Nipo njiapanda kwenye ndoa yangu mpya. Naomba mnishauri mliooa 🤔

Mwanaume mzima na midevu unalilia uwanja uliochangia laki 2?
Kwanini usingenunua kwa hela yako?
 
Usikute hata hiyo laki 7 aliyotoa hiyo single mama amepewa na mzazi mwenzake ili amnunulie mtoto wao kiwanja wewe umekaakaa kizembe tu.

Hivi ulikosa kabisa mke wa kuoa hadi ujitumbukize kwenye matatizo yasiyo na ulazima?
 
Kmmk huo mkeka unaenda kuchanika vibaya mno pamoja na handcup yako. Simama kama mwanaume kama hawezi kukubali kuandika jina lako wewe mwanaume basi hapo huna chako
 
Mkuu wala usiseme kitu piga kimya aandike jina la mtoto wake.... laki mbili sio kesi

Chakufanya fanya juu chini upate hela ununue kiwanja kingine kimya kimya andika jina lako...... Hakikisha hichi ndio utajenga nyumba

Next time kama baba wa familia hakikisha mambo makubwa kama hayo wewe ndio unayaanzisha na mke unampa taarifa tu

Changamoto ni kama mkeo kakuzidi sana kipato kiasi kwamba unahitaji sapoti yake kwa kiasi kikubwa mambo yaende..... kwa mentality zake hizo jipange sana mkuu anachungulia mbali sana huyu kwamba siku mkishindwana uondoke na nguo zako tu

Mi wife alinunua kiwanja kupitia viwanja vya ofa kazini kwao akaandika jina lake sikuongea kitu
Nilichofanya nilitafuta kiwanja kimya kimya kisha nikamtaarifu nimepata kiwanja na baada ya hapo nikaanza ujenzi mara moja
Basi nguvu zetu zote tukahamishia kwenye ujenzi
 
Asante kwa ushaurini

Je wife wako pia alikuwa msimbe?
 

Kama umetoa Box 2 means yeye ametoa zaidi ya 75% kwa maana hiyo yeye ndiyo mwenye final say ,muache amuandikishe JANJARO.

============
Ukitaka chai tumia TATEPA.
 
Milioni 2 mkashushana hadi laki 9?na dalali akakubali...inamaana hapa bado dalali inamlipa.
Kiwanja kitunda mwanagati kwa laki 9?sio mwanagati ninayoijua mimi.
 
Ndio nachowaza yule fala ikitokea tumezinguana anaweza kukaribishwa ndio akawa mwenye nyumba😁
 
Asante boss apo tayari nina alert kichwani 😁
 
Aandike tu jina la mtoto wake. Kwani si ushampenda bwana, si mke wako? Kwanza hapo kiwanja ni kama tu ni cha kwake, ye anatoa laki saba we unatoa laki mbili kama kumsapoti tu. Yaani kiufupi ye anatoa aslimia 78% we umetoa laki mbili ambayo hata smartphone hainunui, na bado unakuja huku kuomba ushauri, una akili kweli.?? Bado una upumbavu kichwani wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…