Nipo tayari kutoa milioni 5 kwa mtu atakayenionyesha hili andiko

Nipo tayari kutoa milioni 5 kwa mtu atakayenionyesha hili andiko

Sasa mkuu kwa maelezo haya huoni kwamba biblia inatambua ubatizo kwa jina la Yesu Kristo na sio kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?
Inaonekana bado hujaelewa kama unatafuta kweli basi mimi nitakuambia yaliyo kweli sikiliza.

Biblia haija andika kila kitu au kila tukio kama vile ulivyo uliza, bali biblia imefupishwa sana hata maisha ya yesu na matukio yaliyofanywa tangu anazaliwa hadi anapaa mbinguni na kuwaambia nendeni mkawafanye mataifa kuwa wnafunzi wangu mkawabatize kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu bado tunaona kuna ufupisho mkubwa sana wa matukio.

Kwahiyo biblia haija andika kila tukio ? jibu ni ndio kila kitu kinge andikwa biblia isingetosha.

Lakini hiki kipande cha yesu kuwatuma mitume wakabatize kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu ni kama kipande kamili au kielelezo cha vipande vingine vilivyo fupishwa mfano umesema niliona mitume wesema walibatiza kwa jina la yesu, hatuwezi kuchukulia hili neno kama lina makosa. kwanini ?

Yesu ni mwana na yeye na baba na roho ni kitu kimoja kwahiyo ni kama fupisho hivyo sio kitu kipya hicho, lakini kielelezo kinasema yesu aliwaambia mkawabatize kwa jina la baba na la mwana na roho mtakatifu, ni vizuri kuelewa kuwa biblia imefupishwa haija andika kila kitu kila tukio au matukio ya ubatizo wa mitume n.k

Likini tutakapo rejea maneno ya flani alibatizwa kwa jina la yesu bali tuelewwe kuwa alibatizwa kwa maagizo ya yesu yale aliyosema na yametajwa kwa uwazi kabisa "mkawabatize kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu" hivyo nadhani hoja nyengine hazina msingi hapo.
 
Wewe ndie unaekalili na kuaminishwa isivyo mkuu. Nionyeshe andiko katika biblia linalounga mkono hoja yako.

Mimi naanza na hili
Marko 16:16-18
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Hilo jina la yesu ndio huyo huyo mungu wa sika wa yakobo na Ibrahim vyote ni vitu sawa hivyo hakuna hoja hapo unayotaka nikisema nimeamini kwa mungu wa mbinguni tayari nishamtaja huyo yesu.
 
Kubatizwa kwa Jina la Yesu maana yake ni kubatizwa kama Yesu alivyoagiza SIO kubatizwa kwa Jina moja la Yesu.
Hapana, nafikiri hapa unajizuia kuukubali ukweli, na kukataa moja kwa moja kazi ya Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani ya mitume.
 
Nina mashaka na imani yako
Mimi naweza kutoa pepo kwa jina la baba na mwana na roho kinacho angaliwa ni imani sio jina, ndio maana kuna watu wanaweza kutumia jina la yesu na pepo lisiondoke pia usikalili msingi ni imani, mungu ni mwelewa sana anasikia na atatenda kutokana na imani yako hata ukitumia mungu wa Ibrahim wa usaka na yakabo pepo litakimbia.
Mathayo 7:22
[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

Luka 10:17
[17]Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.

Matendo ya Mitume 16:18
[18]Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

Matendo ya Mitume 19:13,15
[13]Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.

[15]Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
 
Matendo ya Mitume 2:38
[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Then Peter said unto them, Repent, and be baptized every one of you in the name of Jesus Christ for the remission of sins, and ye shall receive the gift of the Holy Ghost.
 
Matendo ya Mitume 8:16-17
[16]kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
()
[17]Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
 
Matendo ya Mitume 10:48
[48]Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.
 
Wapo watu waliorudia kubatizwa baada ya kuwa hawakubatizwa kwa jina la Bwana yesu kristo na kama umedanganywa kuwa umebatizwa kwa jina nje ya Bwana yesu kristo jua hukuwahi kubatizwa.

Na ukristo wako ni bure.
Mtu asipozaliwa kwa maji na roho hatakusikia tu ufalme wa mungu hatausikia
 
Habari Wakuu.

Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.

Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.

Akili ndogo kutaka kuongoza akili kubwa😂😂😂😍
 
Ukisoma Mathayo 28:19 yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakawabatize watu hivyo baada ya yeye kuondoka.
 
Ukisoma Mathayo 28:19 yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakawabatize watu hivyo baada ya yeye kuondoka.
Ni kweli kabisa, baada ya Yesu kuondoka ni watu gani ulio waona au kuwasoma kwenye biblia waliobatizwa kwa ubatizo huo wa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?
 
Mathayo 28;19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
 
Mtoto anapozaliwa akamwagiwa maji ya mto,ikanenwa nakutenganisha na shetani Kwa maji haya,kazi kwisha,zingine mbwe mbwe tu,siri ipo ndani ya maji,na neno litamkwalo!
 
Wapi katika Biblia tunaweza kuona wanafunzi au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19?

Sasa tuchambue kwa ushahidi wa maandiko:

1. Amri ya Yesu mwenyewe – Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.”

Hapa Yesu mwenyewe anatoa agizo kwa mitume wake kabla ya kupaa mbinguni. Hii ndiyo amri kuu ya ubatizo, na inatajwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

2. Utekelezaji wa agizo – Matendo ya Mitume
Watu wengi walibatizwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini kwa jina la Yesu Kristo:
a) Matendo 2:38 – Siku ya Pentekoste
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo…”

b) Matendo 8:16– Watu wa Samaria
“…kwa maana alikuwa hajamshukia hata mmoja wao ila walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.”

c) Matendo 10:48 – Kornelio na watu wake

“Akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo.”

d) Matendo 19:5– Wanafunzi wa Yohana
“Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”

Hoja ya Kulinganisha:

Ingawaje agizo lilikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utekelezaji wake katika matendo ya mitume wote waliobatiza walitumia jina la Yesu Kristo. Hii imeibua mijadala ya kiteolojia juu ya kama “jina” hilo linawakilisha utimilifu wa Baba (Mungu), Mwana (Yesu), na Roho Mtakatifu ndani ya utambulisho wa Yesu Kristo.

Mwisho kwa Ushahidi:
  • Hakuna maandiko katika Biblia yanayoeleza moja kwa moja kwamba mtu alibatizwa kwa kutajwa maneno “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” wakati wa tendo la ubatizo.
  • Hata hivyo, maandiko yako wazi kwamba agizo lilitolewa na Yesu mwenyewe kwa maneno hayo (Mathayo 28:19), lakini mitume walibatiza kwa jina la Yesu Kristo, wakiamini kuwa ndilo jina lililobeba mamlaka ya Utatu mtakatifu.
Ushauri wa Kiutafiti:
Tafsiri ya “jina” katika Mathayo 28:19 kama “Yesu” inatokana na fundisho la kuwa Yesu ndiye utimilifu wa Mungu katika mwili (Kol 2:9). Ndiyo maana ubatizo kwa jina la Yesu Kristo unaonekana kuwa ni utekelezaji wa ile amri ya Mathayo 28:19.

Niwekee mil 5 sasa na Ubarikiwe !
Je unaona tofauti gani ya kusema kwa Jina la Yesu na kwa jina la baba , Mwana na Roho Mtakatifu
Au ni hicho hicho kimoja?
 
Mathayo 28;19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Baba sio jina walamwana sio jina wala roho mtakatifu.
Mimi ni baba mimi ni mwana mm ni mjukuu.

Mungu akiwa yehovaa
Alipokuja ulimwenguni huyo huyo yehova akawa mwana. Emmanuel.

Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Anapoondoka nakurudi kama roho huyo huyo yehova anakuwa roho mtakatifu.

Izo ni ofisi za Mungu mmoja ambae ananafsi moja tuu.
Isaya 45:15
[15]Hakika wewe u Mungu ujifichaye nafsi yako, Ee Mungu wa Israeli, Mwokozi.

Na hii ndio sababu ukristo wakimadhehebu umeshindwa kuwashawishi wayahudi.
Kwa fundisho la kumgawa Mungu.

Isaya 9:6
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani.

Yesu ndie yule Mungu BABA.
 
⚠️ ChatGPT Detected
Wapi katika Biblia tunaweza kuona wanafunzi au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19?

Sasa tuchambue kwa ushahidi wa maandiko:

1. Amri ya Yesu mwenyewe – Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.”

Hapa Yesu mwenyewe anatoa agizo kwa mitume wake kabla ya kupaa mbinguni. Hii ndiyo amri kuu ya ubatizo, na inatajwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

2. Utekelezaji wa agizo – Matendo ya Mitume
Watu wengi walibatizwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini kwa jina la Yesu Kristo:
a) Matendo 2:38 – Siku ya Pentekoste
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo…”

b) Matendo 8:16– Watu wa Samaria
“…kwa maana alikuwa hajamshukia hata mmoja wao ila walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.”

c) Matendo 10:48 – Kornelio na watu wake

“Akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo.”

d) Matendo 19:5– Wanafunzi wa Yohana
“Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”

Hoja ya Kulinganisha:

Ingawaje agizo lilikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utekelezaji wake katika matendo ya mitume wote waliobatiza walitumia jina la Yesu Kristo. Hii imeibua mijadala ya kiteolojia juu ya kama “jina” hilo linawakilisha utimilifu wa Baba (Mungu), Mwana (Yesu), na Roho Mtakatifu ndani ya utambulisho wa Yesu Kristo.

Mwisho kwa Ushahidi:
  • Hakuna maandiko katika Biblia yanayoeleza moja kwa moja kwamba mtu alibatizwa kwa kutajwa maneno “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” wakati wa tendo la ubatizo.
  • Hata hivyo, maandiko yako wazi kwamba agizo lilitolewa na Yesu mwenyewe kwa maneno hayo (Mathayo 28:19), lakini mitume walibatiza kwa jina la Yesu Kristo, wakiamini kuwa ndilo jina lililobeba mamlaka ya Utatu mtakatifu.
Ushauri wa Kiutafiti:
Tafsiri ya “jina” katika Mathayo 28:19 kama “Yesu” inatokana na fundisho la kuwa Yesu ndiye utimilifu wa Mungu katika mwili (Kol 2:9). Ndiyo maana ubatizo kwa jina la Yesu Kristo unaonekana kuwa ni utekelezaji wa ile amri ya Mathayo 28:19.

Niwekee mil 5 sasa na Ubarikiwe !
 
Mtoto anapozaliwa akamwagiwa maji ya mto,ikanenwa nakutenganisha na shetani Kwa maji haya,kazi kwisha,zingine mbwe mbwe tu,siri ipo ndani ya maji,na neno litamkwalo!
Siri ni maana ya ubatizo .
Watu hawajui kwanini wanabatizwa.

Ubatizo unawakilisha kufa na kufuuka kwa yesu kristo.
Ishara ya kuamini.
Warumi 6:4
[4]Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Baptize ni immerse. Kuzamisha.
Na unapoinuliwa majin ni kufufuka kwa yesu kristo.
Huwez zama kwenye bakuli, ama uzikwe kwa kunyunyiziwa udongo
 
Baba sio jina walamwana sio jina wala roho mtakatifu.
Mimi ni baba mimi ni mwana mm ni mjukuu.

Mungu akiwa yehovaa
Alipokuja ulimwenguni huyo huyo yehova akawa mwana. Emmanuel.

Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

Anapoondoka nakurudi kama roho huyo huyo yehova anakuwa roho mtakatifu.

Izo ni ofisi za Mungu mmoja ambae ananafsi moja tuu.
Isaya 45:15
[15]Hakika wewe u Mungu ujifichaye nafsi yako, Ee Mungu wa Israeli, Mwokozi.

Na hii ndio sababu ukristo wakimadhehebu umeshindwa kuwashawishi wayahudi.
Kwa fundisho la kumgawa Mungu.

Isaya 9:6
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani.

Yesu ndie yule Mungu BABA.
Kweli anajigawa
 
Back
Top Bottom