Nitawashangaa watoto wa Lemutuz wakigandana huko Marekani na kutelekeza mirathi ya baba yao

Nitawashangaa watoto wa Lemutuz wakigandana huko Marekani na kutelekeza mirathi ya baba yao

Yule binti mnamuonea bure tu inavyoonesha alikuwa teyari kuyamaliza na mshua wake Le Mutuz ndiye aliyezingua lkn yule dogo wa kiume ni fala wa kiwango cha juu sana huwezi kumjibu dingi yako vile.

Ktk malezi ya single mamaz wakiume ndio huwa wanahama njia na kuwa viazi,ila watoto wa kike akili huwa kwa baba zao.
 
Sitashanga wasipoona hilo maana tayari akili hawana, kwa afya yake ilipokuea imefikia Lemutuz alikua afe lakini hao watoto wamemuongezea speed

Baraka ni maneno, Mali na Pesa ni matokeo ya baraka
Baraka zinafuata mkondo toka kwa Mungu, zinashuka kwa baba kisha kwa watoto

Nawahurumia sana watoto wa lemutuz kwa waliyomwambia baba yao baada ya baba kuwaomba msamaha. Kuna siku watatamani arudi waongee

KUTOKA 20:12
“WAHESHIMU BABA yako na MAMA yako, ili uishi MAISHA MAREFU katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.

Natamani waupate huu ujumbe.
 
Wanaume wengi wa kiafrika hawajui kuomba msamaha wanapokosea, wale wachache wanaoombaga msamaha na kukubali makosa pepo inawasubiria

Mungu wetu nae kwa kujua tutaleta mashindano kwa watoto kupuuza nafasi aliyompa mzazi kuzaa na kulea akaamua awe dikteta kwa kutoa amri ya kumheshimu mzazi bila kuwa na conditions.

“Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako."

Pole sana kwao
Mwanaume utaombaje msamaha kwa mtoto asiyeelewa umetoka wapi na mama yao?

What if Mwanamke alikwambia huyu mtoto si wako halafu miaka mingi baadae akaja akakwambia ni wako nilikuwambia vile sababu ya hasira tu?

Unataka hayo nayo umwambie mtoto?
 
Nakubali kaka, ni kweli 25k kwa America sio hela mingi... ila ndo mana nimeiweka kama free cash flow maana yake hapo anakuwa amesha cover expenses zote.

Halafu kwa US mtu akipata hiyo 30k ataweza save kiasi gani? Hilo nalo ni suala la kujiuliza. Ama ndo inakuwa kama subsistence wages... ukipata yote inaishia kwenye matumizi

Mimi nime refer zaidi watoto wa Lemutuz, je huko state wana maisha ya kuwafanya wao kutengeneza hiyo net ya 25k? Kama wanayo its fine... ila kama wapo huko state wanapiga ukwara, mi nadhani angekuja mmoja kusimamia bidhara ya mshua... huwezi jua
Msiwapime hivo wale hawaingii mtaani kama wabongo waliozamia.wakimalizq chuo wataajiriwa mshahara wa chini dola 7000 x12=84k usd na insurance ya afya juu
 
Jamaa alikuwa mpambanaji. Fikiria mtoto wa waziri mkuu mstaafu then awe dereva wa taka, tena sio taka tu ni harzadaus waste ambazo zinahitaji special care.
Kumbuka kuwa ni dereva w taka New York City na sio bongo.

Kuna mtoto baba yake ni Rais Africa na yy anaishi Marekani.

Mbele ni mbele tu mkuu
 
Hata kama hawana aibu, hawataweza kupanda Ndege Kuja bongo na kusema wamefuata sijui urithi au kitu chochote cha baba yao kwa jinsi walivyomalizana nae vibaya. Majuto ni mjukuu.
 
Mi naona Lemutuz alikuwa mjasiriamali mpambanaji kwenye sekta ya social media na matangazo. Sekta ambayo kwa Tanzania na kwa ukubwa wake na mazingira ya matangazo mitandaoni, inaweza kuwa na potential ya kukuingizia sio chini ya free cash flow ya Tsh. 5 hadi Tsh. 6 million kwa mwezi ukiondoa gharama za uendeshaji.

Maana yake hiyo inakupa kama Tsh. 60 millioni kwa mwaka au (USD 25,000) na hiyo nadhani ni makadirio ya chini na kati. Sasa sijui kama kuna mtoto wa Lemutuz ambaye yeye huko Marekani anaweza kutengeneza net income ya USD 25,000 kwa mwaka.

Maana yake ni kwamba, mi naona ingekuwa vizuri sana walau hata mtoto mmoja angekuja kusimamia hii biashara ya baba yao na kuiboresha zaidi.

Kwa mahesabu ya ki finance, kwa average return ya 20% kwa mwaka na kwa annual free cash flow ya Tsh. 60 million kwa mwaka, hiyo maana yake inaipa biashara ya Lemutuz, valuation ya kati ya Tsh. 250 milllioni mpaka Tsh. 300 millioni.

Ndio maana narudia tena kusema, nitawaona hawa watoto hawana akili kama wakigandana huko Marekani na kuacha mali ya baba yao ikipotea bure.

Naomba ushauri huu uwafikie popote walipo.
Unaambiwa watoto hawana akili kama Mama yao, wako bize kutukana watu tu mitaani na kuwalazimisha wa suck their dicks.
 
Back
Top Bottom