Ni nani/watu gani waliopanga vita hivi;
Urusi -->Ukraine,
Israel -->Hamas,
Machafuko ya Congo[DRC],
Machafuko ya Sudan.
Ni kwanini/sababu ni nini?
Ukraine na russia —— Nato aggression au kujaribu kuizunguka russia by USA.
Russia ye ndo kaanza
Irael Vs Hamas
Huu n mgogoro wa muda mrefu
Chanzo chake ni kutokubaliana kwa waarabu na mgawanyo wa ardhi ya palestine territor
Lakini chanzo cha Octobar 7 inasadikika ulikua n mpango wa iran ili kuzuia mkataba kati ya israel na Saudi arabia.
Machafuko ya kongo
-Hizi ni coporation za ulaya na marekani ambazo zinataka kupora madini hivo zinawatumia nchi vibaraka rwanda na Uganda kuchochea machafuko ya na kutorosha madini
Machafuko ya sudan
Haya yanaanza na dikteta Al bashir ambae alitaka kuigeuza sudan kuwa nchi ya kiislam bila kuzingatia utofauti wa jamii ya sudan
Ikasababisha kujigawa kwa sudan kusini
Lakini kubagaguliwa kwa watu weusi na waarabu wa kasiskazin mwa Sudan kukafanya kuanza upinzani wa maeneo ya kodofan na dafur.
Kupambana nao akawapa silaha kundi la kabila la kiarabu la janjaweed kuvamia na kuwaua raia weusi wa sudan.
Kundi hili ndio linalokuja kujibrand kama RSF.
Kwakua al bashir alitawala kwa mkono wa chuma maandamani ya wasudan yanakua hayaishi hivo mageneral wanaamua kumpindua akisalitiwa na general pia wa kundi lake ambalo ljmekua likimlinda la rsf.
kwa uchu wa kumiliki nchi magenge au makundi haya mawili yanatofautiana kati ya rsf na jeshi la sudan wanaanza kupigana kutaka kila mtu kuchukua nchi.
Katika vita yyte bas wapambe huingia ambao huwa wanatka kufaidi nchi katika upande utaoshinda
UAE ambae alikua akiuziwa madini na RSF inatumia nafasi hii kulisapoti kundi la rsf kwa kuingiza silaha na pesa kupitia bandari za somalia
wakat huo jeshi la sudan nalo likisaidiwa na iran.
Utaka ujue kwanini RSF inakua na nguvu.
Siri ni kua inatumia vifaa vikali kutoa US ambavyo viliuzwa kwa UAE.
UAE inatumia silaha hizi kufadhili vita ya sudan.