Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Habari mkuu. Hakikisha unaenda mahakamani.
Katika suala la talaka huwa ni LAZMA kabla ya kwenda mahakamani suala hilo lifike kwanza baraza la usuluhishi. Endapo baraza litashindwa kusuluhisha ndipo sasa mlalamikaji huenda mahakamani.
Sababu za mahakama kuvunja ndoa huwa ni
1. Ukatili(kipigo, matusi, nk)
2. Kumtelekeza mwenza
3. Kubadili dini iwapo ndoa ilikua ya kidini
4. Kushindwa kuchakatana
Nenda kaeleze namna ulivyochangia kuchuma mali mlizo nazo, kajitetee namna sababu za kuomba talaka kama zina mashiko.

Usiache kwenda maana usipoenda mahakama itaendelea na kwa kuwa hutakuwepo itakua ni ngumu ama haiwezekani kuchallenge chochote hata kama mwenza wako atakua amezingumza uongo.
Usisuse kwa ajili ya hasira, utanishukiru
 
MSALITI hasamehewi
Ibaki kua hivo tum
 
Ahsante mkuu. Katika sababu ukizotaja hapo, ya kwanza inanihusu. Nilimlamba vitasa baada ya kukuta picha za hovyo kwenye simu yake
 
Daah Naichukia taraka, watoto wanaenda kuishi na mzazo mmoja!, pole ndugu, nakutakia maamuzi yenye busara katika kuliamua hili.

.

Wengi wanaishi maisha ya sononi na kukosa Furaha sababu ya kuwaza kama wewe.
Maisha bila amani na Furaha ni Sawa na sifuri.
Watoto Mungu atajua jinsi ya kuwasaidia maisha yataendelea vema tu eventually.
Wanaishi yatima na machokoraa sembuse watoto wa kuishi na baba tu au mama yao tu.
Sasa Watu hadi wanafika pa kutoaminiana kutaka kuuana , wameambizana Maneno na matusi yote wamemalizana, umazani ni salama kuendelea kuishi dari moja ??!
 
Ni kwel lakin, japo kwa watoto inawapa shida hasa mwanzo ingawa after a while wanazoea.
 
Huu ndiyo uanaume!
 
Ahsante mkuu. Katika sababu ukizotaja hapo, ya kwanza inanihusu. Nilimlamba vitasa baada ya kukuta picha za hovyo kwenye simu yake
Nenda kadefend talaka mzee, usiruhisu jazba ukufanyie maamuzi. Kama kesi ipo Dar tuwasiliane PM lakini usiache kutokea mahakamani na hasa kuhoji uhalali wa yeye kuomba talaka
 
Power of attorney mkuu itapingwa kwa sababu atakuwa amewaandikia kukiwa na mgogoro tayari! Hiyo MAWAKILI watasema ni janja ya mwanaume! Kikubwa wagawane mbao tu!
 
Nenda kadefend talaka mzee, usiruhisu jazba ukufanyie maamuzi. Kama kesi ipo Dar tuwasiliane PM lakini usiache kutokea mahakamani na hasa kuhoji uhalali wa yeye kuomba talaka
Nimekuelewa mkuu, na nitakuchek Pm
 

Ni kweli wanawake wengine huwa wanawaroga wanaume zao uchawi wa sakizi.
Mwanaume wa Watu anajikuta anaondoka na nguo alizovaa mwilini tu anaacha kila kitu hata kama ni ghorofa 👌👌
Wanaume ni vile wanaona aibu kusema lakini wengi wamefanyiwa dhuruma kubwa na wake zao.
Iła mwanamke unaefanya hayo ni dhambi kumbwa sana na ujue Mungu atakulipa kwa dhuruma żako hizo.
Halafu ukiwakuta wanawake wakiongea utasema wameonea kumbe hakuna kuonewa.
Wanaume wanatembea wamebeba mambo mazito vifuani Wengine ndio maana wanaumwa visukari na presha, wengine wanapata ajali wanagonga Magari kwa msingi wa mawazo n.k
Kisa egi mwanamke amekuta meseji ya mchepuko Basi inakuwa nongwa hadi talaka na kudai mali. 🤔🤔
 
Nilikuta picha za hovyo kwenye simu hale karekodiwa ,nikataka ufafanuzi kwa amani tu ila akajibu shit, nikamchapa
Huyo mkeo ni mhuni tu ila ulikosea kumchapa....

Hupaswi kuwa na maamuzi ya hasira dhidi yake, achana naye kwa amani, nenda mahakamani mkamalizane kisheria kisha endelea na maisha yako ila chukua watoto wako ukae nao.
 
Hawa wanafanya wanaume tudharaulike asee🤣🤣🤣

Yaani nijenge nyumba kizembe tu nimwachie mtu
Wanaojua mziki wa kujenga wataelewa
Anazingua huyu!

Halafu wenzake wanachofanya baadhi ya vitu ambavyo mwanamke alimkuta navyo ambavyo ni vya thamani, wakiona mwanamke ameshaanza kudai talaka zile hatua za mwanzoni, wenzake huwa wanahamisha umiliki. Kama yupo baba yake anahamisha umiliki kufanya ni mali ya familia ili kulinda mali zake.


Mwanamke afanye yote ila mali zangu, hapana. Bora warithi familia yangu ukoo wangu ila siyo yeye!
 
Huyo mkeo ni mhuni tu ila ulikosea kumchapa....

Hupaswi kuwa na maamuzi ya hasira dhidi yake, achana naye kwa amani, nenda mahakamani mkamalizane kisheria kisha endelea na maisha yako ila chukua watoto wako ukae nao.
Mkuu ndio ilishatokea tena hivyo
 
Ahsante mkuu. Katika sababu ukizotaja hapo, ya kwanza inanihusu. Nilimlamba vitasa baada ya kukuta picha za hovyo kwenye simu yake
Yani ndo kilichomkimbiza mahakamani hiki😳,,nenda mahakamani naamini huwa haitoi maamuzi hapo hapo,kuna muda mtapewa wa kujitafakari huku mkiendelea kuishi pamoja,,,,,, nasema ivi coz nna ushuhuda wa wazazi wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…