Niwape maua yenu Wasabato, mnajua kuimba nyimbo za dini

Nafikiri mitindo ya Zabron Singers, Rose Muhando, Good luck na wengineo ndio inawavutia wasikilizaji wengi wa Gospel bongo tofauti na namna SDA yenyewe inavyoimba.

Japo zipo kwaya maarufu za SDA zilizo tamba na zinazo tamba Mfano Mbiu SDA Choir ni maarufu na ina Album kubwa tu
 
So do I napenda sana kijaluo japo sio kibantu. Kuna mtu anaitwa Tony nyadundo anaimba sana nyimbo za kijaluo nina nyimbo zake kama 20 hivi unawezajua nami mjalauo
NAkutumia nyimbo Kali kuliko zote ulizozitaja Hapo juu. Kagoro sda wimbo unaitwa ka uwodha oserumo
 

Attachments

  • Kagoro_SDA_Choir-ka_wuodhwa_oserumo(240p).mp4
    10.1 MB
Yaani hua sichagui nyimbo ilimrad niaikie tu melody yake imekaa vizuri. Ninanyimbo za kijapan hapa hata sijui zina maana gani ila nasikiliza
Binafsi tuna fanana nina nyimbo za kizulu hata sielewi wanaimba nini ila zinanivutia na nazipenda
 
OMBI:

Anayeufahamu huu wimbo tafadhali anijuze niupakue YouTube, nimeshautafuta sana ila nimeshindwa kuupata, niliusikilizaga Morning Star Radio...[emoji116][emoji116]

BETI 1:

Twaitazamia asubuhi ya fahari yenye pumziko jema, waliochoka wakaribie msalaba wapate pumziko...×2.

CHORUS:

"Tuimbe kusifu, Haleluya, damu yake Yesu sisi yatusafi, asubuhi ya fahari tutamwona, akija nayo mawingu...×2".

BETI 2:

Wale wote waliosikia wito wake warejee kwa Bwana, wakaishi makao yale yenye amani wafurahi milele...×2.

CHORUS:

"Tuimbe kusifu, Haleluya, damu yake Yesu sisi yatusafi, asubuhi ya fahari tutamwona, akija nayo mawingu...×3".



Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mimi huwa narekodi audio za mahubiri na nyimbo zao kwenye smart phone nikiwa nimelala usiku.

Pia hata mahubiri yao yameshiba sana.

Kuna Mchungaji mmoja alifafanua vizuri unabii wa Daniel tokana na ndoto ya Mfalme Nebuchadnezzar "DANIEL 2" kuhusu tawala mbali mbali za kifalme za kidunia hadi Unabii utapotimia wa Yesu kuja kuutawala ulimwengu kwa ujio wa mara ya pili nilibarikiwa sana.

Uhakika wa kupata nyimbo za Wasabato zote ni vigumu sana ila ukisikiliza Morning Star Radio ya Wasabato na ukavizia siku za Alhamisi, Ijumaa kuamkia Jpili na J4 usiku utapata nyimbo zao nyingi sana tena zingine hadi za Msumbiji.



Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
So do I napenda sana kijaluo japo sio kibantu. Kuna mtu anaitwa Tony nyadundo anaimba sana nyimbo za kijaluo nina nyimbo zake kama 20 hivi unawezajua nami mjalauo
Wajaluo wana karama za uimbaji, huoni hata ile kwaya ya mbiu sda choir Mbagala Dar ilivyotikisa kwa asilimia kubwa Wajaluo ndiyo walikuwa wanakwaya, eg. "Tukutane paradiso".

Nimemkumbuka Marehemu Mwalimu wa kwaya Kurasini Mjaluo Kibaso.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli wanaimba sana tena vizuri
Japo ni wadhinifu sana sijui kwanini
Wengi wao ni wabishi wajuaji hasa siku ya sa7to
Miaka ya hivi karibuni 2010-2023 Ambassadors Of Christ kwaya toka Rwanda wametikisa sana wakifuatiwa na Light Bearers ya TZ japo zipo kwaya nyingine nyingi sana zinaimba vizuri sana.

Golden Gate ya Uganda nayo ilikuwa tishio East Africa enzi hizo.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Christina Shusho, Bahati Bukuku, Rose Muhando, Martha Mwaipaja wamekimbiza sana hasa hasa album zao za awali, ila hatimaye pumzi imekata kabakia Mwaipaja tu wengine wote siku hizi wanaimba nyimbo za kimataifa zisizo na utukufu wa Mungu kiuwasilishwaji kwa Hadhira husika.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi
 
Ningewapa maua iwapo wangeshika guitar, keyboard, drums, trumpet nk wakapiga wenyewe live badala ya kupigiwa na computer

Mimi nawapa maua yao kwa
  1. Usafi wa mavazi, mwili na mazingira
  2. Ulaji wa vhakula asili
  3. Kwa akina mama kukata nywele badala ya curl kit
  4. Nidhamu katika ibada
Ila sifurahishwi na kitendo chao cha kuwashambulia wakatoliki kwamba Papa ni mnyama
 

Rose mhando nae vipi ? Kuna mwimbaji wa kisabato anamzidi rose mhando kwa mauzo ya nyimbo zake ?
 
Mbona kwaya zinazotumia hivyo vifaa kama magita zipo nyingi tu, mfano Manzese SDA church Dar.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…