Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Kama wewe una elimu ya uhandisi umeme, nakushauri urudi chuo. Hesabu yako na huo mfano wako wa A/C ni ya kinadharia, maana ingekuwa uhalisia umeme unaozalishwa nchi ingekuwa gizani.
 
Bila
Bila kupunguza ladha ya maelezo yako mazuri yenye wingi wa busara. Wakati tunaimbushwa uchumi wa gas kama mwendawazimu, nyie mlikuwa kimya. Tuliambiwa kuwa mradi huo tutaweza kuzalisha 5,000m na ziada kuuza nje. Sasa nashindwa kuelewa iweje Magufuli aliyekuwa kimya mpaka tukakopa 1.5t kuwekeza kwenye gas, kwanini asipinge mradi huo na kusema wa maji sio sahihi?

Sasa hivi anakopa kimya kimya kisha anasema analeta umeme wa bei rahisi, ambao ni 2115m, anaacha kuwekeza ulioanza wa gas wenye 5,000m! Je ni kwanini hizo 6.5t zisiwekezwe kwenye mradi wa gas ambao umeshaanza, ule tulikuwa tunaimbishwa kama watoto wa shule ya msingi? Je akija rais mwingine akasema umeme wa upepo ni mrahisi zaidi, akaachana na huu wa maji nani atalipa deni la huo mradi mwingine?
 
Kuna porojo mbili umeongea:

1. Porojo ya kwanza ni kudai kuwa unit 565 zitabaki kwa hiyo zinapaswa kuuzwa.Hii ni porojo kwa sababu usichokijua ni kwamba huo umeme wote wa Stiglers Gorge bado ni mdogo sana kwa sababu kila mwaka idadi ya watu wanaongezeka na kuongezeka kwa idadi hiyo ya watu kunaambatana na kuongezeka kwa matumizi ya umeme majumbani, viwandani, madukani, mashuleni, kwenye vituo vya afya,etc

2.Porojo ya pili ni kudai kuwa mradi huo unatengenezwa kwa fedha zetu za ndani
 
'Mafuriko' ya 'Miradi' mingi nchini haina 'Tija' sana kama 85% ya Watanzania wanalia Njaa, Ajira hakuna, Elimu duni na Uchumi kuwa Duni sana tu.
Serikali haiwezi kutoa ajira kwa wote wanaohitaji ajira ila kuweka mazingira ya kujiajiri. Hii ni pamoja na kujenga vyuo vya VETA.

Karibu zaidi ya ¾ ya vijiji nchini vinapata umeme. Vijana wajasiriamali waliopata na watakaopata mafunzo wa stadi za maisha VETA, watajiajiri kutoa huduma huko huko vijijini km kufanyia matengenezo vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi, birika za umeme nk. Au hilo hulitambui unasubiri kuajiriwa! Serikali haiwezi.
 
tupe hizo mashine zinazochoma gas mkuu ambazo ni sawa na inavyochomwa petrol, na unisaidie hizi tulizonazo ni aina gani ya turbine kitaalam na hizo unazodhani ndo gas turbine ambazo zingetufaa hebu zilielezee operation yake mtaalamu. nataka niongeze elimu kidogo kwenye hii tasnia nahisi kile kidogo nachokijua kinapwaya baada ya kuona comment yako hii
 
Hesabu za asiekwenda shile ndo hizo swali ni je hio unit moja kwa 36tshs itaanza kutozwa baada ya muda gani? Ukizingatia kuna kurudisha gharama za huo mradi/mkopo/ etc?
 
ALL in ALL... alternator au kinu kinachofua umeme kinahitaji mzunguko ili kizalishe umeme (Rotation). Mzunguko huo unaweza ukaupata kwenye upepo (windmill), mechanical engine (petrol ro diesel engine) maporomoko ya maji (water turbine - hapa akina Kidatu wanahusika), steam engine, GAS TURBINE ETC

Majenereta yaliyopo Mtwara mjini yote yanachoma gas kama inavyochomwa petroli au diesel ili kupata MZUNGUKO utakaozalisha umeme. Gas hiyo ikishachomwa, ndo mwisho wake, kama ambavyo diesel ikishachomwa ndo basi tena huwezi kuwa na diesel hiyo..

Kwenye turbines, ntaanza na water turbine... maji yanayoporomoka sehemu, kwa sababu ya HEAD (umbali toka mporomoko yanapoanza hadi maji yanapokwenda kutua) maji hupata na energy... sasa maji hayo yanayoporomoka, yakipelekwa kwenye gurudumu (turbine) yatalizungusha, and hence alternator iliyounganishwa na turbine hiyo itazalisha umeme. Kwa maji, yakishazungusha turbine, yanaweza yakatumika tena kwenye maisha ya kila siku ya binadamu mfano uvuvi, kilimo etc

Sasa kwa gas, gas yenyewe huwa inatoka huko ardhini ikiwa na high pressure. Pressure hiyo inaweza ikasukuma gurudumu linalohimili gas (gas turbine) na rotation ikapatikana na mwisho umeme kuzalishwa. Kama ilivyo kwenye maji, gas iliyokwisha tumika kuzalisha umeme, inaweza ikatumika tena kwenye shughuri za kibinadamu mfano viwandani (kama ilivyo kwa TBL, wazo cement etc), ingeweza kusambazwa majumbani kwa kupikia etc.

Sasa kwa hali ilivyo sasa, tunachoma gas na hivyo ukitaka ya matumizi mengine lazima uichimbe upya...

ALL IN ALL, SHIDA KUBWA NI SIASA
 
Bahati mbaya kubwa tuliyonayo watanzania ni kwamba...

1. Wanaojua madini hasa yale makinikia pale KAHAMA MINING YAPOJE na nini hasa kilitokea, ni wachache sana nadhani hawazidi wataalamu laki 2 OUT 55M... ( NAZUNGUMZIA WANAOJUA MAMBO HAYO KWA UHALISIA WAKE)

2. Wanaojua GAS na nini hasa kilitokea, ni wachache sana nadhani hawazidi wataalamu laki 1... ( NAZUNGUMZIA WANAOJUA MAMBO HAYO KWA UHALISIA WAKE)

NA HAO WOTE HAWANA PLATFORM YA KUSEMEA... sasa akitokea mkubwa mmoja akaanza kuwadanganya watu wanadanganyika haswa....
 
sikuwah kuelewa kuhusu megawats
 
Nawaoneaga wivu wazungu, wao kila jambo linalowahusu ktk Taifa liwe la kisayansi,kiuchumi,kisiasa wana taarifa za kutosha,faida,hasara zake n.k wananikosha sana ukiona wanavyochangia mijadala ya masuala mtambuka!! Huenda ni ELIMU ELIMU ELIMU au ni UWAZI wa serikali zao sijui!

Lakini njoo tz! Watu hawana habari na kinachoendelea wala kinachopaswa kuendelea! Ndio maana wanasiasa wanatumia muanya huo kutuhadaa siku zote
 
Electrical engineering analysis inafanywa kisiasa jukwaani hapa huo uliofanya ni uhuni na kudharau taaluma zetu tuliokaa darasani 4 years
Kukiwa na kiongozi dhaifu anayetoa maamuzi dhaifu, taaluma huwekwa pembeni na valaza hujitokeza kuwa washauri wa kiongozi na kwa bahati mbaya wanageuka kuwa wataalamu wa kuwafundisha hata wasomi. Kuhusu umeme wa Stiegler's Gorge ni kweli ulikuwa Mradi wa Mwalimu lakini si kweli kuwa alishindwa kutekeleza bali aliheshimu mikataba ya Kimataifa na kuiridhia badala yake akajenga Mtera kusaidia kuhifadhi maji kwa ajili ya Kidatu. Miaka mingi baadaye, Serikali ya Awamu nyingine ilijenga kwa ubabe Bwawa la umeme la Kihansi ingawa kulikuwa na upinzani mkali wa wanamazingira wa ndani na nje ya nchi mpaka Marekani ikajitolea kuhamisha na kuwahifadhi vyura ambao hawapatikani popote duniani. Vyura walirudishwa baada ya Bwawa kukamilika na kujazwa maji lakini wananchi hawaambiwi hali ya vyura wala Bwawa lenyewe halizungumzwi kabisa inawezekana lina matatizo. Mabwawa yote manne ya Kidatu, Mtera, Kihansi na linalojengwa la Nyerere yako kwenye mto mmoja na endapo mto utakosa maji ya kutosha nchi nzima itakosa umeme kabisa na ishara zinaanza kujitokeza kupungua kwa maji. Ruaha tawi muhimu la mto Rufiji linalotoa maji kwenye Bwawa la Mtera maji yameanza kupungua sana ingawa TANESCO hawasemi na Bwawa limeanza kujaa tope kutokana na kilimo cha umwagiliaji cha mpunga kwenye chanzo cha mto. Swali la kujiuliza ni, je hakuna vyanzo vingine vya kuzaliwa Umeme?
 
Mkuu mchakato wa kufanya hili suala unaendelea na TPDC walishatangaza tender nadhani sasa ipo kwenye design stage kwa ajili ya kujenga Mother & daughter stations for CNG, watumiaji wakubwa watarajiwa watano ambao ninawafahamu so far ni pamoja na kairuki pharmaceuticals (kibaha), feri, muhimbili, Dart(Brt ubungo) pamoja na Hawa jamaa wa afya (kigamboni), project ipo njiani na mother station itajengwa pembeni ya magufuli hostel
 
Gereja Akiwa Waziri Alikuja Na Fix Tele Kuhusu Megawatt Mpaka Wananchi Wakawa Hawaelewi Lolote
 
Tatizo linalosababisha sana kwa sasa umeme kukatika sio uhaba wa umeme ni kiundombinu iliyochakaa ya tanesco katika baadhi ya umeme pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wake katika kutimiza majuku yao ikiwemo usimamizi wa mitambo
 
Sina Imani na kila ulichosema wewe hapa.
Lakini walau umeweza kuonyesha kwamba uchambuzi wa mtoa maada umekaa kistori ya kumsimulia mtoto mdogo.

Maana huwezi ongelea mahitaji ya mikoa Kama Lindi, kuweka katika halibya uhalisia wakati tunajua mikoa hiyo sio kila Kaya ama kila pahala wamefikiwa na umeme hivyo ili kila mwekupaswa kufikiwa afikiwe mahitaji yatao gezeka.

Pili unapoongela swala la maendeleo ya kisasa mahitaji ya nishati yataongezeka, maana yake hata hao wa Huko Lindi watahitaji umeme zaidi ya wanavyohitaji Sasa hivi kadri wanavyozidi kuendelea kiteknolojia.

Pili. Watuwakufanya uwekezaji huko mahitaji yatakua Makubwa zaidi. Hapo nimeongelea huko Lindi , Mtwara.
Sasa Mikoa mingine????....

Tatu. Hiyo Bei ya sh. 36 haijaifafanua . Ni gharama ya uzalishaji tu.

Je Hapo RIO inakuaje.
Maana Kama mwenyewe amesema gharama ya mradi Ni Tr 6. Tsh. Hiyo pesa bila shaka Kuna kiasi cha mkopo. Au hata Kama hamna lazima kwa namna moja au nyingine baadhi ya gharama irudi.
Plus maintenance na gharama nyinginezo ambazo serikali itataka Taasisi izigharamie yenyewe lazima zitaingia kwenye Bei.

Bado serikali yetu tunayoijua.
Kutakua na ewura, Rea( au sijui wakati huo itakua nini) bado Kodi , ama yawezekana kukainguzwa na kitu kingine.
Hivyo hiyo hadithi ya juu bado mtu aliye timamu na anaelewa Siasa hizi na Serikali inaendaje. Hawezi kununulika kw ahafithi hii
 
Sio muda wake!
 
Hawapo seriaz hawa watu tuwapotezee tuu
 
Upeo mdogo wa kuchambua mambo, megawhat 2,115 Ni kaproject kadogo tu.ni vile tu uchumi wenu Ni mdogo, ongelea megawatts9,000

Alafu mbwembwe nyingi mbona hamsemi 1KWh mtauza kwa shilling ngapi mradi ukikamilika?
 
Kelele tu bado we ni masikini sana
 
Ukipata nafasi na ukiona ni muhimu pitia ripoti iliyoambatanishwa hapa kuhusu mradi wa gesi na matumizi yakeView attachment 1598093
Soma kiambatanisho hicho kuhusu Mafuta na Gesi Tanzania, utapata majibu ya hoja/maswali yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…