Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mkuu msaada wako gari ndogo ukiwa unaondoka toka kwenye park inakuwa na spridi ndogo baadae inashtuka na spridi inachanganya. Msaa tatizo laweza kuwa ni Nini?
 
Jibu sahihi la Atf ya gari yako ni kuangalia dipstick au chukua chassis no ya gari na google utapata jibu sahihi na mara nyingi gari za automatic zinatumia giabox oil tofaut tofaut

So far biashara unaiona inaendaje mkuu?
 
Mkuu, ubora wa engine unapimwa vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipimo rahisi ni kuwa silence iwe nzuri ya kati ya 500 rpm mpaka 1000rpm, na iwe inapokea accelerator vizuri sana kwa kugusa tu. Vingievyo utahitaji uiweke kwenye computer kupima perfomance metrics nyingine jambo ambalo ni la kitaalam zaidi.
 
Kuna mtaalam aliniambia inatakiwa ikiwaka iwe na mlio mkubwa kisha upungue, hili lina ukweli wowote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli lakini huo siyo ushauri wa kitaalamu.
Kuna mtu kanitumia swali kule kwenye PM akitaka kujua kuwa kwa nini huo siyo ushauri wa kitaalamu. Sikumjibu kule nikasema nitatoa jibu la jumla hapa, na nitamtuma aje kulisoma hapa.

Kanuni ya kwanza ya Nyutoni inasema kuwa asili haitaki kubugudhiwa, sijui kama nimepatia maneno hayo kwa kiswahili vizuri. Fizikia inatufudisha kuwa asili ikiwa imetulia hutaka iendelee kutulia tu, na ikiwa katika kwendo basi inataka iendelee na mwendo huo tu. Sasa ukiistuta asilia kutoka mazingira yake ya faraja, huruka sana kabla ya kutulia katika faraja nyingine.

Ndiyo maana ukiwa abiria kwenye basi likianza kundoka utatitikisika kidogo na baadaye kutulia katika nafasi yako hadi basi basi hilo litakapobadilisha mwendo ghafla au kusimama; kwenye ndege pia wakati wa kupaa wale wahudumu wa ndege waatakuambia funga mkanda wakati ndege inaaaza kuruka, na watakuambia pia funga mkanda wakati ndege inataka kutua, ukiwa angani kwenye mwendo unaweza kutokuwa na mkandao huo. Hiyo yote niwa kwa sababu ya kanuni hiyo ya kwanza ya Nyutoni. Wanafizikia wanaiitia step response. Graph yake ni kama hii ambayo inaaza kwa kuruka juu halafu baadaye inatulia
1591160096038.png

Kwa hiyo injini yoyote iwe mbovu au isiwe mbovu inaponza kuwaka bado itaruka kwenye spidi za juu kabla ya kutulia kwenye spidi yake. Ndiyo maana nikasema kuwa madai ya lazima iruke kidogo kabla ya kutulia siyo majibu la kitaalamu kwani hiyo ni tabia ya asili ya kitu chochote.
 
Habari mkuu,
Nilifanya diagnosis kuhusu gari yangu kuwa speed ndogo na odometer kusoma speed kuwa let's say unaona kabisa upo 70km/hr ila odometer itasoma 95 - 100km/hr.

Mtu wa diagnosis akaniambia strainer na "Knock sensor bank 1" ndio zina shida, je nikibadilisha gari yangu itakuwa poa? Maana hata kubadili gear haipo Safi kuna muda inaishia gear namba 3, gari yangu ni Rav4 kilitime automatic transmission.
 
Japo siye uliyeniuliza swali
Je, ni knock sensor inareport error au knock sensor ni mbovu?

Muhimu kujua pia mambo ya usomaji wa RPM yana uhusiano mkubwa na CRANKSHAFT POSITION SENSOR na KNOCK SENSOR kwapamoja.
 
Back
Top Bottom