kaka akiwa darasa la tano alianza kudokoa vitu vya nyumbani na kucheza pull table. Kipindi hiko pia kulikua na matumizi ya juu sana ya Kuberi. In short alianza na kuiba kabisa vitu vya nyumbani,majirani na mtaani. Baba akimkanya na kumpeleka polisi mama anamzunguka baba na kwenda kumtoa. Now my brother is 37Years bado anaishi nyumbani na kawa mzigo kwa mama na familia kiujumla. Alipelekwa shule ya Seminari but alifukuzwa akiwa Form Two kwa utovu wa nidhamu, by the time i was among the best students na nilisoma kwa hasira mpaka kumaliza elimu ya juu baadae mama ndo akaanza kujisogeza kwangu😂 huwa nikimkumbusha alovyokua hanijali anaumia maana nae sasa ni Mzee wa miaka 75.

So huwa naangalia tu matokeo ya upendo wa kuspoil watoto na kudekeza watoto na mimi nimejifunza jinsi ya kulea wanangu wawili Mungu alonijaalia.
Pole sana kaka, mama alipitiliza sana kwenye huo upendo kwa kaka yako. Na ipo hivyo kwa familia nyingi tuu.

Mithali ninasema mtoto mpumbavu ni mzigo kwa mama. Msamehe tu ubure mama yako. Na hongera kama unalea watoto wako kwa usawa.
 
Sijui kama na wewe umeona, nimekuwa nikichunguza familia nyingi unakuta wazazi hasa wamama kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine.

Nachakushangaza zaidi sio kwamba ni kwa sababu ana mafanikio kiuchumi au tabia njema hapana ila unakuta huyo ndio anapendwa zaidi kuliko hata wale wenye tabia njema na uchumi mzuri.

Nisimalize yote nadhani na nyie mna mengi na mifano mingi zaidi ya kueleza.
Kwa uzoefu wangu, nimeona mara nyingi watoto wanaokuwa wamepitia matatizo wakati wa kukua kwao mfano magonjwa sugu, uzazi wa shida sana, kunusulika mimba kuharibika, au kazaliwa kipindi cha ufakara kwenye familia na kukosa mahitaji muhimu kulinganisha na wenzake hao mara nyingi huwa wannapendwa zaidi....wazazi huwa wanaona ni kama kuishi kwao ni bahati.
 
Ni kweli japo binafsi nimejitahidi kuwapenda wote

Labda huko mbele ya safari nikisikia wameanza kupanga mipango ya kunitanguliza ahera ili wapate kugawana Urithi
Wazazi hupenda watoto watiifu Mimi ni MTIIFU mnyenyekevu sana kwa wazazi na sikuwai kuwa na scandals mbaya

Juzi kati mama akiambiwa na wife kua now nakunywa pombe pia na mchepuko mama ALIPO piga simu alinifokea sana nahakika Navyo mjua anaweza kukupiga mpaka akakun'gata/ kuuma na meno

Napenda kua mtu mzurii siku zoteee na pia lazima watoto wetu tuwakunje angali wabichi
 
Wazazi hupenda watoto watiifu Mimi ni MTIIFU mnyenyekevu sana kwa wazazi na sikuwai kuwa na scandals mbaya

Juzi kati mama akiambiwa na wife kua now nakunywa pombe pia na mchepuko mama ALIPO piga simu alinifokea sana nahakika Navyo mjua anaweza kukupiga mpaka akakun'gata/ kuuma na meno

Napenda kua mtu mzurii siku zoteee na pia lazima watoto wetu tuwakunje angali wabichi
Sahihi kabisa

Wazazi hupenda watoto watiifu

Ukiwa na mambo mengi, sio rahisi kupendwa kihivyo
 
Kuna Mzee mmoja aliwahi kuniambia kwamba, kama unavyoona koo zilizopo katika namna yakuonekana ila pia upande wa pili wa shilingi huwa kuna Koo pia, kwahiyo kuna watu wanatoka kundi moja la mfumo nyota na licha ya kwamba wanatoka kwenye kundi moja ila huwa kunakuaga na utofauti wa ukuu kulingana na eneo frequency za mtu na mtu zilipo.

Kuna watu wao huwa siku zote frequency zao zipo juu na zinakua stable sana (Hawa huwa hawaogopagi chochote hasa kitu kinachoitwa ushirikina ndio hawaamini kabisaaaaa, mtaani kwenu anaweza akawepo mzee anaogopeka ila akijichanganya kwa mtu wa aina hii atakula hata makofi na Hana cha kumfanya)

Hawa ni watu ambao huwa wanakubalika sana kwenye familia na pia wengine hadi kuogopeka wanaogopeka kulingana na wao wanavyoishi ile physically (akiwa ni mtu mtukutu basi mtaa mzima au ukoo mzima wanamuogopa na akiwa mtu wa heshima basi watu wengi wanamuheshimu na akiwa mtu wa kawaida basi ni rahisi sana kupendwa na watu wengine hasa wale ambao anatetema juu yao)

Na kwenye familia nyingi huwa wapo watu wa hivyo.

Na matapeli wengi huwa wanatokea kwa watu wa aina hii😅

Ila pia najua hata wewe umewahi kushuhudia unakutana na mdada mrembo ako na kila kitu kwenye maisha ila amezama kwenye penzi na kijana muhuni fulani tu hivi, Hana moja wala mbili ila once akitokea kwa bi mdada anakua anamnyenyekea hadi mnashangaa😅

Anyway, ni ngumu kuelewa kwasababu ni mambo ya nature so kama vile wale wenye upendo wanavyoshindwa kuwa na maelezo ya kutosha kwanini wanawapenda watu hao basi hata prove kwenye mambo haya pia inakua ngumu.
Hakika hii inatokea in nature na huo mfano wa mdada kazama kwa bad boy nineona sana
 
Mimi binafsi kati ya watoto wangu watatu katika mama tofauti. Mtoto mmoja ninampenda sanaa kuliko wengine sababu alizaliwa na mwanamke ambaye nilimpenda sana basi automatically nikajikuta kumpenda sana mtoto. Wale wengine ndio hivyo tu kwasababu wananiita baba.
Sawa sawa mkuu. Upendo umetokea automatically.
 
Mama yangu anatupenda wote ila.. baba alikua na love sana na watoto wa kike

Mama yangu ana love sana na watoto wa kiume

Mimi pia na watoto wa kiume wawili mmoja anamaliza standard seven mwakani

Nina bint yangu kafanana na mama angu nakapenda sana 2years age

Pia na kijana wa 1 years age huyu mzee wangu kabla hajafa alimpa jina la kimila kama mbarikiwa/ mteule / mrithi wa ukoo
Yeah mimi kati ya watoto wote nane ndio nafanana na b mkubwa kuliko wote wengine ni mzee , nahisi ndio sababu
 
Inategemea sana kwa upande wa mzazi. Labda walikuwa karibu sana utotoni, labda mtoto alipatikana kwa shida, labda mtoto anatumika kama msaada wa kihisia baada ya mzazi kupitia jambo fulani...

Kuna sababu mtambuka pia kama za kiimani/kidini. Mfano kuna matukio yanaweza kupelekea mzazi aamini mwanae analogwa/ana vita ya kiroho, hivyo atamzingatia zaidi.

Hakuna sababu moja, ni saikolojia ya wazazi.
Inakuwa ni mchanganyiko wa sababu inatofautiana kwenye familia moja na nyingine.
 
Dah mfano ulio hai na unaishi. Ila jamaa amekuwa na mwisho mbaya. Na mara nyingi wazazi wao wakifariki huwa wanaumia sana watu wa namna hiyo.
Alikuwa kipenzi cha mama! Ukitaka umlize mkumbushe enzi zake. Kitaani walimbatiza jina Sajenti Chotta akisikia hivyo atacheka mpaka jino la 32
 
Back
Top Bottom