Nini kitatokea endapo Dunia itaacha kujizungusha ktk mhimili wake na pia endapo itaacha kulizunguka jua?

Masahihisho:
Majira ya mwaka yanapatikana kwa dunia kuzunguka jua, dunia kujizungusha katika mhimili wake tunapata usiku na mchana tu.
 
Ungeuliza hivi! Nini kitatokea kama dunia ikianza kujizungusha?? Hilo ndio lingekuwa swali?? Kwakuwa haijizungushi na tunaona mambo yako poa tu, hivo swali lako halina swali ondoa alama ya ulizo kwenye habari hii
Wewe ulikuwa mtoro sana somo la jografia.
 
Sorry but this is future impossible tense....
Unajua watu hawajui kwamba hata kufikiria kuna mipaka yake. Ukifikiri kwa mipaka utajua muelekeo wa fikra zako. Yaani utajuwa huku kunawezekana na huku ni kinyume chake.

Kufikiria bila kuchunga mipaka ndio kumetuletea mabazazi wakana uwepo wa Mola muumba.

Kufikiria bila kuchunga mipanga kuna wafanya watu wafikirie kutokywezekana halafu wenyewe wakikaa pembeni wanasifiana na kupeana moyo ya kwamba amefikiria sanaaa. Kufikiri au kuuliza maswali yasiyo wezekana ni uchache wa elimu,kupoteza muda na kuikosea AKILI.

Inabidi tufundishane jinsi ya kufikiri.
 
Kuna mdau aliwahi kuuliza hapa kitatokea nini kama mtu akirudi kwenye tumbo la mamaaake... I was truly speechless
 
Kuna mdau aliwahi kuuliza hapa kitatokea nini kama mtu akirudi kwenye tumbo la mamaaake... I was truly speechless
Sisi kabla tulikuwa tunauliza maswali mfano wa hayo. Wasomi wetu wakawa wanatujibu hivi "Subirini itokee kwanza ndio tutawajibu"
 
Dunia ikisimama gafla maana yake ni
1.mfumo mzima wa ulimwengu utakua umeingiwa na interference
2.jua litakua limeloose its powers,forces na energy..maana jua litakua limezima
3.maana yake litakua halitoi tena mwanga na joto
4.maana yake hata its gravitational pull litakua halina tena
5.maana yake hata zile chemical reaction za fussion na fission ztakua hazifanyik tena,..nkimaanisha pale kwenye jua kila sekunde ni kama mabomu ya nyukilia trilion 1 yanalipuka kila siku hyo energy yake yaan
6.maana yake hakutakua na nguv za uvutano kokote katika ulimwengu..sabab nyota ztakua znakufa,kufa maana yake ni ku luz energy
7.maana yake jua likizima dunia ita freeze in a mata of seconds kila kitu kitakua barafu
8.maana yake vitu vitagongana gongana na kuvunjika
9.maana yake imagine unapogandisha kitu halaf ukakivunja,kitavunjika vipande vipande

Namalizia hzo ndo scenario ztakazo tokea,..na nyingne nying. Sjaziweka hapa. Sio kitu rahis rahis tu.

Na NINAPINGA kwamba tutarushwa nje huki kwenye outerspace..
 
hivyo vitu tunafikiria tu lakini haviwezi kutokea kwame,
uhakika huo tunaupata kwenye Zaburi 104: 5 "Ameiimarisha dunia juu ya misingi yake; Haitasogezwa kutoka mahali pake milele na milele."
 
Habari zenu tena.
Kama kichwa cha uzi kisemavyo, nini kitatokea endapo dunia itaacha kujizungusha ktk mhimili wake na kulizunguka jua ghafla na kutulia tuli, nini kitatokea? Wale wajuao in advance, please share nasi!

More to come!
Kiwango cha nishati za joto na mwanga kutoka moja kwa moja kwenye jua kitaendelea kubaki hivyo hivyo katika kila sehemu ya dunia kama kilivyokuwa wakati dunia inasimama. Kama dunia ilisimama wakati sehemu A ni usiku na sehemu B ni mchana, basi hali itaendelea kuwa hivyo hivyo. Kama sehemu C ilikuwa katika jua la 'utosini' na sehemu D ilikuwa katika jua la mawio, basi hali itaendelea kuwa hiyo hiyo. Vivyo hivyo, kama sehemu E ilikuwa ni masika na sehemu F ilikuwa ni kiangazi, basi hali itaendelea kuwa hivyo hivyo. Kwa ufupi, majira yatasimama kama yalivyo, na labda sehemu zenye giza basi mwanga pekee utapatikana kwa kuakisiwa kutoka katika unajimu mwingine kama vile nyota na mwezi
 
Nitatamani nirushwe Saturn.... My fav planet.
 
Lakini naona ni swali firikishi tu mfano unaweza kusema itakuaje kama Trump akatawala Tanzania na Anko Magu akatawala Marekani... ni kweli haiwezekani lakini je kama ingewezekana unahisi ingekuaje??

Ndio maana ya mtoa uzi.
 
Nimesoma RELATIVITY (both special and general) zile za albert einstein na pia QUANTUM MECHANICS lakini hakuna hata sehemu moja imekiri hichi kitu sa sijui hiyo uliyosoma wewe umezitolea wapi?
 
Mi nimezaliwa na akili kwa jinsi uelewa wangu ulivo sahihi sina mashaka na elimu yangu. Wewe uliyekaa kila siku dawati la mbele kudanganyika kwa vitu vya kizungu ni wewe,

Kama unatetea una akili ila ulishindwa pata maarifa na kuelewa kuhusu ulichoandika hapa chini na unaona uko sahihi kabisa basi kuna tatizo kubwa mkuu.

Nikufahamishe kuwa dunia tayari inajizungusha yenyewe ktk mhimili wake, inayosababisha tupate usiku na mchana.

Ungeuliza hivi! Nini kitatokea kama dunia ikianza kujizungusha?? Hilo ndio lingekuwa swali?? Kwakuwa haijizungushi na tunaona mambo yako poa tu, hivo swali lako halina swali ondoa alama ya ulizo kwenye habari hii
 
Sio kila jambo ni la kufikiria
Watanzania bana, ndio maana tunaambiwa kuna wajinga wengi.
Hicho kilichosemwa ni kweli kutokea sio rahisi ila fikiria endapo imetokea itakuaje. Mkuu Usiwe mvivu wa kufikiri kiasi kwamba unatafuta easy escape route, kama nilivyosema mwanzo. Ulikuwa mtoro darasa la jografia maana hujui hata usiku na mchana unapatikana vipi.
 
Lakini naona ni swali firikishi tu mfano unaweza kusema itakuaje kama Trump akatawala Tanzania na Anko Magu akatawala Marekani... ni kweli haiwezekani lakini je kama ingewezekana unahisi ingekuaje??

Ndio maana ya mtoa uzi.
Kwa kweli nashindwa elewa kwa nini watu wanakuwa wagumu hivi kumuelewa aliyeleta uzi.
Ni swali fikirishi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…