Huwezi kujibu kwa sababu ni ukweli usiopingika. Mitume hawana ubavu wa kubadili agizo la aliyewatuma.
Yohana 13:16
Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyemtuma.
Kama hukubaliani na agizo la Yesu, nenda kwenye biblia yako unayoiamini, ondoa Maandiko yote aliyonena Yesu ubakiwe na ya mitume tuu, mkuu, halafu subiri siku ya mwisho uone kama Yesu hatakuambia maneno haya:
Lk 13:27
Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.