Niwaombe watu wa dini wakae mbali na siasa za Afrika

Mbaya zaidi hawa viongozi wa dini ni kama vile huwa wanachagua upande kiongozi akiwa wa dini yake akifanya vibaya hukaa kimya ila akija kiongozi sio wa dini yake watamkosoa huyo hadi akome kwa matamko kama yote
 
Unalaumu wakoloni wa kiarabu na wazungu kwa waliyoyatenda(ni sawa kuwalaumu kwa sababu viongozi wa dini hawakusema) ila kwa upande mwingine hayo yakitendwa na watawala weusi (unawalaumu viongozi wa dini wanapowakemea). Mbona kama huelewi unalisema.
Dishi limeyumba huyo
 
kuna kiongozi alituuzia mashirika na nyumba za serikali zote lakini walikaa kimya kabisa. Watafanya kufa na kupona mwenzao awe kiongozi ili wamtumie kwa faida. Tumeshuhudiwa watu wakirejeshewa majengo yaliyokuwa yametaifishwa huko nyuma. Wanadhani kuwa hatujui.
 
Unalaumu wakoloni wa kiarabu na wazungu kwa waliyoyatenda(ni sawa kuwalaumu kwa sababu viongozi wa dini hawakusema) ila kwa upande mwingine hayo yakitendwa na watawala weusi (unawalaumu viongozi wa dini wanapowakemea). Mbona kama huelewi unalisema.
ushahidi tunao kuwa maskofu na masheikh ndio waliowapokea wakoloni na kuwapatia hifadhi, chakula na vinywaji. Baada ya kuwanyonga babu zetu Jumapili na Ijumaa wanakwenda kusali makanisani na misikitini kama watu wema. Mapadre, maaskofu, maustadhi na masheikh hawakuwakemea wala kuwaambia mlichofanya ni dhambi. Leo hii eti wanaona viongozi wetu wanakosea na wanasema hadharani. Wanadhani sisi woote ni wajinga.

Kama watu wa dini hawa wangejitokeza hadharani kuwakemea wakoloni (jamaa zao) huenda tusingeibiwa kwa kiasi kile na akina Nyerere wasingehangaika na mifumo michafu ya uchaguzi ya kura tatu.
 
wewe tulia kabisa hakuna watu wanaosikilizwa na viongozi wa siasa kama viongozi wa dini hivyo ni lazima watoe matamko
 
wewe tulia kabisa hakuna watu wanaosikilizwa na viongozi wa siasa kama viongozi wa dini hivyo ni lazima watoe matamko
Hawasikilizwi yote. Kaka ngoja nikwambie kitu; hizi dini ziko zenye nguvu ya kutusimikia viongozi wa kwenda Ikulu na sehemu za maamuzi. Ndiyo maana tangu tupate uhuru ni aina mbili tu za madhehebu ndiyo yanayopokezana kwenda Ikulu, na hii haitokei kwa bahati mbaya; maslahi mapana ya pande zao. Unadhani ni kwanini dhehebu ileee ndio lilikuwa mstari wa mbele kupinga bandari kukodishwa kwa waarabu, kuwa na Kadhi na kujiunga OAC? Hukuwahi kumsikia mgombea mmoja kutoka dhehebu mojawapo akisema "mwaka huu ni zamu yetu"? unadhani alikuwa hana akili? Wandani hatujui.
 
Hii ni vita kati ya uovu na wema.
Wema lazima ushinde,ni suala la muda tu
 
Viongozi wa dini ni akina nani? Ebu wataje; alafu uje uniambie kuanzia Mh. Rais hadi waziri wa Sheria na Katiba kama hawakuwai kuwa viongozi kwa nyakati tofauti kwenye dini zenu hizo.

Kwahiyo kama wewe hukupata kumsaidia jirani yako kipindi ukiwa na uwezo huo ndiyo wanao pia wasiwasaidie majirani zao wakiwa na uwezo? Penye makosa yanahitaji kukemewa hata kama wengine hawapendi
 
Mpaka mnafanywa watumwa ni dhaifu kabisa ,dini zitaendelea kuwepo .
 
NOREFORMSNOELECTION.
 
NImekwambia dini zinazoaminika ni dini za asili tu; ni heri ya mpagani anaweza kulivusha bara la Afrika kuliko mwenye dini hizi exotic (ngeni) barani Afrika. Wachina na Wahindi wanasogea kwaasabu ya kutumia dini zao za asili. Hizi dini za Kiislam na Kikristo ni vichaka vyenye miiba mingi. Vichaka vilivyojaa majasusi, walanguzi, wezi, njama, mikakati na watu wasiolitakia bara mema. Vichaka hivi vinatupangia nani awe kiongozi na nani asiwe. Ni vichaka vinavyotudhoofisha kupitia njia za wazi na njia za siri.
 
Mpaka mnafanywa watumwa ni dhaifu kabisa ,dini zitaendelea kuwepo .
Kwa wakoloni walikuwa hawasali? HAPA tz walikuwa wakisali makanisa yapi na misikiti ipi? Je, Masheikh, mapadre na maaskofu walikuwa hawajui kama wakoloni hawa walikuwa wanatunyonya na kupeleka kwao? Mbona walikaa kimya dhidi ya wakoloni, mbona sasa wanasema kuhusu marais wetu? Wanamfanyia kazi nani? JIbu tafadhali
 
Nioneshe wapi viongozi wa dini walifanya utuwa,nikupe milion 100 ..Bila hizo dini mngekuwa wajinga mpaka leo ,tena mngekuwa watumwa..

Mmeanza kuuzwa na viongozi wenu ,chanzo cha utumwa ni watumwa wenyewe.
 
Wazungu wanasema "nioneshe rafiki Yako nikwambie wewe ni mtu Gani/nikwambie tabia Yako". Viongozi wa dini walikuwa wanasalisha, wanakula na kunywa na watu wakoloni wakoloni wanaonunua na kuuza watumwa na kutoa fungu la kumi, zaka, sadaka na malimbuko kanisani/msikitini.

Ukienda pale Zanzibar misikiti waliokuwa akiswali Sultan bado inaswaliwa mpaka Leo, hapa bara makanisa ya st. Peter, st. Joseph, Lutheran, Anglican, etc ambayo wakoloni walikuwa wakisali yapo hadi Leo
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Achana na ujinga nawe utakuwa mjinga ..Babu zako walikuwa wapumbavu ,waliuzana wenyewe kwa wenyewe
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Achana na ujinga nawe utakuwa mjinga ..Babu zako walikuwa wapumbavu ,waliuzana wenyewe kwa wenyewe
Wangeuza wapi kama kusingekuwa na soko?
 
Hii ni vita kati ya uovu na wema.
Wema lazima ushinde,ni suala la muda tu
Kakaaa!!! Dini hizi ni nyenzo muhimu kwa ukoloni mamboleo (neocolonialism). Ni grease ya wakoloni kuendelea kutuamulia na kutuibia. Majasusi wanakuja na kujificha kwenye makwapa ya dini. Alshabab, Al-qaida, Boko Haram, mapinduzi, na chaguzi zetu vyote vinayumbishwa na watu wa nje kupitia dini hizi za kigeni.

Umesikia wapi dini hizi zikilaani wazungu kwa uvamizi wa wazungu kule Palestine, Iraq, Libya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…