Nipo tayari kutoa milioni 5 kwa mtu atakayenionyesha hili andiko

Nipo tayari kutoa milioni 5 kwa mtu atakayenionyesha hili andiko

Wewe unaandiko la wao kubatizwa KWA majina ya kina nani?

Pia inamaanisha walimgomea Yesu kubatizwa KWA AGIZO hilo au ?
Matendo ya Mitume 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Baada ya Yesu Kristo kuwapa wanafunzi wake maagizo ya kuwabatiza watu kwa jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu aliwaambia wasifanye jambo lolote mpaka huyo roho ayakayewafunulia namna ya kufanya. Ndipo roho alipowashukia hawakuendelea na kuwabatiza watu kwa jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu kwasababu hayo siyo majina bali ni vyeo tuu. Mtu mwenye mtoto anaitwa Baba, kwenye familia yenu wewe ni Mwana, vivyo hivyo kwenye Roho, hakuna jina linaitwa roho.
 
Mwenyewe katangaza dau la mil 5. humu ndani watu wanashuka tu na maandiko, sasa sijui kama mtoa mada anazo hizo mil 5 za kugawa burebure hivi... Bando ni shida
Hela ipo mkuu..sijapata bado mtu aliyejibu kwa usahihi
 
Kwa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu = Katika Jina la Yesu...!

Chagua tu kile mdomo wako utakua rahisi kutamka
Kwahiyo mitume wakaona wachague kwa jina la Yesu nawakati boss wao aliwaambia kwa jina la Baba, Mwana na Roho. Asante kwa kushiriki mkuu
 
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.

Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Weka 5milion kwenye escrow account nikupe scripture nikianza Yesu pale Jordan halafu nikimalizia na alieagiza watu wabatizwe
 
Ninahisi Mtoa mada anafuata mafundisho ya “Jesus Only” au "Oneness Pentecostals", ambao wanaamini kwamba ubatizo unapaswa kufanywa kwa jina la Yesu tu. Sababu kuu wanayoitoa ni kwamba katika Biblia hatusomi popote kuhusu mtu au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Ni kweli hakuna andiko linaloonyesha kwamba mitume walibatiza kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Lakini je, mitume walikuwa wakamilifu kiasi kwamba tufuate kila walichofanya? La hasha. Mitume, walikuwa wanadamu walioweza kukosea. Hivyo sio kila walilofanya ni mfano wa kuigwa.

Angalia hapa baadhi ya makosa yaliyofanywa na mitume:

Petro alijitenga na Mataifa waliomwamini Kristo - Paulo akamkemea vikali kuwa ni mnafiki (Wagalatia 2:11–14).

Kumbuka tena Petro alitaka Yesu asife msalabani. Yesu alisema lazima afe, Petro akamkataza. Yesu akamkemea: “Rudi nyuma yangu, Shetani...” (Mathayo 16:22–23).

Yakobo na Yohana walitaka kushusha moto juu ya Wasamaria. Yesu akawakemea kwa kuwaambia: “Hamtambui ni roho ya namna gani mliyo nayo” (Luka 9:54–55).

Mitume walipigania vyeo badala ya utumishi. Waliulizana ni nani mkubwa kuliko wote. Yesu akawafundisha kuwa mkuu ni yule anayehudumu (Luka 22:24–26).

Tomaso alikataa kuamini kwamba Yesu amefufuka mpaka aone kwa macho. Alisema: “Nisipoona zile alama za misumari mikononi mwake, na kuweka kidole changu kwenye hizo alama za misumari, na mkono wangu ubavuni mwake, sitaamini.” (Yohana 20:25). Yesu alimkemea: “...usiwe asiyeamini, bali aaminiye” (Yohana 20:27).

Yuda Iskariote ingawa alikuwa miongoni mwa mitume 12, alitenda kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu kwa kumsaliti Yesu.

Mitume walikosea kuhusu huduma kwa Mataifa mwanzoni, hadi baadaye Petro alipopewa ufunuo (Matendo 10).

Hata mtume Paulo, tunayesoma kuwa alijaa ufunuo mkuu, alifanya makosa ya kibinadamu. Mojawapo ya makosa aliyoyafanya ni kugombana vikali na Barnaba hadi wakatengana!(Matendo 15:36–40).

Kwa mifano hiyo, msisitizo sio kuiga walichofanya mitume, bali agizo la Yesu mwenyewe. Yesu alisema:

“Kwanini mnaniita Bwana, Bwana, lakini hamtendi ninayowaambia?”(Luka 6:46). Mojawapo ya mambo aliyotuambia Yesu tufanye ni hili lihusulo ubatizo:

“Mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.”(Mathayo 28:19).

Hilo ni agizo la moja kwa moja kutoka kwa Yesu mwenyewe kabla ya kupaa mbinguni. Linapaswa kutekelezwa kwa utiifu, bila kupunguzwa wala kubadilishwa, hata kama mitume hawakufanya hivyo.

Yesu Kristo ni Mungu. Na ndiye Bwana na Mwokozi wetu. Hivyo agizo lake ndilo linalobeba uzito wa mwisho. Kwahiyo ubatizo wa kweli ni ule unaotii agizo la Yesu.

Soma uzi huu upate mafundisho ya kina zaidi kuhusu ubatizo wa kweli.

cc: patrickk
Kama haukubaliani na mitume. Nenda kwenye biblia yako unayoiamini, ondoa vitabu vyote vilivyoandikwa na mitume ubakiwe na Yesu tuu mkuu. Siwezi kujibu maelezo yako uliyomezeshwa mkuu
 
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.

Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Luka 20:4-7, 4 Ubatizo wa Yohana, je! Ulitoka mbinguni au kwa wanadamu? 5 Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema ulitoka mbinguni, atasema, Basi, mbona hamkumwamini? 6 Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii.
 
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.

Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Huku ni kuchanganyikiwa hizo Milion tano unazoahidi katoe sadaka kwa Wanawake wajane na Yatima. Sio Kuja kutuletea ushamba wako humu.
Fu******** off 👹
 
Huku ni kuchanganyikiwa hizo Milion tano unazoahidi katoe sadaka kwa Wanawake wajane na Yatima. Sio Kuja kutuletea ushamba wako humu.
Fu******** off 👹
Hata Yuda alipoona Mwanamke kahaba akimpaka Yesu mafuta ya gharama alikuja na hoja kama yako mkuu..Rudi nyuma ee shetani
 
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.

Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Tatizo lako unachukulia Biblia kama hadithi. Biblia ni kitabu kilichoandikwa ktk level ya juu sana. Huwezi kuelewa baadhi ya mistari hadi Roho Mtakatifu akuongoze. Mathalan Yesu alipowaelekeza wanafunzi wake wakabatize katika Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu "Mathayo 28:19", Na Patro alipohubiri akawaambia watubu na kubatizwa katika jina la Yesu Kristo "Matendo 2:38". Mistari hiyo haigongani. Ngoja nikufafanulie:
Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu sio jina bali ni nafasi. Mungu ana nafasi tatu (Baba, Mwana na Roho Mtakatifu). Kwa hiyo maelekezo ya Yesu ni kubatiza katika Jina la Mungu yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa jina la Mungu ni lipi? Mungu ana majina mengi yaliyofunuliwa ktk Agano la Kale. Lakini ktk Agano jipya wanadamu wamepewa jina moja tu nalo ni
Jina la YESU KRISTO. Soma Wafilipi 2: 5-11 na Matendo 4:12. Hakuna jina lingine tulilopewa ni Yesu Kristo ndilo jina la Mungu. Ndio maana sisi Wakristo tunakiri ya kwamba YESU NI MUNGU. Ukibisha shauri yako utakuja kujikuta Jehanamu!
 
Nionyeshe katika biblia yako unayosoma ni kifungu gani kimesema Mungu ana nafsi tatu
 
Hata Yuda alipoona Mwanamke kahaba akimpaka Yesu mafuta ya gharama alikuja na hoja kama yako mkuu..Rudi nyuma ee shetani
Toa Upumbavu wako basi Mkuu 🤣
Kama una hiyo hela ichangie hata Jamiiforums ili iendelee kuwa hewani.

Yaani haya matatizo ya akili ni janga hasa miaka 10 ijayo
 
Je, Baba ni jina?
Je, Mwana ni jina?
Je, Roho Mtakatifu ni jina?

Hapana, hivyo vyote ni uhusika, ni cheo kinachobebwa na Fulani,

sasa huyo Baba jina lake ni nani?
Jibu - Yesu.

Huyo Mwana jina lake ni nani?
Jibu - Yesu.

Huyo Roho Mtakatifu jina lake ni nani?
Jibu - Yesu.
 
Back
Top Bottom