Nipeni maua yangu - Roma Mkatoliki
Kama hujapata kusikiliza wimbo wa Roma Mkatoliki basi hujachelewa;

1. Jeshi gani limeishindwa kumtambua Kigogo?

2. Nchi wameifanya mti.

3. Mbona mama anarudia kilemba? Afu mbona vyuma vimekaza afu mama anaificha ndizi?

4. Mimi sio CCM wala CHADEMA ilo niliweke wazi, nikiwekewa CCM na andazi mi nitachagua andazi.

5. Amjasikia remote iko Msoga?

6. Jimbo hili aliendelei kisa mlimchagua mpizani basi shinda na huu mtihani.

7. Wengine mmewaona viongozi wakazi walikuwa marapa (Mwana FA).

8. Vijana siasa ndio inaweka kila kitu safi.

9. Anayechelewesha mshafara ni ng'ombe wa mbele ila anapigwa wa nyuma ili apige kelele [emoji120]

Ujumbe Toka Kwa Roma Mkatoliki.

....... Tanzania Yangu......

View attachment 2593500

“Vyuma vimekaza afu mama anaficha grease”
 
Kama umepata wasaa wa kuusikiliza wimbo Roma mkatoliki nipeni Maua yangu..Apo kwenye verse alioimba ngolo kante anampa mbappe krosi anafunga Pogba alikuua anamaanisha nn???
 
Kama umepata wasaa wa kuusikiliza wimbo Roma mkatoliki nipeni Maua yangu..Apo kwenye verse alioimba ngolo kante anampa mbappe krosi anafunga Pogba alikuua anamaanisha nn???
Yaan hiyo ni kombineshi.... perfect kombo....
😊😊😊
🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Huyu mwamba harudi tena bongo
Ndo mpango wake boss .Anataka maisha mazuri.Anataka watoto wake wapate green cards.Anaendelea kujustify kuwa anastahili kuendelea kuishi Marekani kwa ajili ya usalama wake...
 
  • Thanks
Reactions: K11
Roma ana miziki michache sana ila anazo hotuba nyingi nzuri.Ameongeza hotuba nyingine nzuri kwenye maktaba yake.....Watu wengine ambao wana hotuba kali ni akina Mdee,Lema Mbowe,Mnyika,Wenje,Bulaya,Heche nk..
 
Ile sanaa ya jamaa ni noma sana, kuna sehemu alisema sio watumishi tena ni watumwa wa umma, hii si nchi ya amani tunaishi kwa dhuluma hapo aliuponda mfumo wote wa Magufuli ambapo watumishi walianza kuogopa kila raia wakawa wanafanyakazi kinoma akaendelea _ukiwa mnyonge hauwezi ukala na kushiba wenye nguvu za ufisadi wanakula za kuiba ripoti ya CAG imekubali hii verse alafu ndio akaanza mambo ya Baba uliye juu (Nyerere) we ndo baba wa taifa, huyu baba uliyetupa (Magufuli) hana lolote ni sifa alivyo chizi akaendelea Nitawashinda Mahakamani nitawakabili Mitaani hapa akawagusa wasiojulikana alafu akaanza kuuliza niseme nisisemee? alafu ghafla akabadilisha mada

Ukimsikiliza vizuri kwa kile kipindi jamaa alifanya jambo gumu sana akiwa live redioni
Nani aliimba hivi....??
 
Jamaa ameupiga mwingi Sana kudadeki!

Amenikumbusha kuhusu king Kaka aliyetoa diss Track moja matata sama kwa serikali ya Kenya,wimbo ukapigwa pini naye akataitishwa.
 
Roma _Mkatoliki kukimbia NCHI yako na kukubali kuwa foreigner pia huo ni "UANDAZI".

Kukimbia familia yako na Kwenda Marekani kuosha vyombo pia huo ni "UANDAZI" dogo!

Tuendelee kukosoana kwa hekima ndugu zangu! Huu ni uchambuzi wangu kuhusu wimbo wa Roma_Mkatoliki!
 
Roma _Mkatoliki kukimbia NCHI yako na kukubali kuwa foreigner pia huo ni "UANDAZI".

Kukimbia familia yako na Kwenda Marekani kuosha vyombo pia huo ni "UANDAZI" dogo!

Tuendelee kukosoana kwa hekima ndugu zangu!Huu ni uchambuzi wangu kuhusu wimbo wa Roma_Mkatoliki!

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Wewe ambaye hujakimbia nchi una nini zaidi ya kutegemea hao hao waosha vyombo wawatumie fedha. Hadi serikali inawazimikia kwa kujidai kuwa mwaka huu wameingiza dola bilioni moja na ushei wakati mnawafanyia mtima nyongo na kuwaonea wivu.

Kama ni rahisi mwanangu jaribu uone kama utatoboa. Siyo nyie msemao kuwa ni heri kuzaliwa paka ulaya kuliko binadamu bongo tokana na ujinga na uvivu?
 
Roma kaanza kukosoa tangu wewe ukiwa huko kwenu maporini.
Umesahau wimbo wake wa Mathematics?
Roma sio chawa kama hawa wengine wanalamba midomo.
 
Wewe ambaye. hujakimbia nchi una nini zaidi ya kutegemea hao hao waosha vyombo wawatumie fedha. Hadi serikali inawazimikia kwa kujidai kuwa mwaka huu wameingiza dola bilioni moja na ushei wakati mnawafanyia mtima nyongo na kuwaonea wivu. Kama ni rahisi mwanangu jaribu uone kama utatoboa. Siyo nyie msemao kuwa ni heri kuzaliwa paka ulaya kuliko binadamu bongo tokana na ujinga na uvivu?
Roma kukimbia nchi niumaandazi
 
Kama umepata wasaa wa kuusikiliza wimbo Roma mkatoliki nipeni Maua yangu..Apo kwenye verse alioimba ngolo kante anampa mbappe krosi anafunga Pogba alikuua anamaanisha nn???
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] chezea football weyeeee.
 
Back
Top Bottom