kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Dini zetu hizi mbili zina bahati mbaya sana Afrika, ujio wake Afrika uliambatana na watu waliotenda mabaya na wanaendelea kuyatenda mabaya Afrika mpaka leo. Bahati mbaya sana watu wa dini hizi hawakuwakemea na hawawakemei hadi sasa. Walikuwa wakiwasalisha na wanawasalisha mpaka sasa bila kuwataka waungame kwa kile walichoitendea Afrika na wanachoendelea kuitendea Afrika.
Waarabu walikuja na dini ya Kiislamu pamoja na wafanyabiashara wa viungo, pembe za ndovu na watumwa. Waarabu hawajawahi kuomba ladhi na hawaombi ladhi mpaka leo. Watu wa dini hii walikuwa wanawaswalisha na wanawaswalisha mpaka leo, ni rafiki zao.
Wazungu walikuja na dini ya Ukristo kama wamisionari na baadae wakafuatiwa na wakoloni (watesi wetu). Wamisionari hawa walikuwa wakiishi mtaa mmoja na wakoloni waliotununua na kutusafirisha kama watumwa, walipora rasilimali zetu na kuua tunapokataa kunyonywa na kutawaliwa. Wasionari hawa walikuwa wakiwasalisha wakoloni bila kuwataka waungame, ni rafiki zao.
Watu wa dini hawa wasifikiri kuwa hatujui kuwa masheikh wana uhusiano na waarabu walitufunga minyororo na maaskofu wana uhusiano na wakoloni wetu waliotuibia rasilimali zetu. Sisi tunajua na serikali inajua pia.
Watu wa dini ni marafiki wakubwa wa watesi wetu maana walikuwa ni waumini wao wakubwa; hivyo wanapotaka kufanya siasa hapa Afrika wasisahau hilo ili wasije wakaeleweka na kudhaniwa vibaya. Kama walivyokuwa wakiwasalisha na kuishi na watu waovu (wakoloni) bila ya kuwakemea wanyamaze hivyohivyo milele hata kwa wanasiasa wa Kiafrika la sivyo wataonekena kama vile wamebeba ajenga kuhusu rafiki zao (wakoloni). Hakuna ubishi kuwa watu wa dini walisikitika sana wakati wakoloni (waumini wao) walipoondoshwa Afrika.