NIULIZE SWALI: Hii vita ya USA, Israel vs Iran, nani mshindi?

Ili kufaham nani kafanikiwa na sio kushinda tuanze na kujikimbusha malengo ya hii vita yalikuwa yapi?
Je yamefanikiwa?
Lakini nani baada ya vita kusimama anaonekana kutoa mashart na muelekeo.?
 
Mbabe ni nani? Naona kama vile Iran anawapelekesha puta hawa magwiji wa kila kitu duniani!

WHO IS THE WINNER Echolima1
Vita vya siku hizi inapiganwa KIMKAKATI na sio kutafuta mshindi kama mashindano.

USA/ISRAEL Mkakati wao mkuu ilikua ni kumdhoofisha Iran kwenye mpango wake wa nyukilia, kuharibu au kupunguza kasi ya Iran kutengeneza silaha kali zaidi, kuchochea uasi wa ndani na kufyeka viongozi wakuu kadiri iwezavyo

IRAN Mkakati wao ilikua ni KUJILINDA na kulipiza kisasi, kuhakikisha haijalishi watauliwa viongozi wangapi lakini serikali lazima ibaki stable
Kuhakikisha Dunia yote inafeel maumivu wanayopitia kushambuliwa kwa kuuthibiti mlango bahari na biashara ya mafuta

Kila mmoja kwa mikakati yake kuna sehemu kafanikiwa na sehemu kafeli

Mwisho wa siku vita hii imetuumiza wengi kwenye upande wa mafuta
 
Mbabe ni nani? Naona kama vile Iran anawapelekesha puta hawa magwiji wa kila kitu duniani!

WHO IS THE WINNER Echolima1
Ni akili za kipimbi tu kuamini kuwa Iran ambayo Inapigwa kama ngoma inashinda vita.

Ni upimbi kuamini Iran ambayo imepoteza viongozi wake wa serikali na kijeshi zaidi ya 300 walio angamizwa na Majeshi ya Israel.

Ni upimbi kuamini Iran ambayo imepoteza jeshi lake lote la anga(Airforce) kuwa Inashinda.

Ni upimbi kufikiri kuwa Iran ambayo Mifumo yake yote ya ulinzi wa anga iliangamizwa na majeshi ya Israeli na sasa Ndege-vita za Israel na Marekani zinaingia na kutoka kwenye anga la Iran bila kikwazo chochote harafu unadai kuwa Iran inashinda!!

Ni upimbi kuamini kuwa Iran ambayo kuna ndege-vita ya marekani ilianguka na marekani wenyewe kwa msaada wa Israel waliweza kuja na kuwachukua marubani wao bila kikwazo chochote halafu udai kuwa Iran inashinda!!

Ni upimbi kufikiri Iran anashinda vita wakati Meli-Vita zake zote sasa hivi ziko chini ya bahari zimezamishwa na Majeshi ya Israel na Marekani!!

Ni upimbi uliopindukia kuamini Iran inashinda wakati hakuna mtawala wa nchi hiyo maana kila mmoja anajisemea tu anapojisikia maana hata Majitaka Khamenei naye hajulikani alipo!!
 
Mayahudi wa Chifumfu uwanja uko wazi mje kujimwagia sifa za ushindi
 
Kutukana si kujenganhoja! Achana na mambo ya Upimbi! Nina uhakika kama USA angelikuwa amefanyanhayo yote uliyoyasema kwa. Kutukana, Hormuz ingelikuwa wazi to date! Meli zote zingelipita bila vikwazo under USA capture!

Matusi si hoja!
 
Nataka mafuta 1 litre ipande mpka 15k ili akili zitukae sawa
 
Kutukana si kujenganhoja! Achana na mambo ya Upimbi! Nina uhakika kama USA angelikuwa amefanyanhayo yote uliyoyasema kwa. Kutukana, Hormuz ingelikuwa wazi to date! Meli zote zingelipita bila vikwazo under USA capture!

Matusi si hoja!
Una akili kweli kufikiri Iran apigane na Marekani na Israel harafu Iran aibuke mshindi!!!!

Kama una mawazo hayo basi nakushauli sana ukimbie haraka sana Dodoma kuna Hospital inaitwa Milembe!!
 
Kwanin Hormuz ni muhimu kwa Africa ilihali
Kuna nch za Africa zinazalisha mafuta?

Waafrika ni watu wajinga sana, umasikini tulionao kwenye bara hili ni kwasababu ya viongozi na raia vilaza kwenye nchi zote 54.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…