YESU KRISTO alifundisha Amri zote kumi za MUNGU wala hakupunguza wala kufuta hata moja.
Amri ya kuabudu siku ya saba (Sabato) iko pale pale na ndiyo maana BWANA YESU alisema yeye ni "BWANA WA SABATO".
Kuikataa "sabato" na kuabudu siku ya Jumapili ni machukizo kwa MUNGU. Kitendo cha kuabudu siku ya Jumapili ni kuvunja Amri ya 4 ya MUNGU. Yeyote atakayevunja hata Amri moja ndogo hataingia kamwe kwenye UFALME WA MUNGU.
Kuna watu watakuja na vifungu kutoka "Warumi" , "Wakolosai" na "Wagalatia" wakisema Mtume Paulo aliifuta sabato. Siyo kweli hata kidogo, Mtume Paulo hakuifuta Sabato bali maandiko yake yalipotoshwa makusudi ili kuwapoteza wengi. Mtume Petro alitahadharisha mapema sana kuhusu upotoshaji wa maandiko ya Mtume Paulo.
Soma 2 Petro 3:15-17
"15 Hesabuni uvumilivu wa Bwana kuwa ni wokovu, kama ndugu yetu mpendwa Paulo alivyokwisha kuwaandikieni kwa hekima aliyopewa na Mungu. 16 Ameandika hivyo hivyo katika barua zake zote akizun gumzia mambo haya. Barua zake zina mambo mengine ambayo ni magumu kuelewa, ambayo watu wajinga na wasio na msimamo huyapotosha, kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko; na hivyo wana jiletea kuangamia.
17 Basi, ninyi wapendwa mkijua haya, jihadharini msije mka potoshwa na makosa ya hao waasi na kupoteza uthabiti wenu.
Ukisoma waraka kwa Waebrania utaona kuwa Mtume Paulo anasisitiza umuhimu wa kuishika siku ya "Sabato", tena anasema wazi wazi kuwa yeyote yule asiyepumzika katika kazi zake hawezi kamwe kuingia katika pumziko la MUNGU, yaani raha ya milele katika Ufalme wa MUNGU. Someni Waebrania 4:9-11
"9 Kwa hiyo basi ipo bado sabato ya mapumziko waliyowekewa watu wa Mungu; 10 kwa maana, mtu anayeingia katika pumziko la Mungu, pia hupumzika kutoka katika kazi zake kama vile Mungu alivyopumzika baada ya kazi zake.
11 Basi tujitahidi kuingia kwenye pumziko hilo asije mtu akaanguka kwa kutokuamini kama hao."
Wapendwa, nawakumbusheni tu kuwa MUNGU hana kigeugeu (1 Samweli 15:29) "Yeye aliye Utukufu wa Israeli hasemi uongo wala hana kigeugeu; kwa kuwa yeye si mwanadamu, hata abadili nia yake.”
MUNGU hajabadili nia yake wala Amri yake ya 4. Amri ya kuishika Sabato iko pale pale. Hata YESU KRISTO alisisitiza hilo kwa kusema; "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni".
Kuikataa "sabato" na kuabudu siku ya Jumapili ni kuvunja Amri za MUNGU. Mwenye masikio na asikie!!!