Nini unapaswa kufanya ili kuepuka kulea watoto ambao sio wako?

Nini unapaswa kufanya ili kuepuka kulea watoto ambao sio wako?

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Kuna hili suala nafikiria mara mbilimbili.

Mwanaume aliyelea watoto na kuwasomesha halafu mwisho wa siku anakuja kugundua watoto hao sio wake, kumbe mke alisha cheat tangu zamani, sipati picha atajisikiaje. Kivyovyote vile hiyo feeling itakuwa ni mbaya kuliko hata kuumwa

Now, huwezi kulaumu watoto, kosa sio lao, lakini unaweza kumlaumu mwanamke kwa kutokukuambia, labda kwa hofu kuwa ungemuacha, ila miaka imepita umeshatumia ujana wako kuwalea hao watoto, ila kiuhalisia wewe huna chako hapa duniani. Labda ulikuwa unatamani ulete chata yako hapa duniani na umri umeshaenda tayari, mwanamke amekupotezea muda wako mwingi

Sasa kuepuka haya yote, unapaswa kufanyaje?
Watu wanasema oa mwanamke anayejiheshimu, na unayemuamini. Wewe utajuaje kama huyu anaaminika? Unaweza kumuamini 100% kwa sababu anakuigizia kukupenda au huenda ni mtu mwema outside ila ndani yake huwezi kujua. Kuna watu wengi tu waliwaamini wapenzi wao na mwisho wa siku wakaja kuwa cheated, sio kingono tu bali hadi kulea watoto ambao sio wa kwao, huku baba yao halisi yupo somewhere anakula maisha, probably anaendelea kupelekea moto wake za watu

Na pia nikifikiria kama ukitaka kupima DNA kwa kila mtoto atakayezaliwa, mke wako ataanza kuhisi haumuamini, itapunguza kuaminiana kwenye ndoa

Je unapaswa kufanya nini kuzuia kulea mtoto ambao sio wako, maana nikifikiria naona ni kitu cha kutisha mno
 
Huku kwa masai,mfano; mke wangu wa ndoa hata akizaa na mume mwingine mtoto ni mali yangu daima, huyo mwanaume hana mamlaka wala namna yeyote kujaribu kusema mtoto ni wake!!
Na hata mke akichepuka ili mradi tu huyo mwanaume awe ni rika langu, kama si rika nikaenda shtaki kwa wazee hapo faini mtu atakula chapu 😂
 
hiyo dhambi acha Mungu mwenyewe aingilie kati, kuna uchungu usiolezeka ukishajua mtoto/watoto sio wako ni ngumu sana kuishi nayo ila pia ni rahisi sana kama ukimkabidhi Mungu uzito wa uchungu ulionao,hakika watoto hawana hatia huwezi kumwambia mtoto mimi sio baba yako mtoto aliezoea kukuita baba hiyo ni dhambi na ni ukatili kuliko hata mkeo aliekusaliti,
 
Huku kwa masai,mfano; mke wangu wa ndoa hata akizaa na mume mwingine mtoto ni mali yangu daima, huyo mwanaume hana mamlaka wala namna yeyote kujaribu kusema mtoto ni wake!!
Na hata mke akichepuka ili mradi tu huyo mwanaume awe ni rika langu, kama si rika nikaenda shtaki kwa wazee hapo faini mtu atakula chapu 😂
utamuduni mzuri wamasai mna akili sana
 
Unadhani kuepuka rahisi basi, hawa viumne wasipokupenda hazai na wewe ng'oo. Anaweza kufanya kila hila asibebe mimba, akaja kubeba ya mwingine anayempenda.

Ukiona hadi kabeba mimba jua kaitaka na wala si bahati mbaya. Mpaka aje kukubambikia watoto si wako kama upo sawa kiafya elewa hataki kuzaa nawe.

Kuepuka hayo mambo ni wewe kuangalia na mwanamke wa kuanzisha mahusiano naye. Usipemde kutumja nguvu au hila kulmpata mwanamke na hana hisia nawe
 
Serikali ingekuwa na utaratibu anapozaliwa mtoto hospital kabla ya kuruhusiwa vingefanyika vipimo vya DNA bure kabisa,ili wakitoka hapo wawe Safi.

Unajua watu kila siku wanaumiza kwa jambo ambalo linge epukika
 
Mambo yote huwa yapo usoni kwao Miwani mnazojivisha ndio zitachagua na kuchangia aidha uyaone au ukikute Steve wonder ukalie mbele ya safari.

Kumbuka Hata Ambulance huwa inalia huku inaondoka.

Usiwe Fala kaa kimaster.
Stay hard Stay safe.
 
Back
Top Bottom