Nisikilizwe nishauriwe ukweli mtupu nisije kujuta maisha yangu yote

Nisikilizwe nishauriwe ukweli mtupu nisije kujuta maisha yangu yote

Yani uolewe na mwanaume ana wanawake wengi, uamue kujua na husijue. Au tuseme hakuzingatia kama ni suala la msingi! Unaassume maisha kwenye future!
Ndo sasahivi kagundua huyo mwanaume ana mke mwingine, alikuwa amemficha.
 
Ni mambo ya kawaida atulie awe mke mwenza tu. Si anapewa kila kitu! Kama anaona hawezi, sivunji ndoa za watu mimi 😂
Mimi sina shida na ukewenza kama mtu karidhia,shida ni pale ambapo yeye hajaridhia. Kama ameridhia aishi tu mbona wengine wanaishi. Tatizo sio kila mwanamke anataka au anamudu mitara, ila anaemudu aende,sheria za nchi zinaruhusu.
 
Habari za muda humu

Nitasema ukweli Kama Kuna hukumu Basi nihukumiwe wote tunakosea Hakuna mkamilifu

Nachoitaji ni ukweli mchungu hata kama utaniuma ni sawa ilimradi nisiharibu maisha yangu maana Naona kama shetani amedhamiria kuniharibia maisha

Nimeshaleta story ya Kijana wangu wa kisukuma humu mkanishauri nikashupataza shingo

Huyu mwanaume tuna miaka 3 sasa tangu 2024 na Nina miezi 7 toka nianze kuishi nae..Tulikutana nikiwa na 24 yeye aliniambia ana 27( alinidanganya now ana 35)

Amenitoa nyumbani kwetu kanipeleka mkoa anaoishi yeye(kanda ya ziwa) ndugu zangu wanajua Niko nafanya kazi kumbe nimewekwa kinyumba na msukuma

Amenifungulia Biashara ninayoiendesha mwenyewe kwani aliniambia nitafute wazo la Biashara yeye ataniwezesha ametimiza inaendelea vizuri na yeye hausiki na chochote kwenye hiyo Biashara na ananihudumia vizuri

Changamoto
Tulikuwa na ugomvi mzito tangu mwezi wa 6 baada ya kugundua ana mke (amemlipia mahari wamezaa watoto wawili kwa msukuma ukishalipiwa mahari ni mke tayari)
Ukweli nimeumia sana maana sikutegemea Kama ningekutana na kitu Kama hiki
Lakini mwenzangu yuko kawaida kabisa Kama Hakuna kilichotokea anasema ni kawaida kwao kuoa mitala nitulie Mimi ndio mke mdogo yule atabaki kwenye nafasi yake Kama mke mkubwa na Hakuna anaeachwa

Hii hali inaniumiza Kila nikifikiri mekuaje nimejiingiza humo
Halafu yeye hajali yaani kama Hakuna kilichotokea

Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo

Nishauriwe jamani msianze kunichamba na maneno ya kejeri 🥺🥺
Lakini dada zetu muwe mnatulia, ona sasa ulimwacha ex, umeyatimba sahivi untaka kumrudia ex. Na huyo jamaa hajui kama muda huu anaitwa ex.

Dada zetu muwe mnatuliza akili mnapoamua kuchagua wachumba. Sasa unaenda kuolewa na mwanaume huna taarifa zake, unategemea nini?
 
Sidhani kama itawezekana maana ni mtu Ambae anajielewa ameelimika sio mshambamshamba.. kitabu kimepigwa sana humo na exposure ya wanawake ni mzoefu 😭
Basi mimi nilijua labda mshamba mshamba mmoja mchunga ng'ombe...umeyavagaa mwanetu, na huyo ukimuacha atahakikisha huondoki na kitu hapo
 
Kinachokusumbua ni huyo ex wako wala sio msukuma kuwa na mke mwingine. Ningekuelewa kama ungejikita kwenye kujiasses ikiwa utaweza kuishi kwenye ndoa ya uke wenza au hutaweza uondoke uendelee na maisha yako lakini kitendo cha kumzungunguzia x tayari unatia shaka, huenda ulikuwa unajua kuhusu huyo mke mwingine hukujali ila sasa kwakuwa x karudi umefanya ishu ya mke mwingine kuwa kisingizio
Binti changa karata zako vizuri, unaweza kukosa vyote kwa papara zako.
 
Lakini dada zetu muwe mnatulia, ona sasa ulimwacha ex, umeyatimba sahivi untaka kumrudia ex. Na huyo jamaa hajui kama muda huu anaitwa ex.

Dada zetu muwe mnatuliza akili mnapoamua kuchagua wachumba. Sasa unaenda kuolewa na mwanaume huna taarifa zake, unategemea nini?
Single mazas wote Tabia zao ni hizi, Unakuta kaachwa na Mume na Yule wa zamani naye anambato Tu anamtema.

Tamaa kwao zinatangulia kwanza
 
Habari za muda humu

Nitasema ukweli Kama Kuna hukumu Basi nihukumiwe wote tunakosea Hakuna mkamilifu

Nachoitaji ni ukweli mchungu hata kama utaniuma ni sawa ilimradi nisiharibu maisha yangu maana Naona kama shetani amedhamiria kuniharibia maisha

Nimeshaleta story ya Kijana wangu wa kisukuma humu mkanishauri nikashupataza shingo

Huyu mwanaume tuna miaka 3 sasa tangu 2024 na Nina miezi 7 toka nianze kuishi nae..Tulikutana nikiwa na 24 yeye aliniambia ana 27( alinidanganya now ana 35)

Amenitoa nyumbani kwetu kanipeleka mkoa anaoishi yeye(kanda ya ziwa) ndugu zangu wanajua Niko nafanya kazi kumbe nimewekwa kinyumba na msukuma

Amenifungulia Biashara ninayoiendesha mwenyewe kwani aliniambia nitafute wazo la Biashara yeye ataniwezesha ametimiza inaendelea vizuri na yeye hausiki na chochote kwenye hiyo Biashara na ananihudumia vizuri

Changamoto
Tulikuwa na ugomvi mzito tangu mwezi wa 6 baada ya kugundua ana mke (amemlipia mahari wamezaa watoto wawili kwa msukuma ukishalipiwa mahari ni mke tayari)
Ukweli nimeumia sana maana sikutegemea Kama ningekutana na kitu Kama hiki
Lakini mwenzangu yuko kawaida kabisa Kama Hakuna kilichotokea anasema ni kawaida kwao kuoa mitala nitulie Mimi ndio mke mdogo yule atabaki kwenye nafasi yake Kama mke mkubwa na Hakuna anaeachwa

Hii hali inaniumiza Kila nikifikiri mekuaje nimejiingiza humo
Halafu yeye hajali yaani kama Hakuna kilichotokea

Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo

Nishauriwe jamani msianze kunichamba na maneno ya kejeri 🥺🥺
Basi utulie , uwe mke mdogo mbona hakuna shida hapo kakufungulia Hadi biashara.
 
Single mazas wote Tabia zao ni hizi, Unakuta kaachwa na Mume na Yule wa zamani naye anambato Tu anamtema.

Tamaa kwao zinatangulia kwanza
Kuna hii tabia ya wadada akishafika mbele mambo yanaenda tofauti, anaanza kufikiri options miongoni mwa wale vijana watulivu waliowai kumtaka amchape tukio.
 
Basi mimi nilijua labda mshamba mshamba mmoja mchunga ng'ombe...umeyavagaa mwanetu, na huyo ukimuacha atahakikisha huondoki na kitu hapo
Msukuma huwezi kuondoka ukishakula Mali zake awe makini sana, unakumbuka Yule aliyepigwa Bunduki Mwanza? Unakumbuka Yule Dada celebrity alipigwa Bunduki kule Goba?
Sikiliza stori za huko Geita au Mwanza Msichana ukishalipiwa mahali na Msukuma hata kama umeshaolewa miaka 15 kujifanya unaondoka Ng'ombe zote za mahali unarudisha ustake Asitake.

We ukimdharau ma
shamba msukuma anakuonyoosha
 
Mkuu, mtu kukuficha kwamba ana familia nyingine ni kosa dogo? Kama msingi wa mapenzi yao ni uongo ili wadumu itabidi waendelee kuishi kiuongo uongo hivyo. What if huyo mwanaume ana wanawake wengine zaidi ya huyu na amemficha pia? Siku akijua wapo wanne/watano/ sita ataweza kumudu? . Mi binafsi mapenzi yanayojengwa kwenye msingi wa uongo hapana kwa kweli. Kuna vitu mtu akikuficha ni sawa, ila mtu kukuficha kama ana familia nyingine hapana kwa kweli.
Bidada anaweza kuendelea na maisha mengine cha muhimu tu asirudi kwa X, X harudiwi.
Naunga mkono hoja.

X harudiwi hata kama ni x mzuri 😂💔

Comparatively; bora msukuma kuliko X… Suggestion yangu ya kwanza ilikuwa huyu aondoke atapata mtu mwingine huko .
 
My situation: Siwezi never kamwe kurudi kwa X, siwezi never kamwe kuolewa uke wenza.

Lakini kwa situation yake, Msukuma amemkosea nini? Zaidi ya kumficha kuwa ana familia? Msukuma ni mwanaume muongo tu anayetaka kumiliki wanawake wawili kwa nguvu ya uongo. Ndio maana amemsaidia ili ajitegemee (atengeneze familia yake) na wasukuma ni kawaida yao kuwa na nyumba zaidi ya moja, hata awe mkristo, wao hujali mila zaidi kuliko dini.

Tunajuaje kuwa X anataka kumuoa kweli? Kikawaida X wanaume lazima wakurudie ndivyo walivyo, na wakirudi neno lao ni hilo hilo “nataka tuyaweke sawa nikuoe “ Hakuna ke hata mmoja kwenye circles yangu ambaye hajarudiwa na X, na ukiwa mjinga kinakuramba upya. Wanaume huwa wanakosa option huko waliko wanarudia magoma yao ya zamani, not out of love, kikawaida wanakuona mjinga, hata akikuoa ataendelea kukuona mjinga (this is my perception)

Sio ngumu kukutana na mtu mpya akaolewa…. x ni chaguo baya zaidi bora abaki na msukuma.

I stand to be corrected.
Sasa mkuu hatujajua X alijiondokea au ni bibie ndo alimuacha X. Kama bibie ndo alimuacha X kwa tamaa za fedha za msukuma, basi arekebishe makosa yake aishi na X.

Sweetie, hata Mungu hutupa nafasi ya pili tunapokosea. Yeye na X hawakufunga ndoa na kama hakukua na usaliti na sababu nzito zaidi, sioni kama kuna ubaya wakirudiana.
 
Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo
Muache ex wako ale maisha yake vizuri, wewe endelea kunyoshwa kidogo...

Cc: Mahondaw
 
Uamue huku ukimshirikisha Mungu wasukuma wengi ni washirikina utashangaa hauzai kwny ndoa mpya..ni bora umwambie ukweli na umwambie kuwa kwenu watakutenga ukiolewa mke mdogo mkubaliane uondoke
 
Dah kumbuka ngosha kakupa mtaji lakini ukitaka ukaolewe huko ni sawa uko sahihi ila jitahidi sana muachane kwa amani kwa maridhiano sisi ni pipo, point yako kuu apo mueleze hukutegemea kaoa/ku share na mtu so mbanie hapo hapo mengine watajazia wanasaikolojia nguli humu.
Nakubaliana na weww aondoke kwa amani... mwishowe alogwe bureeee
 
Sasa mkuu hatujajua X alijiondokea au ni bibie ndo alimuacha X. Kama bibie ndo alimuacha X kwa tamaa za fedha za msukuma, basi arekebishe makosa yake aishi na X.

Sweetie, hata Mungu hutupa nafasi ya pili tunapokea. Yeye na X hawakufunga ndoa na kama hakukua na usaliti na sababu nzito zaidi, sioni kama kuna ubaya wakirudiana.
Kwasababu umeniita sweetie wacha nikubali.

🤣
 
Kwasababu umeniita sweetie wacha nikubali.

🤣
Si nilishaanza kuona umeingiza utata. Kabla ya kupigwa matukio, nikiona nmekosana nae nilikuwa namkumbatia kwa nyuma mikono naweka kiunoni namwambia atulie, neno sweetie nilikuwa napenda sana kulitumia.
 
Haha pole.

Wanawake tukiwa tunampenda mtu tunataka mambo madogo sana walahi! 🥹 hivyo tu mtu analainika.
 
Back
Top Bottom