Nini tafsiri ya mabinti kuzaa wakiwa bado wapo kwa wazazi?

Kwaio unataka kuniambia mzazi akiona mwanae ni mjamzito ampeleke kutoa??? Vile mtoto akinyea kiganja......... Hizo habar hata maadili yawe ndoo zima akili ya mtoto hapo......

nafikir hujamwelewa huyo Eli79 anamaanisha watoto hawajengwi kimaadili badala yake wanaendekezwa kwa tamaduni za kizungu kitu ambacho watoto hukosa maadili mema, hebu imagine mtoto anakuja amevaa kinguo hicho kimebana na mzaz anasifia, mtoto anamleta mvulana eti huyu ni boyfriend wangu na mzaz anachekelea tu, mtoto mda wote yeye club mzaz anakenua tu.
Hapo unafikir matokeo yake ni nn?
 
Last edited by a moderator:
Wamwera wanaishi mkoa gani?
 
Asante Mgirik kwa ufafanuzi..! MankaM alidhani nam attack.
 
Last edited by a moderator:

Kwa fikra zangu kosa lipo kwa wazazi wenyewe kutokuwa makini katika uangalizi wa watoto wake.
Au ni matokeo ya historia ya wazazi wenyewe ambapo ndio hayo hayo waliowafanyia mabint wa wengine.
Au watoto kupewa uhuru wa kutosheleza kufanya watakavyo.
Au mapenzi ya mzazi kwa mtoto wake mpaka anashindwa hata kumkanya.
Au ni familia isiyo na uwezo wa kiakili ambayo haiwezi kupambanua kati ya pumba na mtama.
Au hali ngumu ya kimaisha waliomshikisha bint katika kupata mahitaji yake ya lazima ndio sababu ya yeye kuamua kuyatafuta mahitaji hayo nje nako hakuna cha bure
 
Kwahili wazazi wanachangia sana nakumbuka mwaka 93 dada yangu alipewa mimba akiwa home mzee akamtimua akakimbilia kwa bibi akamfata kule akamtimua nikawa namwambia mzee sasa ataenda wapi msamehe akanijibu ataenda kwa aliempa mimba halafu akasema kuwa akimuacha pale itakua chanzo cha waliobaki kuiga tabia hile wataona dada alipewa mimba hakufanywa chochote ndomana mzee akaamua kumtimua ilikuwahofisha waliobaki kweli ilifanikiwa waliobaki woote wameolewa freshii kabisa sasa siku hizi mtoto anapata mimba unamsapoti
 
Nimekusoma ndugu Mgirik Merry Christmass
 
Last edited by a moderator:
Kusema kweli sisi wazazi ndio tunachangia sana tunajifanya kuwapenda watoto wetu na uzungu mwingi tofauti na maadili yetu pia kama mtoto hawekwi kwenye misingi ya imani ya dini toka akiwa mdogo uoga unakuwa mdogo sana kwenye ngono

Hapana manake uswahilini ndo kuna rate kubwa ya mabinti kuzalia nyumbani, tena wakiwa na umri mdogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…