Nimetoka Leo kwenye interview ya Anwani za makazi nitashare maswali kadhaa ninayokumbuka hapa yawasaidie wale ambao Bado hawajafanya usaili
1, Anwani za makazi na postikod ni nini?
2,Taja faida 5 za mfumo huu wa Anwani za makazi
3, kwanini mfumo wa Anwani za makazi unaonekana kuwa Bora kuliko mfumo wa posta ambao umeonekana kuleta usunbufu?
4, Ni lini Rais ameagiza zoezi hili la ukusanyaji Taarifa za ANWANI ZA MAKAZI kuwa limekamilika!?
5, Dunia Ina pande kuu nne lakn unaweza kuziweka na kueleza zifike nane au kumi na sita....chora dira ya pande nane za Duniani na kuziainisha.
6,taja aina 3 za Anwani zinazotumika ulimwenguni.
7, Mambo matatu ya KUZINGATIA unapoenda kukusanya Taarifa za ANWANI ZA MAKAZI na postikod.
8. Unaishi tarafa gani, halmashauri gani,Kata gani.
Taja jina la afisa tarafa wako,jina la Diwani wako,mtendaji WA kata,mtendaji WA mtaa.
Wakuu haya hapa ndio kadhaa nayakumbuka kwenye paper la interview leo... fanyien Kazi