Nini sababu ya Matajiri wengi kutokuwa wakweli juu ya utajiri wao?

Mkuu samahan IVi ni Kweli, kwenye vituo vya police ya TZ, mahabusu Bado wananyea ndoo AU debe,
 
Umeeleza vema mkuu
 
Hata wewe ukitoboa utasema ulikua unalala njaa. Mo alisema alikua anaenda shuleni peku ila kasoma IST.

Bakhressa alianza kuuza ukwaju Leo ana viwanda. Wewe ukianza kuuza ukwaju Leo hadi unakufa hununui hata vitz.
Na wewe ukifanikiwa utatuambia ulikuwa unatembea kilometres 10 kila siku kuuza mboga za majani leo ni billionea 🤣🤣🤣
 
Ambao sio ukweli ni upi hapo?
 

1. Niffa alianza na elfu 40
2.Shamim Zeze Alianza na elfu 10
3.Super Feo alianza na ELfu 20
4.Dotto Magari alianza na mtaji wa mia 5 ya bando
5.Issa Tambuu alianza na mtaji wa elfu 50.
6.Bakresa alianza na kushona viatu
7.Mo alianza na mtaji wa usd 1m.
8.Musukuma alianza na mtaji wa afu thalathini.
9.Kishimba alianza na mtaji wa afu 6.
10.Vunja Bei alianza na mkopo wa milioni 3.
 
Alhamduli:Llah Bakhressa nalifahamu mpaka duka lake aliloanza nalo la viatu.

Kishimba nafahamu duka leke Mwanza na Mzee aliekuwa anamkopesha bidhaa za kuweka dukani namfahamu.

Kishimba ni mtu mwaminifu sana. Hilo nalifahamu sana.

Bakhressa ni mtu ambae kawanyanyua kimaisha wale waaminifu wote ambao kaanza nao kazi, wengine na wao ni matajiri sasa, wengine wana hali nzuri, wengine wanalalamika kama kawaida ya binadam, Wengine hawataki hata kumsikia, wanasema hakuna bahili duniani kama yeye.


Ili mradi binadam duniani hatukosi kasoro.
 

Ni kweli unayoyasema ila behind the scene na ku-make fortune si viatu wala maduka yao!! SSB anatajwa sana kwenye poaching ,Musukuma udhulumati wa madini ,kishimba anatajwa sana kurun bizness za Vigogo wa serikali kwa kupitia jina lake kwakuwa ni muaminifu hapo hapo na yeye akajiongeza.

Kuna jamaa mmoja maeneo flani alikuwa ana duka tu kubwa la nguo anatoka kanda ya kaskazini ,alikuwa pia ana duka genge ,anauza mkaa ,maji na vitu vingi vingi ,lilijaza balaa akajenga nyumba mbili enzi hizo tulikuwa tunaita "SEFU KONTENA" ,jioni alikuwa anasema anafanya kazi ulinzi kumbe behind the scene alikuwa "MANDONGA MTU KAZI SHOW SHOW aka MZEE WA MJEGEJE" ilikuja kubainika baada ya kushikwa kwa ujambazi....Kwahiyo kuna baadhi ya watu wanafanya biashara front kucover ufirauni wao wa nyuma.
 
NbxHuyo Mungu Alishindwa na Anashindwa kuwapa hata chakula Maelfu ya watoto, waake na wazee wanaokufa kwa njaa wakilia na kumuomba awasaidie,

Halafu ndio unasema huyo Mungu anagawa utajiri?

Utajiri gani
View attachment 30783855
Kwa hiyo kiongozi uamini kuwa dhahabu na kila kitu hata wewe mwenyewe unatoka kwa Bwana.?

Naye Bwana Mungu ndiye mgawaji wa riziki.
 
Ilimasikini muendelee kuwepo
 
Kwa hiyo kiongozi uamini kuwa dhahabu na kila kitu hata wewe mwenyewe unatoka kwa bwana.? Naye ndio mgawaji wa ridhiki.
Kwanza siamini kwenye kuamini. Sina imani ya aina yeyote ile.

Huyo Bwana hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Hakuna mtu au kitu chochote kilichotoka kwa huyo Bwana.
 
Mtu anasema alianza kwa mtaji fulani, wewe unabisha! Sasa unataka akuambie nini?

Wafanyabiashara wengi huanzia chini sana, ila character zao ndiyo huwajenga kibiashara mpaka wanakuwa na mafanikio makubwa.

Watu wasio wafanyabiashara hudhani mpaka uwe millionea ni uanze na mamilioni.. hawawezi ku-imagine process nzima ya kutoka chini kwenda juu, so huishia kusema wanadanganywa.
 
Ni kweli kabisa kama ulivyo eleza kwa kina kuwa mtu anaweza kuwa alianza na mtaji anao sema ila process hapo

katikati ya kumfanya awe alivyo sasa kimafanikio ndio zinawekwa sirini ndio tuna shauri vijana wapambane kwa uwezo wao wasiamini sana story zao.
 
Hii ya kutakatisha pesa matajiri wanatumia sana ila siamini katika utajiri wa masharti kama ipo ni nafasi ndogo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…