Umenikumbusha mbali sana, nilizaa na mwanamke, nikaamua kuishi naye bila kufunga ndoa, (sukutaka kufunga ndoa haraka haraka) nilimtambulisha kwetu na Kwao nilienda kujitambulisha nikaishia hapo.
Miaka kadhaa baadaye nikagundua Ana-date x wake, nikathibitisha pasiposhaka kwamba ameliwa siku tatu mfululizo! (Aliniaga anakwenda kusalimia Msiba wa shangazi yake, kumbe anaenda kuliwa na jamaa yake wa zamani)
Nilimuuliza baada ya kujiridhisha na ushenzi aliofanya, akawa mbogo hataki kuulizwa chochote, nikaamua kufanya maamuzi magumu, nikamwambia NITALEA MTOTO na wewe uendelee na mahusiano yako, akanijibu sheets za maana! Nikalazimika kujizuia kumpiga ili nisiingie kwenye kesi isiyo na ulazima!
Nilipomuacha cha kwanza akakimbilia mahakamani, alipoulizwa anataka nini akasema anataka tugawane mali ili akaendelee na maisha yake, nilipoitwa nilienda, nikawaambia sijawahi kumuoa huyo mwanamke zaidi ya Kazaa naye, hivyo nitawajibika kmtunza mtoto tu.
Alipotakiwa kuthibitisha mimi kuwa mume wake akasema tumeishi pamoja zaidi ya miaka 2, nikwaambia sijawahi kuishi naye kwa hata miezi Sita Kwani nilikuwa nafanya kazi mahali tofauti na palipokuwa na makazi!
Baada ya purukushani nyingi na matusi juu, hatimaye nikapewa jukumu la kutunza mtoto!
Kwa kuwa Ali kuwa jeuri, mtoto alikuwa na miaka 9 nikaiomba mahakama inipe idhini ya kuishi na mtoto, nikakubaliwa!
Ameridi mwaka Jana December, kuniomba msamaha na kutaka turudiane, nikamwambia asithubutu kuniletea ushenzi, nisijeondoka na shingo yake! Anajiliza liza mpaka leo kutaka turudiane!