Nisikilizwe nishauriwe ukweli mtupu nisije kujuta maisha yangu yote

Yani uolewe na mwanaume ana wanawake wengi, uamue kujua na husijue. Au tuseme hakuzingatia kama ni suala la msingi! Unaassume maisha kwenye future!
Ndo sasahivi kagundua huyo mwanaume ana mke mwingine, alikuwa amemficha.
 
Ndo sasahivi kagundua huyo mwanaume ana mke mwingine, alikuwa amemficha.
Ni mambo ya kawaida atulie awe mke mwenza tu. Si anapewa kila kitu! Kama anaona hawezi, sivunji ndoa za watu mimi πŸ˜‚
 
ukienda kwa uyo x wako nae akioa mke mwingine mbeleni una hama pia
Obvious ataoa Mwingine, Maana huwezi kumuachia mtu ukaolewa harafu yakikushinda urudi, umeshatunduliwa miaka na miaka ndio urudi kwangu?
 
Ni mambo ya kawaida atulie awe mke mwenza tu. Si anapewa kila kitu! Kama anaona hawezi, sivunji ndoa za watu mimi πŸ˜‚
Mimi sina shida na ukewenza kama mtu karidhia,shida ni pale ambapo yeye hajaridhia. Kama ameridhia aishi tu mbona wengine wanaishi. Tatizo sio kila mwanamke anataka au anamudu mitara, ila anaemudu aende,sheria za nchi zinaruhusu.
 
Lakini dada zetu muwe mnatulia, ona sasa ulimwacha ex, umeyatimba sahivi untaka kumrudia ex. Na huyo jamaa hajui kama muda huu anaitwa ex.

Dada zetu muwe mnatuliza akili mnapoamua kuchagua wachumba. Sasa unaenda kuolewa na mwanaume huna taarifa zake, unategemea nini?
 
Sidhani kama itawezekana maana ni mtu Ambae anajielewa ameelimika sio mshambamshamba.. kitabu kimepigwa sana humo na exposure ya wanawake ni mzoefu 😭
Basi mimi nilijua labda mshamba mshamba mmoja mchunga ng'ombe...umeyavagaa mwanetu, na huyo ukimuacha atahakikisha huondoki na kitu hapo
 
Kinachokusumbua ni huyo ex wako wala sio msukuma kuwa na mke mwingine. Ningekuelewa kama ungejikita kwenye kujiasses ikiwa utaweza kuishi kwenye ndoa ya uke wenza au hutaweza uondoke uendelee na maisha yako lakini kitendo cha kumzungunguzia x tayari unatia shaka, huenda ulikuwa unajua kuhusu huyo mke mwingine hukujali ila sasa kwakuwa x karudi umefanya ishu ya mke mwingine kuwa kisingizio
Binti changa karata zako vizuri, unaweza kukosa vyote kwa papara zako.
 
Single mazas wote Tabia zao ni hizi, Unakuta kaachwa na Mume na Yule wa zamani naye anambato Tu anamtema.

Tamaa kwao zinatangulia kwanza
 
Basi utulie , uwe mke mdogo mbona hakuna shida hapo kakufungulia Hadi biashara.
 
Single mazas wote Tabia zao ni hizi, Unakuta kaachwa na Mume na Yule wa zamani naye anambato Tu anamtema.

Tamaa kwao zinatangulia kwanza
Kuna hii tabia ya wadada akishafika mbele mambo yanaenda tofauti, anaanza kufikiri options miongoni mwa wale vijana watulivu waliowai kumtaka amchape tukio.
 
Basi mimi nilijua labda mshamba mshamba mmoja mchunga ng'ombe...umeyavagaa mwanetu, na huyo ukimuacha atahakikisha huondoki na kitu hapo
Msukuma huwezi kuondoka ukishakula Mali zake awe makini sana, unakumbuka Yule aliyepigwa Bunduki Mwanza? Unakumbuka Yule Dada celebrity alipigwa Bunduki kule Goba?
Sikiliza stori za huko Geita au Mwanza Msichana ukishalipiwa mahali na Msukuma hata kama umeshaolewa miaka 15 kujifanya unaondoka Ng'ombe zote za mahali unarudisha ustake Asitake.

We ukimdharau ma
shamba msukuma anakuonyoosha
 
Naunga mkono hoja.

X harudiwi hata kama ni x mzuri πŸ˜‚πŸ’”

Comparatively; bora msukuma kuliko X… Suggestion yangu ya kwanza ilikuwa huyu aondoke atapata mtu mwingine huko .
 
Sasa mkuu hatujajua X alijiondokea au ni bibie ndo alimuacha X. Kama bibie ndo alimuacha X kwa tamaa za fedha za msukuma, basi arekebishe makosa yake aishi na X.

Sweetie, hata Mungu hutupa nafasi ya pili tunapokosea. Yeye na X hawakufunga ndoa na kama hakukua na usaliti na sababu nzito zaidi, sioni kama kuna ubaya wakirudiana.
 
Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo
Muache ex wako ale maisha yake vizuri, wewe endelea kunyoshwa kidogo...


Cc: Mahondaw
 
Uamue huku ukimshirikisha Mungu wasukuma wengi ni washirikina utashangaa hauzai kwny ndoa mpya..ni bora umwambie ukweli na umwambie kuwa kwenu watakutenga ukiolewa mke mdogo mkubaliane uondoke
 
Nakubaliana na weww aondoke kwa amani... mwishowe alogwe bureeee
 
Kwasababu umeniita sweetie wacha nikubali.

🀣
 
Kwasababu umeniita sweetie wacha nikubali.

🀣
Si nilishaanza kuona umeingiza utata. Kabla ya kupigwa matukio, nikiona nmekosana nae nilikuwa namkumbatia kwa nyuma mikono naweka kiunoni namwambia atulie, neno sweetie nilikuwa napenda sana kulitumia.
 
Si nilishaanza kuona umeingiza utata. Kabla ya kupigwa matukio, nikiona nmekosana nae nilikuwa namkumbatia kwa nyuma mikono naweka kiunoni namwambia atulie, neno sweetie nilikuwa napenda sana kulitumia.
Haha pole.

Wanawake tukiwa tunampenda mtu tunataka mambo madogo sana walahi! πŸ₯Ή hivyo tu mtu analainika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…