Nisipowaambia ukweli nitahukumiwa siku ya mwisho. Haya ni machukizo kwa Mungu

Huu nao ni usanii kama mwingine tu.
Mathayo 24:8
Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.

Mathayo 24:8
Mateso Yatabiriwa

Mathayo 24:9
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.

Mathayo 24:10
Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.

Mathayo 24:38
Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,

Mathayo 24:39
wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
 
Kuna dini zingine ni Peponi kwa muumini akiwa duniani, na zingine ni jehanamu kwa muumini duniani,
 
10. Mapambo kwa wanawake ni machukizo mbele za Mungu
11. Kuvaa nguo zisizo na staha ni machukizo mbele za Mungu
12. Wananwake kua mchungaji kiongozi ni machukizo mbele za Mungu
 
Umesahau kitu kimoja, hiyo biblia pia wao ndio wameihifadhi na ndio wame-iframe
ambayo ndio msingi wa madhehebu yote ya kikristo.
 
Umesahau kitu kimoja, hiyo biblia pia wao ndio wameihifadhi na ndio wame-iframe
ambayo ndio msingi wa madhehebu yote ya kikristo.
Luka 19:40
Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.

Roho Mtakatifu akuongoze kwenye hili pia
 
Mbona hujibu kwamba hiyo biblia hao ndio walikuwa nayo pia na wameiframe wao
Bibilia ni mkusanyiko wa Maandiko Matakatifu na ukiiondoa Injili ambayo waandishi wake wengi walifahamiana na kuishi karne moja lakini agano la kale ambalo ndo msingi wa agano jipya, waandishi wake hawakufahamiana na hawakuishi pamoja. Hebu fikiria nikikwambia Ayubu hakuwa Muisrael kama alivyokuwa Rahabu wa Yeriko na kadhalika.

Kuishika ama kuiunganisha Biblia kwenye mtiririko siyo hakimiliki ya kuhodhi njia ya kwenda uzimani. Kumbuma Eli Kuhani alisikiwa na Mungu ingawa alitenda uovu yeye na wanae.

Nimekupa huo mstari wa Neno la Yesu kuhusu mawe kunena kwa sababu mawe hayana uhai wala nafasi kwenye ufalme wa Mungu lakini anayweza kuyatumka kueneza habari za Ufalme wake kama vile Balaamu alivyowabariki wana wa Israel pale alipoitwa na Balaki ili awalaani
 
Mkuu Msanii amani iwe nawe. No. 2 Naomba nikupe andiko kabisa Kumbukumbu la Torati 4:15-19
Barikiwa sana mkuu.

Kumbukumbu la Torati 4:15
Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;

Kumbukumbu la Torati 4:16
msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke,

Kumbukumbu la Torati 4:17
mfano wa mnyama ye yote aliye duniani, au mfano wa ndege ye yote arukaye mbinguni,

Kumbukumbu la Torati 4:18
au mfano wa kitu cho chote kitambaacho juu ya ardhi, au mfano wa samaki ye yote aliye majini chini ya nchi;

Kumbukumbu la Torati 4:19
tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.
 
mleta mada akasome biblia ya vitabu72siyo ya66 hapo ataona kuhusu maelezo yake ya namba7
Mkuu wangu
Siyasemi yaliyo yangu. Bali leo nimejiwa na hizi aya na sijui zimejipangaje kichwani kwangu.

Hivyo nitatekeleza agizo lako kwa sababu najitahidi sana kusoma maandiko mbalimbali kuupa elimu ufahamu wangu
 
Unaruka ruka kama maharage, hivyo vitabu unavyo quote sio
wacatholic ndio walio vi-release wewe ukasoma!?
Kuna maandishi ya kale ya biblia ambayo wewe unayo au kanisa lako zaidi
ya wacatholic!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…