Nini tafsiri ya Megawatts 2,115 za umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiegler's Gorge)?

Megawatt 2115 ni umeme mwingi sana maana ujanja mzima wa umeme upo kwenye transformer na copper wire za kusafishia unaweza ukabalance transformer zako ukajikuta Tanzania tunatumia megawatt 1000 tu na mambo yakasonga. Kupata hydropower at once ya zaidi ya MW 2000 huo ni ushindi sana
 
Sasa naomba unieleweshe Kama tutauza hizo megawatts 500 ...tutajuaje Kama ni megawatts 500 zimeenda huko...je hawatakula nyingi tukajikuta tuko kwenye shida tena?
Mbona unajua bill yako ya umeme unayolipa nyumbani kwako? Ni kipimo hicho hicho kinachotumiwa wakati wa kuuza huo umeme
 
Hilo bwawa la Nyerere limetumia eneo la asilimia tatu tu la eneo lote 3% sionioni kwa nini watu wasemeseme kwa kaeneo kadogo hako.
 
Mwegeso..umeongea vyema kabisa. Lakini reserve ya maji itategemea na uwepo wa feed up channels..labda kuwepo na chemichemi ya kudumu ambazo pia msimu wa kiangazi hupungua uwezo wake wa kutoa maji. Unakumbuka kukauka kwa mabwawa miaka ya 2007-2008 ikaletelezea Richmond saga? Waswasi wangu uko hapo Mwegeso. HEP easy and cheap but very unreliable kutokana na kutegemea single sources of water resources hasa kwa sisi Tanzania. Mabadiliko ya tabia nchi na yenyewe hayatabiriki sana kutokana na population. Tuombe kama unasema kusitokee majanga ya mazingira. Lets hope all factors are constant then bwawa la Stigler gorge litadumu milele.
 
Kama tofasri yako ni sahihi swali ni hili
Kwanini umeme unakatika?
Wakati wastani wa matumizi ya Umeme mikoa yote ni megawatt 1,550 bila umeme kukata
Na Kinyerezi huzalisha 1,560 megawati hivyo salio hubaki kadirio la 10megawatt.
 
Mkuu South Africa pamoja na umeme wa nyuklia lakini Wana power cut au mgawo mwaka huu wote yangu mwaka Jana.

Umeme huwaga hautoshagi. Na gharama za kupatikana kwa wananchi ndio shughuli pevu
 
Mbaya zaidi, wengi wa wanaobishana humu jukwaani ni full siasa... unabaki unashangaa tu... mtu hata kwenye unit anaandi 2115m akimaanisha 2115mW... yaani ukiona mtu anaandika mw (millwatt) badala ya mW (Megawatt) ujuwe hajui units za power lakini ubishi unashika hatamu.. wataalamu hawapewi nafai... hasa kama TECHNICAL OPINION ya project husika ITAKWENDA TOFAUTI NA MATAKWA YA MTAWALA..

Tunajua wa mazingira almanusura yamkute na NO zake za kistigla
 
Mkuu South Africa pamoja na umeme wa nyuklia lakini Wana power cut au mgawo mwaka huu wote yangu mwaka Jana.

Umeme huwaga hautoshagi. Na gharama za kupatikana kwa wananchi ndio shughuli pevu
Kwani kuwa na nyukli maana yake mna umeme unaowatosha wakati wote..?
 
ha ha haa aaaaaaaa, sasa ni wakati muafaka JF waongeze kitu kingine cha kubofya ili kuwapa notisi kwa watu wanaoposti upumbafu na ujinga uliopitiliza,utakuta Mtaalam Bingwa aliyebobea anabishana na watu wa "miliwatts"
 
Hilo bwawa la Nyerere limetumia eneo la asilimia tatu tu la eneo lote 3% sionioni kwa nini watu wasemeseme kwa kaeneo kadogo hako.

..hoja yako ni nzuri sana na nimewahi kuisikia ikitolewa na Raisi.

..sasa moyo wa binadamu ni 0.69% ya uzito wa mwili wote.

..miguu ya binadamu ni 20.37% ya uzito wa mwili wote.

..sasa madaktari wakikwambia wachomoe moyo, au miguu, utachagua nini?

..hoja ya kutetea au kupinga bwawa la umeme haitakiwi ijikite kwenye ukubwa wa eneo la mradi peke yake.

..hoja inatakiwa iwe ni eneo la mradi lina umuhimu / athari kiasi gani kwa bonde zima la mto rufiji.

..kwasababu ujenzi umeshaanza, basi tunatakiwa tuwe na taarifa za kina za athari za kimazingira, na pia tupange mikakati ya kukabiliana na athari hizo. hakuna bwawa la umeme lisilo na athari kwa mazingira, cha msingi ni kiwango cha athari hizo, na mbinu za kupambana nazo.

cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Salary Slip
 
Tujulishe pia kuhusu athari zake za muda mrefu kimazingira. Tulipopata umeme wa bwaws la mtera tuliambiwa tatizo la umeme lingeisha. Haikuchukua muda ukaja ukame wa msimu 97/98 bwawa likapungua maji tujaingia kwenye mgao uliotuingiza kwenye mkenge wa IPTL na DOWSNS. Tuna uhakika gani na uendelavu "sustainability" wa umeme huu hasa ukizingatia kwamba asilimia zaidi ya 90 ya maji yake yanategemea mito ya Ruaha mkuu na Kilombero anbayo maji yake yaneshaanza kupungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uharibifu wa mazingira?
 
Hilo bwawa la Nyerere limetumia eneo la asilimia tatu tu la eneo lote 3% sionioni kwa nini watu wasemeseme kwa kaeneo kadogo hako.
3% ya Tanzania nzima? Hivi unajuwa ukitaja kwa percentage watu wanaweza wasipate picha halisi ya eneo lililofyekwa... MWAMBIE MTU ENEO LILILOFYEKWA NI SAWA NA UKUBWA WA DAR ES SALAAM YOTE... sasa ukijumlisha na vilivyoondolewa (bearing in mind kuwa ni mbuga) ndo utapata picha kubwa ya kilichofanyika.. Viumbe hai wote wameswagwa mbalii na operations zitakazokuwepo during production ndo kabisaa..!!!

Jaribu kuwaza pia.. Loriondo ni percentage ngapi kwenye ukubwa wa eneo la Tanzania? Je! kwa sababu ni kaeneo kadogo ka Tanzania, NI SAWA ILIVYOUZWA, KWA VILE NI KADOGO?
 
KIONGOZI...... Five years years to come, we will be back to square one...
 
Kama wewe una elimu ya uhandisi umeme, nakushauri urudi chuo. Hesabu yako na huo mfano wako wa A/C ni ya kinadharia, maana ingekuwa uhalisia umeme unaozalishwa nchi ingekuwa gizani.
Hawa ni wanachuo ndo wamekaririshwa, [emoji3][emoji3] Aibu nimehisi mimi asee
 
Nimesema eneo la Mbuga ya Selous
 
Moja ya mada zenye mashiko hapa jf siyo kulslamikaga tuu..hongera mleta mada hii ...natabiri baada ya mradi tutanunua jogoo wa Singida kwa 5000/- tuu ,2030 Tanzania itapelekea msaada wa chakula nchi za Kenya, Sudani,Ethiopia,Somalia .. Kauli mbiu itakuwa kwa msaada wa watu wa Tanzania! #Tz Aid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…