Mkuu
Kunguru wa Manzese em fanya kutuwekea maswali yalioulizwa kwenye interview iwe faida kwa wengine watakao itwa kwenye hyo interview, bila shaka maswali yanaweza kuendana kwa vile ni kazi za aina moja!
Haya mambo naelewa umuhimu wake kiongozi kama uzi ulivyosema basi system yetu ya interview nilieleza huko juu uki scroll post zilizopita unaweza ona
Ngoja nirudie tena kiongozi
Cha kwanza sisi hatukuwa written interview
Sisi ulikuwa unaingia ndani na simu yako hakikisha ni yako iko full charge
Cheti original cha form 4 na Cha kuzaliwa basi hakuna ziada
Ukifika ndani wanakuuliza miaka yako japo cheti cha kuzaliwa ushawapa so unaweza jiuliza si wanaweza angalia hapo
Elimu yako au umeishia level gani na unafanya nini kwa sasa yaani kinachokuingizia income maswali wanaweza kuuliza kwa kingereza au kiswahili depend na mood yao [emoji3]
Wanawakuwa watu wawili. Mmoja anakuuliza hayo maswali mwengine anakwambia umpatie simu yako
Kwenye simu kwanza wataangalia kama email inaendana na ile iliyoandikwa
Na wataangalia na android version ya simu yako vengine sijui maana anaikagua simu kwa mda kidogo na huwezi ona la kwa ujanja
Baada ya hapo unapewa simu yako unaambiwa ondoka