Nitumie mbinu gani kumfikishia ujumbe girlfriend wangu kuwa hajui kupika pasipo kumuudhi?

Nitumie mbinu gani kumfikishia ujumbe girlfriend wangu kuwa hajui kupika pasipo kumuudhi?

Mimi nilikuwaa na gf wangu, alikuwa hajui kupika nilivumilia siku moja nikamwambia hebu leo kaa kwanza nikupikie chakula na mimi, kwa kupika wali ni mimi ni fundi yani ni fundi haswa, nikampikia wali wangu mmoja matata unachanganywa na beef masala, alipokula alijua kuwa hajui kupika na akaomba nimwelekeze... nikamwelekeza kuanzia siku hiyo akajua jinsi ya kupika wali siyo uji.

Hii comment imefanya nijione sijui kupika, wali wa beef masala 😂
 
Unakuaje kwenye mahusiano na mtu unashindwa kumchana? We mwambie tu "baby hujui kupika, sasa tutafanya nini kuhusu hilo swala?". You should learn to solve your problems.
well noted
 
Hivi mapishi ya Kitanzania kuna watu waneandika vitabu vya mapishi kufundisha kupika vyakula mbalimbali?

Kuna kitabu cha recipes za mapishi ya Kitanzania?
Vipo vingi sana baba.
 
Mfundishe kupika tu, kama na ww ujui kupika bas mwambie "baby mwakan nafungua mgahawa mkubwa na wenye hadhi hapa mjini na ww ndio utakuwa msimamizi na mpishi mkuu, so inabidi ukachukue short course ya mapishi ili uwe na ujuzi wa kupika vyakula mbalimbali kwaajiri ya special guest"
Had hapo utakuwa umemaliza
 
.......hayo maeneo niliotaja ni kumenya kuweja maji na chumvi basiii ndo wanachojua.
Mkuu, kama ulikuwepo unachosema. Nilibahatika kuishi kanda ya ziwa miaka mitatu. Chakula nilichokuwa napikiwa ndani ni staili hiyo. Ilifika kipindi nikaona chakula nachopika Mimi mwenyewe kitamu
 
Huu ni mtifuano wa wapikiwa na wala vizuri kwa wapishi wabovu lakini wapenda vizuri
 
Msifie tu,mwambie Unajua Kupika sanaa basi hapo atazidisha ufundi.
 
Unakuaje kwenye mahusiano na mtu unashindwa kumchana? We mwambie tu "baby hujui kupika, sasa tutafanya nini kuhusu hilo swala?". You should learn to solve your problems.
Mkeo, mumeo, mchumba ni vyema ujue approach za kumfanya mwenza wako asijisikie vibaya wakati wa ku address issue inayokukera kuepuka makwazo yasio nalazima, ukimwambia kwa kumchana unafikiri ndiyo utakua umemsaidia au umemuongeza uoga zaidi,
 
Hello JF.

Ebana nina mtihani hapa ndugu zangu kuna huyu bibie niko naye, kiukweli huyu mrembo hajui kupika kabisa, yawezekana hata mimi namshinda, akikupikia wali utadhani ugali na msosi unakuwa hauna ladha kabisa. Cha kusikitisha yeye hajui kuwa msosi anaopika hauna ladha.

So nimepanga kumfikishia ujumbe kuwa hajui kupika ila sitaki kumuudhi.

Naombeni mbinu wakuu.

Tafuta dada yako aje au rafiki yake anaejua kupika ndipo apike chakula kizuri unachokipenda au wapike wote huko huko jikoni watasemana kwamba wanaume anapenda chakula kipikwe na kwa maandalizi mazuri
 
Tafuta dada yako aje au rafiki yake anaejua kupika ndipo apike chakula kizuri unachokipenda au wapike wote huko huko jikoni watasemana kwamba wanaume anapenda chakula kipikwe na kwa maandalizi mazuri
ok..nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom