Nipo njiapanda kwenye ndoa yangu mpya. Naomba mnishauri mliooa 🤔

Kaa kitalamu hapo
 
Kuna masuala ya kumshirikisha mwanamke na kuna mambo ya kufanya mwanaume kama mwanaume, ulichokifanya ni upumbavu wa kuendekeza kichwa cha chini,acha ikutafune meeee wewe anyways laki mbili sio nyingi sana fanya kama umenunua simu halafu imeibiwa
 
Kaka, hapa uko kwenye uamuzi mgumu sana, na inabidi utumie akili kuliko hisia. Huyu ni mkeo, lakini pia anapigania usalama wa mtoto wake, jambo ambalo ni la kawaida kwa mzazi. Tatizo ni kwamba kama kiwanja kitaandikwa kwa jina la mtoto wake pekee, wewe unajitoa kabisa kwenye umiliki, na hapo kuna hatari ukija kupata changamoto za ndoa au msimamo wake kubadilika.


Mambo ya kuzingatia:


  1. Mchango wako kwenye manunuzi – Umechangia pesa zako, kwa hiyo ni haki yako kuwa na umiliki.
  2. Suluhisho la haki – Badala ya kuandika kwa jina la mtoto, andikeni kwa majina yenu nyote wawili (wewe na mkeo). Hii inahakikisha kiwanja ni mali ya familia, si ya mtu mmoja.
  3. Sheria za urithi – Ikiwa nia yake ni kumhakikishia mtoto usalama, basi mnaweza kuandika wosia badala ya kumpa umiliki wa moja kwa moja sasa.
  4. Uaminifu – Kama anasisitiza sana kiandikwe kwa jina la mtoto wake pekee, jiulize kwanini haoni wewe kama sehemu ya hii mali? Kuna kitu anawaza ambacho hujui?
  5. Ongea naye kwa hekima – Usianze ugomvi, bali eleza wasiwasi wako kwa utulivu na uelewe mantiki yake. Kama ana mapenzi ya dhati, atakuelewa na kupata njia ya kati.

Mwisho: Usiingie kwenye mtego wa kutoa mali bila uhakika wa usalama wako wa baadaye. Kama upendo upo, basi maamuzi yafanywe kwa haki kwa wote.
 
Kuna masuala ya kumshirikisha mwanamke na kuna mambo ya kufanya mwanaume kama mwanaume, ulichokifanya ni upumbavu wa kuendekeza kichwa cha chini,acha ikutafune meeee wewe anyways laki mbili sio nyingi sana fanya kama umenunua simu halafu imeibiwa
Laki mbili ndogo?
 
Asante kaka jini nimekuelewa.vizuri
 
Tafuta kiwanja chako kingine, hicho siyo chako. Kama yeye kaweka 7 na ww umeweka 2, hapo umemsaidia tu kiroho safi mwache dogo awe na urithi wake. Mengine jiongeze.
 
Umenikumbusha hesabu za "ratio" yaani inakuwa hivi; M:K=2:7
Leo ndio nimejua matumizi ya zile hesabu.
Nani kakuambia uño kama nyigu au kalio kama gunia ndio ndoa? Beauty it's not enough.
 
Kuonyesha aibu kwa yeye kuchangia pesa kiduchu mpaka ameamua atumie lugha ya kifasihi
YEYE AKAWEKA BOKSI SABA MI NIKAWEKA BOKSI MBILI...
 
usituone mafala umetoa laki saba na yeye katoa laki mbili acha kugeuza stori kama ingekua umetoa laki mbili ww basi hata usingewaza ila unashangaa kwakua umetoa hela nyingi alafu anataka kumuandika mwanae mzee punguza ujinga wakati unatoa hiyo laki 7 hukutushirikisha saa hizi umezidiwa akili na dem unakuja kulialia utawekewa dyudyu mikindani
 
Yaani mwanaume umetoa laki mbili unataka jina lako liandikwe kwenye hati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…