Nisikilizwe nishauriwe ukweli mtupu nisije kujuta maisha yangu yote

Nisikilizwe nishauriwe ukweli mtupu nisije kujuta maisha yangu yote

Sasa mkuu hatujajua X alijiondokea au ni bibie ndo alimuacha X. Kama bibie ndo alimuacha X kwa tamaa za fedha za msukuma, basi arekebishe makosa yake aishi na X.

Sweetie, hata Mungu hutupa nafasi ya pili tunapokosea. Yeye na X hawakufunga ndoa na kama hakukua na usaliti na sababu nzito zaidi, sioni kama kuna ubaya wakirudiana.
Tumeachana zamani sana yaani ni ex wangu wa kishuleshule hata utamu hatujawai kupeana ni zaidi ya Miaka 8

Mimi ndio nilimuacha na sio kwasababu ya mtu kwa kipindi hicho siku na hisia za kupenda nilijisikia tu kumuacha na hatukugombana japo yeye kwa miaka yote anataka tu tuwe na mahusiano
 
Uamue huku ukimshirikisha Mungu wasukuma wengi ni washirikina utashangaa hauzai kwny ndoa mpya..ni bora umwambie ukweli na umwambie kuwa kwenu watakutenga ukiolewa mke mdogo mkubaliane uondoke
Sawa japo mke wake ni wa kaskazini
 
Sawa dear
Msukuma huwezi kuondoka ukishakula Mali zake awe makini sana, unakumbuka Yule aliyepigwa Bunduki Mwanza? Unakumbuka Yule Dada celebrity alipigwa Bunduki kule Goba?
Sikiliza stori za huko Geita au Mwanza Msichana ukishalipiwa mahali na Msukuma hata kama umeshaolewa miaka 15 kujifanya unaondoka Ng'ombe zote za mahali unarudisha ustake Asitake.

We ukimdharau ma
shamba msukuma anakuonyoosha
😂😂😂 vitisho
 
Kinachokusumbua ni huyo ex wako wala sio msukuma kuwa na mke mwingine. Ningekuelewa kama ungejikita kwenye kujiasses ikiwa utaweza kuishi kwenye ndoa ya uke wenza au hutaweza uondoke uendelee na maisha yako lakini kitendo cha kumzungunguzia x tayari unatia shaka, huenda ulikuwa unajua kuhusu huyo mke mwingine hukujali ila sasa kwakuwa x karudi umefanya ishu ya mke mwingine kuwa kisingizio
Binti changa karata zako vizuri, unaweza kukosa vyote kwa papara zako.
Ukweli ndio niliouandika huyo ex hana nguvu kwangu maana hatuna bond yoyote kati yetu
 
Basi mimi nilijua labda mshamba mshamba mmoja mchunga ng'ombe...umeyavagaa mwanetu, na huyo ukimuacha atahakikisha huondoki na kitu hapo
Amna huyu msomi tena wa vyuo vya nnje so sio mshamba
 
Lakini dada zetu muwe mnatulia, ona sasa ulimwacha ex, umeyatimba sahivi untaka kumrudia ex. Na huyo jamaa hajui kama muda huu anaitwa ex.

Dada zetu muwe mnatuliza akili mnapoamua kuchagua wachumba. Sasa unaenda kuolewa na mwanaume huna taarifa zake, unategemea nini?
Duuh Sawa
Ila huyu ex wangu sio wa ukubwani ni wa utotoni na hatukuwai kuhusiana kimwili ndio maana ikawa rahisi kuachana… so nilimuacha miaka 8 iliyopita Mimi nilikuwa mtoto na yeye alikuwa mtoto so Hakuna sababu strong za kuachana
 
Relax kadogo kwa msukuma mitala ni jambo la kawaida kabisa na hutopata mateso yoyote maadam anatimiza majukumu yake we take ease kubaliana tu na hali mheshimu mke mkubwa kama hajafuata taratibu za kutoa mahali mwambie afanye hivyo.

Kwa sisi wanaume kuwa na wake wengi ni asili yetu hata kama hatuwatambulishi rasmi kama wake ila papuvhi tunaxipiga kama kawaida na tunatulia maana pia tuna uwezo mkubwa Sana wa kubalance upendo na heshima kwa wake tuna tamaa kiujumla tofauti na wanawake ambao hamjui kutofautisha tamaa na upendo ukidanganywa unapenda unajaa mazima unamsahau na mmeo.

Kwahiyo achana na huyo ex hayo yabaki kama historia tulia fanyeni maisha isitoshe tuna muda mfupi Sana hapa duniani unaweza kwenda kwa ex ukakuta naye anakutamani tu na hana future na wewe haiwezekani kwa muda wote huo asiwe na mtu.

Usukumani suala la wake wengi siyo issue kabisa na wanawake wanaelewana tu kama mtu na mdogo au wadogo zake. Tulia tunza familia usikigawe hicho kipapiro kwa wengine kisa mmeo ana mke mwingine.
Ngoja tuone
 
Pole sana, umeolewa na mume wa mtu bila kujua ni mume wa mtu sio! Pole sana.

Ni wakati wa wewe kukubaliana na hali, na kufanya maamuz ambayo utaishi kwa amani. Husifanye maamuzi kwa hisia ukaja kujudia baadaye.
Sawa Asante
 
Kama unatafuta "ukweli mchungu", basi ni huu:
  • Usibaki kwa sababu tu amekufungulia biashara au anakuhudumia vizuri. Hayo ni mambo ya kuzingatia, lakini yasikufanye uvumilie uhusiano ambao msingi wake ulianza kwa udanganyifu.
  • Jiulize kama ungekuwa umejua siku ya kwanza kwamba ana miaka 35, ana mke na watoto, ungeingia kwenye uhusiano huo? Kama jibu ni hapana, hiyo ni ishara muhimu.
  • Mitala ni chaguo ambalo baadhi ya watu hulikubali kwa misingi ya mila au imani zao. Lakini si lazima nawe ukubali. Una haki ya kusema, "Sikuwa nimekubali kuwa mke wa pili."
Sawa Ila Kama chartgpt maana alinijibu hivi 🤣🤣🤣
 
Ila huyo jamaa kamdanganya vitu vingi sana, mtu kusema miaka 27 wakati ana 35 hata macho huoni?

Sema Mshikaji alikuwa Msukuma na kama Demu ana Rangi nyeupe basi alimpaghai kwa pesa na simu nzuri nzuri hapa hakuna Mwanamke anachomokaga
😂😂 Mimi kweli ni mweupe pee Ila kwenye mahusiano hakuwai kunihonga kitu kikubwa labda tukionana ndio aniachie kakitu..

Kuhusu umri nafikiri aliniona ni mdogo yeye ni mkubwa akitaja umri wake naweza mkataa labda alijua nitataka wa rika langu
Kimuonekano hiyo Miaka 35 hafiti labda 30
Miaka yake niligundua nilipoona pasport yake

Anyway tulikutana Dar na yeye alikuja kikazi hakukuwa makazi yake so hata kuonana kwa miaka yote Mimi nilikuwa namfuata alipo mpk mwaka huu ndio tunakaa wote
 
😂😂 Mimi kweli ni mweupe pee Ila kwenye mahusiano hakuwai kunihonga kitu kikubwa labda tukionana ndio aniachie kakitu..

Kuhusu umri nafikiri aliniona ni mdogo yeye ni mkubwa akitaja umri wake naweza mkataa labda alijua nitataka wa rika langu
Kimuonekano hiyo Miaka 35 hafiti labda 30
Miaka yake niligundua nilipoona pasport yake

Anyway tulikutana Dar na yeye alikuja kikazi hakukuwa makazi yake so hata kuonana kwa miaka yote Mimi nilikuwa namfuata alipo mpk mwaka huu ndio tunakaa wote
Well
 
Back
Top Bottom