Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 33,952
- 56,156
Mtoa mada hana helaVipi kakupa 5M yako
Mtoa mada hana helaVipi kakupa 5M yako
Mkuu umejibu vyema, me nakupa mfano mdogo tuu.Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu
Kabla ya Yesu watu walibatizwa kwa jina gani?Mkuu umejibu vyema, me nakupa mfano mdogo tuu.
Tuna Rais ambaye ndie kiongozi wa nchi, Huyo huyo ni amiri Jeshi mkuu. Huyo huyo ni mwenyekiti wa chama tawala.
Sasa Rais ni jina? Ni cheo
Amiri jeshi ni jina? Ni cheo
Mwenyekiti wa chama ni jina? Ni cheo
Unaposema kwa jina la Baba, Baba sio jina ni cheo. Mwana sio jina ni cheo, Roho Mtakatifu sio jina ni cheo, Jina ni moja tu nalo ni Jina la YESU KRISTO.
Usiwe na wasiwasi kwamba itakuwaje Sasa,unaweza rudia tena kubatizwa na hakikisha unabatizwa kwa jina la Yesu Kristo. Soma Matendo ya Mitume 19:1-7 utapata kitu.
Nashukuru mkuu, hatulumbani bali tunaelekezana. Tunaweza kupata andiko linalosema mtu akibatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu na aliyebatizwa kwa jina la Yesu Kristo ni sawa. Mimi kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba kipindi Yesu yupo hapa duniani Kuna mambo alikua akiwafunulia wanafunzi wake lakini walikua haelewi na ndio maana baada ya makutano kutawanyika, walikua wakimuendea jioni au usiku kumuuliza juu ya Yale aliyokuwa akiyaongea katika makutano. Alipoondoka duniani aliwaahidi kuto waacha Yatima akiwatumia Roho Mtakatifu ili awafunulie Yale aliyokuwa amewaagiza kufanya. Na ndio maana utaona Yesu aliwaagiza wakahubiri ulimwengu kwote wakiwabatiza watu kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu lakini waliposhukiwa na Roho Mtakatifu aliwafunulia kwamba ubatizo ni kwa jina la Yesu Kristo.Hakuna haja ya kulumbana.
Kwa jina la baba, mwana na Roho Mtakatifu= Jesus.
Msifanye mambo kuwa magumu.
Yesu aliwaagiza wakabatize kwa jina la baba mwana na Roho Mtakatifu ila mitume wakampa heshima yote wakijua yeye ndiye Mungu mwenyewe mkuu.
Anayebatiza kwa jina la baba mwana na Roho Mtakatifu hafanyi dhambi ila anayebatiza kwa jina la Yesu huyo amepata ufahamu zaidi na kumtambua Mungu.
Ubatizo wa Yohana Mbatizaji. Kabla ya Yesu walikua wakitimiza sheria na torati kama ilivyokuwa tangu kipindi cha Musa. Hapakuwa na jinaKabla ya Yesu watu walibatizwa kwa jina gani?
Wewe wasemaMtoa mada hana hela
Umemjibu vyema sana kwa kuongezea kutoka kwenye neno la msingi la agizo la yesu pale mathayo 28:19Wapi katika Biblia tunaweza kuona wanafunzi au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19?
Sasa tuchambue kwa ushahidi wa maandiko:
1. Amri ya Yesu mwenyewe – Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.”
Hapa Yesu mwenyewe anatoa agizo kwa mitume wake kabla ya kupaa mbinguni. Hii ndiyo amri kuu ya ubatizo, na inatajwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
2. Utekelezaji wa agizo – Matendo ya Mitume
Watu wengi walibatizwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini kwa jina la Yesu Kristo:
a) Matendo 2:38 – Siku ya Pentekoste
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo…”
b) Matendo 8:16– Watu wa Samaria
“…kwa maana alikuwa hajamshukia hata mmoja wao ila walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.”
c) Matendo 10:48 – Kornelio na watu wake
“Akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo.”
d) Matendo 19:5– Wanafunzi wa Yohana
“Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”
Hoja ya Kulinganisha:
Ingawaje agizo lilikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utekelezaji wake katika matendo ya mitume wote waliobatiza walitumia jina la Yesu Kristo. Hii imeibua mijadala ya kiteolojia juu ya kama “jina” hilo linawakilisha utimilifu wa Baba (Mungu), Mwana (Yesu), na Roho Mtakatifu ndani ya utambulisho wa Yesu Kristo.
Mwisho kwa Ushahidi:
Ushauri wa Kiutafiti:
- Hakuna maandiko katika Biblia yanayoeleza moja kwa moja kwamba mtu alibatizwa kwa kutajwa maneno “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” wakati wa tendo la ubatizo.
- Hata hivyo, maandiko yako wazi kwamba agizo lilitolewa na Yesu mwenyewe kwa maneno hayo (Mathayo 28:19), lakini mitume walibatiza kwa jina la Yesu Kristo, wakiamini kuwa ndilo jina lililobeba mamlaka ya Utatu mtakatifu.
Tafsiri ya “jina” katika Mathayo 28:19 kama “Yesu” inatokana na fundisho la kuwa Yesu ndiye utimilifu wa Mungu katika mwili (Kol 2:9). Ndiyo maana ubatizo kwa jina la Yesu Kristo unaonekana kuwa ni utekelezaji wa ile amri ya Mathayo 28:19.
Niwekee mil 5 sasa na Ubarikiwe !
Kubatizwa kwa Jina la Yesu maana yake ni kubatizwa kama Yesu alivyoagiza SIO kubatizwa kwa Jina moja la Yesu.Sawa, hebu useme ni kwanini Mtume Petro na wengine wote walibatiza kwa Jina Yesu Kristo?
Watu wanaofundisha kubatizwa kwa Jina la Yesu tu hawaamini pia kuwa Mungu ana nafsi tatu: Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Watu hawa wanadai Utatu ni fundisho la kibinadamu lisilo la kibiblia! Wenye imani hiyo bila shaka ni wavivu wa kusoma Biblia maana mafundisho ya Utatu yako wazi kabisa.Kubatizwa kwa Jina la Yesu maana yake ni kubatizwa kama Yesu alivyoagiza SIO kubatizwa kwa Jina moja la Yesu.
MKuu kama Yesu aliwaagiza wanafunzi wabatize ina maana wanafunzi walitii agizo hilo kama kawaida. Mathayo 28:18Habari Wakuu.
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.
Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Nashukuru mkuu, sio kwamba wanafunzi hawakutii agizo la kubatiza, ila walibatiza kwa Jina na wala sio majina..nauliza tuu jina la Baba ni lipi? Jina la Mwana ni lipi? Na Jina la Roho Mtakatifu ni lipi?MKuu kama Yesu aliwaagiza wanafunzi wabatize ina maana wanafunzi walitii agizo hilo kama kawaida. Mathayo 28:18
Jaribu kutoka kwenye box. Hizo m5 baki nazo
Sasa mkuu kwa maelezo haya huoni kwamba biblia inatambua ubatizo kwa jina la Yesu Kristo na sio kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?Hakuna mahali katika Biblia ambapo majina ya wanafunzi au watu fulani yameorodheshwa moja kwa moja kwamba walibatizwa kwa fomula kamili ya “kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu” kama ilivyoandikwa kwenye Mathayo 28:19. Hata hivyo, agizo hili la Yesu ndilo msingi wa ubatizo wa Kikristo, na kanisa la kwanza lilitekeleza agizo hili.
Katika Matendo ya Mitume, watu wengi walibatizwa baada ya kuamini, kama vile wale 3,000 siku ya Pentekoste (Matendo 2:41), lakini maandiko yanasema walibatizwa “kwa jina la Yesu Kristo”. Hii haimaanishi walipuuzia agizo la Mathayo 28:19, bali walikuwa Wayahudi waliomtambua tayari Mungu Baba na Roho Mtakatifu; walihitaji tu kumkiri Yesu kama Masihi.
Kwa hiyo:
• Watu waliobatizwa siku ya Pentekoste (takriban 3,000), na wengine waliotajwa katika Matendo (kama Kornelio, Towashi wa Ethiopia, na wengine), walibatizwa kwa utambuzi wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, ingawa mara nyingi maandiko yanataja “kwa jina la Yesu” kama msisitizo wa imani yao mpya kwa Kristo.
• Hakuna orodha ya majina binafsi ya watu walioandikwa walibatizwa kwa fomula kamili ya Mathayo 28:19, lakini Wakristo wote wapya walifuata agizo hilo la Yesu.
Kwa muhtasari, Biblia haitaji majina ya watu mmoja mmoja waliobatizwa kwa maneno hayo kamili, lakini inathibitisha kwamba kanisa la kwanza lilifuata agizo la Yesu la kubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu
Hakunaababa si jina wala.mwaana wala roho mtakatifu.Habari Wakuu.
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.
Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Baba jina lako ulilonipa nami nawapa.Nashukuru mkuu, sio kwamba wanafunzi hawakutii agizo la kubatiza, ila walibatiza kwa Jina na wala sio majina..nauliza tuu jina la Baba ni lipi? Jina la Mwana ni lipi? Na Jina la Roho Mtakatifu ni lipi?
NB: Hela nitabaki nayo kwasababu hakuna mtu kwenye biblia aliyebatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu wala hakuna kitu ktu kinachoitwa utatu. Mtakatifu
Nimekuelewa sana mkuu. Kama wanaamini katika utatu Mtakatifu, wakemee pepo kwa utatu Mtakatifu.Hakunaababa si jina wala.mwaana wala roho mtakatifu.
Wote walibatizwa kwa jina la yesu kristo.
Peepo tu hatoki kwa jina la baba na mwana na roho.
Lolote mfanyalo kwa neno ama kwatendo fanyeni kwa jina la Bwana yesu kristo
Bado hujapata jibu au hujaelewa niingilie kati sihitaji hiyo hela yako ?Nimekuelewa sana mkuu. Kama wanaamini katika utatu Mtakatifu, wakemee pepo kwa utatu Mtakatifu.
Mimi naweza kutoa pepo kwa jina la baba na mwana na roho kinacho angaliwa ni imani sio jina, ndio maana kuna watu wanaweza kutumia jina la yesu na pepo lisiondoke pia usikalili msingi ni imani, mungu ni mwelewa sana anasikia na atatenda kutokana na imani yako hata ukitumia mungu wa Ibrahim wa usaka na yakabo pepo litakimbia.Hakunaababa si jina wala.mwaana wala roho mtakatifu.
Wote walibatizwa kwa jina la yesu kristo.
Peepo tu hatoki kwa jina la baba na mwana na roho.
Lolote mfanyalo kwa neno ama kwatendo fanyeni kwa jina la Bwana yesu kristo
Wewe ndie unaekalili na kuaminishwa isivyo mkuu. Nionyeshe andiko katika biblia linalounga mkono hoja yako.Mimi naweza kutoa pepo kwa jina la baba na mwana na roho kinacho angaliwa ni imani sio jina, ndio maana kuna watu wanaweza kutumia jina la yesu na pepo lisiondoke pia usikalili msingi ni imani, mungu ni mwelewa sana anasikia na atatenda kutokana na imani yako hata ukitumia mungu wa Ibrahim wa usaka na yakabo pepo litakimbia.