Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

'Spirituality' ina maana gani kwako?
Umeishia tu hapo, haitoshi kuky define wewe ni nani?

Una amini katika Mungu wa kidini, au tafsiri yako ya neno Mungu ni ipi

Au unaamini katika roho isiyokufa?
Twambie wewe ni nani tujue tuna deal na mtu wa aina gani

Pia, naona umekua trapped kwenye 'God of the gap fallacy'

Hoja za namna hii,
Kama Mungu hayupo kwanini kuna hiki na kile

Sayansi haina uwezo wa kujibu kila swali kwenye lifetime yako

Sayansi ni progressive,hatua kwa hatua inatupa majibu

Mpaka hivi tunavyofahamu sasa ni zao la miaka mingi, zao la wenye busara waliotutangulia

Zao la wakristo, waislamu na non believers ambao waliacha imani na mitazamo yao walipofika kwenye sayansi

Unapotaka kuthibitisha uhalali wa imani yako kwa ku point gape lililipo kwenye sayansi ni makosa

Sayansi, haiwezi kuelezea 99% ya jinsi gani ubongo unavyofanya kazi

Tunafahamu 1% tu, kutumia hili gape sio wewe tu hata mimi naweza sema kwenye kila ubongo wa binadamu kuna 'vijitu vidogo vidogo' Vinavyotengeneza ufahamu

Wala sina ushahidi wowote wa ninachosema

Unapo uliza energy imetokea wapi, ushawahi tenga mda wako na kujifunza kuhusu Casmir effect

Unafahamu kwamba, notion ya absolutely empty space haipo

vacuum ni bahari ya virtual particles zinazo tokea na kupotea kila sekunde, haijawahi kuwa empty na ndio origin ya ordinary particles zilizopo

Na hio sio theory tu, ni result ya maabara
Na haina ulazima wowote wa ku make sense kwako, kama huwezi tenga mda wa kufanya research

Kukipa kiumbe uhai maana yake nini?

Hebu elezea hata procedure unayotaka ifanyike?

Ushawahi sikia kuhusu GMO au cloning?
Au unataka wanasayansi wa design kiumbe hai out of thin air?

Hata wanasayansi wakishidwa kuumba kiumbe unachotaka kivipi kuna thibitisha imani yako?

Hata kama sijui squre ya 4 kwanini iwe 1?

Pia unaongea kama mtu ambaye hajawahi kusoma biological evolution

Possibly unachanganya biological evolution na historia ya chimpanzee na home sapience uliyosoma kwenye history

Kwenye historia ulionyeshwa just tip of the iceberg

Ukisoma evolution ukiwa open minded utagundua kwanini Charles Darwin anaheshima kubwa kwenye Biology kama Einsten kwenye Physics

Na ina applications kila sehemu mpaka kwenye computer science

Nikikwambia tunaweza kupata software yenye uwezo wa kufanya brain surgery kwa mafanikio bila ya kuitengeneza (kui program) utaamini?

Ushawahi sikia kuhusu Genetic programming?
Kivipi tunaweza pata high quality software kwa ku apply principle ya natural selection tukianza na trivial programs zisizoweza fanya chochote kile useful

Ndio maana kuna msemo unasema 99% wanaopinga evolution ni wale ambao hawajawahi soma kuhusu evolution
kwa kuongezea sayansi kwa mara ya kwanza inakubali inferantion conclusion hii n kwenye gravitional force only tunaona effect yake tu vitu vikirushwa juu vinarudi chini beyond that hakuna prove yeyote.
Hiyo bahari ya vacuum unaongelea dual-particle nature ambayo ndio basis ya law energy cannot be created no destroyed but can change from one state to another.
Hiyo walikuwa wanafanya maabara kuobserve hiyo particle baada ya mda ilipotea afu ikarejea ndio wakaja na hiyo law .
 
Ndio ulichosema ni kweli kwamba nilitakiwa nianze na tafsiri ya neno Mungu.

Tafsiri uliyotoa ni sahihi kulingana na huyo mwanasayansi anavyoeleza lakini tafsiri iliyokuwa bora zaidi naweza sema hivyo inapatikana kwenye vitabu vya kidini kitu ambacho toka mwanzo nlikataa kuvitumia kama reference

Neno Mungu sio kazi ya wanasayansi ndio maana naweza sema hiyo tafsiri yake inaweza isiwe bora. Wanasayansi wamepata hili neno nadhani kwa watu wanaoitwa theologists ambao misingi ya maisha yao na uelewa wa hii dunia wamekuwa wakiongozwa na Imani kitu ambacho kwa wanasayansi na wanafalsafa wanakataa pale wanapokuwa wanatafuta kujua ukweli

Ukweli tunaotafuta hapa ni juu ya kuwepo kwa Mungu. Ukitumia misingi ya kisayansi trust me ukweli utakuwa mgumu kupatikana vivyo hivyo ukifanya reasoning bado utakwama. Kwanini nasema itakuwa ngumu ni kwa sababu utakuwa unajaribu kutafuta ukweli ambao tayari upo

Mwanzo kabisa walioweza kuja na vitu tangible kuprove existence of God were prophets but kwa sasa hawa watu hatuna tena but we have their message

Kuhitimisha ni kuwa naweza nsiweze kuprove hili kwako kwa sasa but trust me after two years I will be back here with something tangible to prove existence of God

Thank You!
Maswali yaliyoshindwa sayansi vitabu vya dini haviwezi yapatia majibu. Vitabu hivyo ni hadithi tuu
 
Ukifa hutopata nafasi ya kujua chochote tena,
Jitahidi ujifunze ukiwa hai

Pia concept ya 'causation' kuwa kuna 'chanzo' na 'matokeo' ni dhana inayofanya kazi kwenye maisha yetu ya kawaida

Ubongo wetu ume evolved kuyaelewa maisha ya kila siku, rejea mada iliposema zamani tulikua part ya animal kingdom

Sasa kutafuta chanzo cha tokeo fulani, ilikua sifa muhimu kwa maisha yetu, unajua kuwa kunapofuka moshi lazima kuliwashwa moto au kuna moto, nikimbie au nibaki

Ila binadamu tulivyo staarabika na kujitenga na animal kingdom, tukaanza ku interact na vitu ambavyo vilikua nje na mazingira yaliyochochea evolution ya ubongo wetu

Vitu vikubwa sana kama Cluster s za galaxies, black holes au vitu vidogo kama neutrino au vitu kama 'anti matter' vinavyo safiri nyuma ya mda

Kwa ubongo wetu haviingi akilini, hio sentensi ya mwisho tu huwezi kuiamini, na yet ni fact.

So maana yangu ni kwamba ulazima wa kuwepo na chanzo cha kila kitu mpaka ulimwengu ni over generalization ya akili yetu ya kawaida ambayo ukitolewa nje ya mazingira ya kawaida ya miti na mito, haiwezi kutupa majibu
Mzee unatoa dozi sana wanabisha bure tuu
 
Mungu YUPO.

Kama unasema hayupo Mimi NAKURUHUSU utumie hizo principal zako ZOTE toka kwa wanadamu wote.. ILA, Niruhusu na Mimi nitumie Neno Lake Tu kutoka kwenye Biblia Takatifu.

Only a word..
 
JE MUNGU YUPO??

KAMA YUPO KWANINI WATU WANAPITIA KATIKA MAGUMU KAMA MAGONJWA, UMASKINI, LAAMA, MIKOSI N.K

#Jibu
Jamaa mmoja alikwenda saluni kunyolelwa.
Akiwa anaendelea kuhudumiwa (kunyolewa) akawa anapiga stor na kinyozi
Stori zao zilikuwa nzur na walizungumza mambo mengi sana bila kupishana kauli
Lakini pindi mteja alipogusia habari za neno la Mungu kinyozi akasema "hebu tuachane na hizo stori maana mimi siamini kama Mungu yupo"
"Kwanin unasema hivyo?" Mteja akauliza
Kinyozi akasema "kwa ushauri wangu ni bora uende huko nje na ukawatangazie watu ya kwamba Mungu hayupo"
Na akaendekea akisema "Hebu niambie
-kama mungu yupo kwann ukienda mahospitalini utakuta watu ni wangonjwa?
-Kama mungu yupo kwann ukienda huko mitaani unakuta kuna watoto omba omba?
-Kama mungu yupo kwann ukienda magerezani unakuta watu wamefungwa kwa kuonewa?
"Hivi unafikiri kama Mungu angekuwepo kweli angeruhusu mambo yote haya?"

Mteja akafikiria kidogo na kumuomba Roho Mtakatifu kimoyomoyo ili amfunulie kwani alikua ana Imani sana na alitaka kumsaidia yule kinyozi arudishe Imani yake kwa Mungu na amvute kwa Bwana ila hakuweza kujibu chochote maana hakuwa na Jibu la haraka kwa wakati ule na pia alihitaji busara ya Roho wa Bwana hivyo alikaa kimya kimya akisubiri Roho wa Mungu ampe jibu na hekima ya kumjibu
Na Kinyozi alipomaliza kumnyoa, Mteja akaenda zake akiwa anatafakari swali lile aliloulizwa.

Akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake mteja akakutana na mtu mmoja akiwa na nywele ndefu, chafu huku ndevu zake zikiwa nyingi kupita kawaida kwa ujumla alikuwa ni mchafu.

Ndipo akagundua kwamba Roho wa Mungu alikua Kamjibu kwani kwa kupitia Mtu yule alipata hekima ya kumjibu vyema yule kinyozi aliyevunjika moyo na kupoteza imani yake.

Mteja akaamua kurudi saluni kwa mara nyingine na kusema "unajua nn? Vinyozi hawapo"

"Kwann unasema hivyo?" Kwa mshituko kinyozi akauliza "si mimi hapa kinyozi na muda si mrefu nimetoka kukunyoa"
“hapana!” mteja akasisitiza. "Vinyozi hawapo kwa sababu Kama wangekuwepo kusingekuwa na watu wenye nywele ndefu,chafu na ndevu nyingi kupita kawaida kama mmoja niliyemuona huko nje.”

Kinyozi akasema; “Ah, vinyozi tupo ila kinachotokea ni kwamba watu hawajataka kuja saluni ili tuwanyoe.”
“Sawa kabisa”- mteja akakazia;

“Hiyo ndo pointi niliyokuwa nikiisubiri.”

Mungu pia yupo;

Ila kinachotokea ni kwamba watu hawamfuati yeye na nyoyo zao bado hazijafunguka kwaajili ya kuutafuta utetezi na uponyaji wake.
Ila kama watu wakimtumainia yeye kwa roho na kweli huku wakimfanya kuwa ndiye mlinzi, mponyaji na mtetezi wao.
Amini watakuwa salama maana hakuna jambo gumu yeye asiloliweza.

Watu wengi tumeshindwa kujua majibu yetu halisi au kutambua ishara tunapojibiwa na Mungu kupitia Roho wake kutokana na uzito wa akili zetu kwani tumekua tukichanganywa na hisia za Milango yetu ya fahamu...

Mfano
-Unaweza kujiona upo tayari kuanza huduma lakini je Roho wa Mungu kakujibu au kakuruhusu kuanza hiyo huduma?
au unataka upande madhabahuni kuhubiri lakini je Roho wa Mungu kakuruhusu?
_________________________________
MAOMBI.
Kwa Jina la Yesu Kristo namuomba Roho wa Mungu Akupe hekima na Majibu sahihi pale unapojikuta katika wakati Mgumu wa kukosa Majibu na akaifanye akili yako iwe nyepesi kutambua ishara na hekima zake
Amina
____________________________________
Kama una amini kwamba Mungu yupo na una imani ipo siku atakushindia dhidi ya magonjwa,umaskini,laana ,kuonewa,kudharauliwa, na magumu yote unayopitia katika maisha yako Comment "AMEN"Kudhihirisha uwepo wake katika maisha Yako na Mungu wa Mbinguni atakujibu sawa sawa na Ukiri wako.
Hizi ni hekaya
 
Ebu nipe mchanganuo wa sifa za huyo Mungu wako ambaye unamuamini kua yupo nijue ana sifa zipi

Maana ukiniambia evil ni part ya hoja inayothibitisha huyo Mungu yupo basi huyu atakua ni Mungu wa kitofauti kidogo na ambao nimekua nikimsikia akihubiriwa na wa watu wengi hususani abrahamic religion.

Kwasababu sifa ya kuu ya Mungu wao ni mwenye upendo wote, sasa mwenye upendo wote hachangamani na evil, evil mara nyingi ni sifa ambayo nimeiona akipewa shetani.

Kwa hiyo mimi naomba udadavua kidogo maana ya Mungu kisha unipe na sifa zake ndio tumjadili kimapana zaidi
Hapa mkuu nilikuwa nafanya utangulizi tu sio kama nilitaka kusema Mungu anachangamana na uovu

Ukwel ni kuwa nilitaka kutumia njia ya chanzo cha wema na uovu kuprove the existence of God beyond religion lakini baada ya debate kupamba moto nimebaini nina kazi nyingine ya ziada na nimeona bado kuna kitu hakijakaa sawa but I promise ntalitimiza hili na ntarudi na majibu ya kila hoja ambayo inaquestion uwepo wa Mungu
 
Maswali yaliyoshindwa sayansi vitabu vya dini haviwezi yapatia majibu. Vitabu hivyo ni hadithi tuu
Ukweli mwingine ni kuwa ata sayansi haiwezi kutoa maelezo ya ambacho umekipa tafsiri ya hadithi

Sema ningeomba unipe ufafanuzi kidogo wa hili jambo.Umeongelea kitu sayansi sio? sasa unaweza kunipa ufafanuzi wa hiki unachokipa jina sayansi chimbuko lake ni nini
 
Kwa hiyo hata hoja yako kuhusu uthibitisho wa kuonesha Mungu yupo ulikua based kwenye imani?
Ukweli ni kuwa anayeweza kuprove existence of God bila kuhusisha imani sidhani kama yupo.

Mitume na Manabii waliweza kuprove bila kutumia vitabu vya dini lakini hawakuwahi kukosa imani katika kueleza uwepo wa Mungu kwa maana imani ni nguzo muhimu katika kueleza uwepo wa Mungu

Binafsi naweza kuprove kwako bila kutumia vitabu vya dini ila naona kama kuna vitu inabidi nivikamilishe kwanza. Nkuombe tu subira mkuu,hoja zote nazisoma nadhani zitaniongoza kipindi nakamalisha maelezo yangu
 
Mkuu nitakujibu bila kutumia reference ya vitabu vya dini kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu muweza wa yote,Wakati nasoma kiswahili enzi zile nilifundishwa kuwa uwepo wa neno katika Lugha fulani unathibitisha uwepo wa kitu/Hali hiyo katika jamii ya watu wa lugha husika.

Mfano neno Kijiko Ni neno la kiswahili,ukija katika Lugha ya kisukuma ,kimakonde au kijita huwezi pata neno Kijiko kwa lugha hiyo,hii imamaanisha kuwa makabila niliyoyataja hayakuwa na utamaduni wa kutumia vijiko enzi zao,ndo maana lugha hizo hazina neno sahihi la Kijiko tofauti na kutumia lugha ya kiswahili ili kupata neno husika katika Lugha hizo.

Ukija kwenye neno God kwa kingereza,kwa kiswahili ni Mungu,kwa kihaya/kijita/kizinza ni Mukama na kwa wasukuma ni Lyuba/seba/Mulungu, hivyo maneno haya yanathibitisha uwepo wa Mungu katika jamii nilizozitaja kutokana na kuwepo kwa maneno hayo,ingekuwa kwamba jamii za kiafrika zilipokea tu habari za Mungu toka kwa wazungu Basi neno God/Mungu lingetamkika kwa namna moja katika jamii husika kwani Ni lugha ya kupokea.

Chukulia neno gari au neno simu,kwa jamii za Tanzania sote katika Lugha zetu tunayatamuka maneno hayo Kama yalivyo isipokuwa tunaongeza tu viambishi awali katika mizizi ya maneno husika,hii Ni kutokana na ukweli kwamba watanzania hatukuwahi kuwa na utamaduni wa kutumia simu au gari ndo maana tunakosa maneno sahihi kurejelea vitu hivyo.

Mungu yupo mkuu! Unapokula ukashiba unaweza sema Tanzania hii hakuna watu wanalala njaa,just because wewe unasaza!! Be watchiful mpendwa.
 
Takataka iliyofinyangwa kutoka kwenye udongo na kupewa uhai na ufahamu, takataka iliyojaa uchafu ndani yake, takataka iliyopewa nafasi ya kuishi si zaidi ya miaka 70 ikizidi sana labda miaka 120, takataka hiyo sababu tu imejifunza kusoma na kuandika eti inasimama na kusema, "hakuna MUNGU".

Like seriously hakuna MUNGU?

Let me tell you this you foolish man. GOD's existence is logical and I can prove that to you, but because you are a fool I don't have time to prove anything to fools.

Fools can go to school and be educated but they can never attain the knowledge.

Hata kama mpumbavu atakuwa na PhDs zaidi ya 10 lakini kamwe upumbavu wake hauwezi kumtoka.
Huoni kama umekosa hata staha?
Mwombe basi huyo Mungu unayemuamini akufundishe hata adabu na jinsi gani ya kujenga hoja kisomi mbele za watu

Sio unaanza kuita watu wapumbavu bila kujenga, watu wanao fatilia huu uzi wata ku discredit tu

Kama wewe umeaminishwa wewe ni takataka, kondoo au bibi harusi amini wewe tu

Sio unaanza kuita kila mtu takataka

Kama mpumbavu humu ndani ni wewe. Huna hoja umetumia mihemko

Na hio ndiyo final attempt ya mtu aliyeshindwa kujadili kisomi
 
Mkuu nitakujibu bila kutumia reference ya vitabu vya dini kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu muweza wa yote,Wakati nasoma kiswahili enzi zile nilifundishwa kuwa uwepo wa neno katika Lugha fulani unathibitisha uwepo wa kitu/Hali hiyo katika jamii ya watu wa lugha husika.

Mfano neno Kijiko Ni neno la kiswahili,ukija katika Lugha ya kisukuma ,kimakonde au kijita huwezi pata neno Kijiko kwa lugha hiyo,hii imamaanisha kuwa makabila niliyoyataja hayakuwa na utamaduni wa kutumia vijiko enzi zao,ndo maana lugha hizo hazina neno sahihi la Kijiko tofauti na kutumia lugha ya kiswahili ili kupata neno husika katika Lugha hizo.

Ukija kwenye neno God kwa kingereza,kwa kiswahili ni Mungu,kwa kihaya/kijita/kizinza ni Mukama na kwa wasukuma ni Lyuba/seba/Mulungu, hivyo maneno haya yanathibitisha uwepo wa Mungu katika jamii nilizozitaja kutokana na kuwepo kwa maneno hayo,ingekuwa kwamba jamii za kiafrika zilipokea tu habari za Mungu toka kwa wazungu Basi neno God/Mungu lingetamkika kwa namna moja katika jamii husika kwani Ni lugha ya kupokea.

Chukulia neno gari au neno simu,kwa jamii za Tanzania sote katika Lugha zetu tunayatamuka maneno hayo Kama yalivyo isipokuwa tunaongeza tu viambishi awali katika mizizi ya maneno husika,hii Ni kutokana na ukweli kwamba watanzania hatukuwahi kuwa na utamaduni wa kutumia simu au gari ndo maana tunakosa maneno sahihi kurejelea vitu hivyo.

Mungu yupo mkuu! Unapokula ukashiba unaweza sema Tanzania hii hakuna watu wanalala njaa,just because wewe unasaza!! Be watchiful mpendwa.
Fact kuwa kuna neno linatumika katika jamii nyingi halina maana kuwa kitu kinacho wakilishwa na hilo neno kina ishi in reality

Neno Mungu ni tofauti na neno maji, neno maji linawakilisha kitu halisi kilichopo

Kuwepo kwa hicho kitu, kinafanya dunia nzima tukubaliane kuwa neno maji lina maana gani,

Lakini neno Mungu ni tofauti, neno Mungu lipo katika kundi ambalo wanasaikolojia na wanafalsafa wanali term kama Essentially contested concept au ECC

Ni aina ya maneno yenye sifa hizi
1.Wote tunakubaliana kuwe hilo neno lipo
2.Lakini hatukubaliani kuwa hilo neno lina maana gani

In short ECC ni neno ambalo halina Universal meaning

Mfano wa ECC ni maneno kama 'Maadili', 'uraia', 'utawala wa sheria', 'uhuru', 'vita' , 'mapenzi'

Tunafahamu hayo maneno yapo na kila jamii ina neno hilo katika lugha yake lakini sote hatukubaliani juu ya maana hio

Neno 'uhuru' lina maana tofauti tofauti nchi hadi nchi, neno 'uhuru' kwa mmarekani halina maana na neno 'uhuru' kwa mchina, na wetu wanakubaliana kuwa neno uhuru lipo

Sawa sawa kabisa na neno Mungu, sote tunakubaliana neno Mungu lipo kama concept, lakini hatuwezi kubaliana lina maana gani na hatutaweza

Mu hindu ana maana yake, muislamu ana maana yake, Spinoza alikua na maana yake, kwa imani za africa ya kale kulikua na maana yake

Sasa kutaka kuamini hili neno ambalo hatukubaliani lina maana gani linawakilisha kitu kimoja kinacho ishi haiwezekani

Ku sum up, fact kuwa kuna neno Mungu katika kila jamii halina maana kuwa kuna kitu halisi kinachowakilishwa na hilo neno, na hicho kitu kinaishi na kinajitambua

Utanioni wa ajabu nikikwambia nimetoka kupiga story na vita au nimekorofishana na amani

Ni concept tu, haziwakilishi kitu chochote tangible
 
Hoja ya kuwa hakuna mungu duniani ni unaprovable concept...kwa sababu sayansi Hadi leo haitoi majini yanaeleweka kuhusiana na asili ya ulimwengu huu ukisoma geography utakuta nadharia nyingi ambazo ziko weak na hazijitoshelezi....hata Darwin na nadharia yake ya evolution bado inamapungufu juu ya asili ya viumbe na ulimwengu...na pia inasemekana kabla hajafa alitubu...hata ukiangalia wanafalsafa wanakubali kuwa Kuna natural power which create the universe...lakini kwa kumalizia ushaidi mkubwa zaidi juu ya uwepo wa mungu ni kuwa ukiangalia nature ya miili ya yetu sisi wanadamu na viumbe vingine utaona kuwa mtu katudesign mfano miili yetu iko full mechanized mfano utoaji na uingizaji wa hewa ...mfumo wa chakula kuanzia kwenye meno kisagwa kwa chakula na utolewaji wa taka mwili...ukitafakari kwa undani utagundua tumeumbwa coz tunascientific bodies ambayo inaonyesha dhairi shairi kuwa tumeumbwa na mtu mwingine mwenye nguvu zaidi yetu.....so mungu yupo hata habari za mitume Kama yesu ni real story ...
 
Time ni nin? Time ina exist only in our mind iko deep programmed kweny mind tu.
Only kuna present ambayo ndio real ukisema jana iko wap? ni memory tu tulizonazo.
kesho ni only imagination.
Time consious sio halisi everything exist at per lakini uwezo wetu wa kuperceive matukio uko kwenye series hatuwezi kuyaperceive at once
due to nature of our body. kwa vitu ambavyo sio hai time sio realy ni sisi tunaozani time ni realy.
ukiwa unaangalia movie yote ina exist at once lakini uwezo wako wakuiperceive ni series wise
Now umenielewa, time si kitu halisi ni illusion tu kama concept ya uwepo wa Mungu tu
 
Fact kuwa kuna neno linatumika katika jamii nyingi halina maana kuwa kitu kinacho wakilishwa na hilo neno kina ishi in reality

Neno Mungu ni tofauti na neno maji, neno maji linawakilisha kitu halisi kilichopo

Kuwepo kwa hicho kitu, kinafanya dunia nzima tukubaliane kuwa neno maji lina maana gani,

Lakini neno Mungu ni tofauti, neno Mungu lipo katika kundi ambalo wanasaikolojia na wanafalsafa wanali term kama Essentially contested concept au ECC

Ni aina ya maneno yenye sifa hizi
1.Wote tunakubaliana kuwe hilo neno lipo
2.Lakini hatukubaliani kuwa hilo neno lina maana gani

In short ECC ni neno ambalo halina Universal meaning

Mfano wa ECC ni maneno kama 'Maadili', 'uraia', 'utawala wa sheria', 'uhuru', 'vita' , 'mapenzi'

Tunafahamu hayo maneno yapo na kila jamii ina neno hilo katika lugha yake lakini sote hatukubaliani juu ya maana hio

Neno 'uhuru' lina maana tofauti tofauti nchi hadi nchi, neno 'uhuru' kwa mmarekani halina maana na neno 'uhuru' kwa mchina, na wetu wanakubaliana kuwa neno uhuru lipo

Sawa sawa kabisa na neno Mungu, sote tunakubaliana neno Mungu lipo kama concept, lakini hatuwezi kubaliana lina maana gani na hatutaweza

Mu hindu ana maana yake, muislamu ana maana yake, Spinoza alikua na maana yake, kwa imani za africa ya kale kulikua na maana yake

Sasa kutaka kuamini hili neno ambalo hatukubaliani lina maana gani linawakilisha kitu kimoja kinacho ishi haiwezekani

Ku sum up, fact kuwa kuna neno Mungu katika kila jamii halina maana kuwa kuna kitu halisi kinachowakilishwa na hilo neno, na hicho kitu kinaishi na kinajitambua

Utanioni wa ajabu nikikwambia nimetoka kupiga story na vita au nimekorofishana na amani

Ni concept tu, haziwakilishi kitu chochote tangible
Mkuu unaaelewa juu ya uwepo wa nomino za zahania(uzanifu) maana yake hizo Ni nomino zinazotaja vitu vya kufikirika lakini himaanishi kuwa vitu hivyo havipo,kutokuviona haimaanishi kuwa havipo.

Mfano wa maneno Mungu,uchoyo ,njaa,urafi ,malaika ,furaha,chuki,urafiki nk. Haya Ni maneno zahania,je unataka kuniambia kuwa hakuna furaha Kati ya wanadamu,au chuki ?Maana furaha,chuki ,uchoyo Ni maneno yasiyo na umbo la kitu,maana yake hatuwezi kuona kwa macho kitu kinaitwa chuki,furaha au uchoyo,lakini vipo!!

Kutokuonekana kwa kitu haimaniishi hakipo mkuu!!!
 
Ukinijibu haya maswali vizuri na nikakuelewa basii nitaamini Mungu hayupo kweli..

1)Kwanini binadamu anakufa?

2)Ni nini kinamfanya binadamu afe?

3)Binadamu akifa anaenda wapi?

4)Kwann binadamu awezi ishi milele?
 
Ukweli ni kuwa anayeweza kuprove existence of God bila kuhusisha imani sidhani kama yupo.

Mitume na Manabii waliweza kuprove bila kutumia vitabu vya dini lakini hawakuwahi kukosa imani katika kueleza uwepo wa Mungu kwa maana imani ni nguzo muhimu katika kueleza uwepo wa Mungu

Binafsi naweza kuprove kwako bila kutumia vitabu vya dini ila naona kama kuna vitu inabidi nivikamilishe kwanza. Nkuombe tu subira mkuu,hoja zote nazisoma nadhani zitaniongoza kipindi nakamalisha maelezo yangu
Mkuu imani ni ku accept jambo bila uthibitisho, kilichothibitishwa hakipo kwenye imani. Kusema mitume wamethibitisha mungu yupo kwa imani ni contradiction
 
Now umenielewa, time si kitu halisi ni illusion tu kama concept ya uwepo wa Mungu tu
Sijawah pingana na wew kuhus mda kuhusu Mungu sijawahi kubaliana na wew
Japo sio katika Mungu aliye be proclaimed na vitabu vya dini
 
Mkuu unaaelewa juu ya uwepo wa nomino za zahania(uzanifu) maana yake hizo Ni nomino zinazotaja vitu vya kufikirika lakini himaanishi kuwa vitu hivyo havipo,kutokuviona haimaanishi kuwa havipo.

Mfano wa maneno Mungu,uchoyo ,njaa,urafi ,malaika ,furaha,chuki,urafiki nk. Haya Ni maneno zahania,je unataka kuniambia kuwa hakuna furaha Kati ya wanadamu,au chuki ?Maana furaha,chuki ,uchoyo Ni maneno yasiyo na umbo la kitu,maana yake hatuwezi kuona kwa macho kitu kinaitwa chuki,furaha au uchoyo,lakini vipo!!

Kutokuonekana kwa kitu haimaniishi hakipo mkuu!!!
ndio maana nikakwambia yana exist kama dhana tu
dhana ni human construction
na ndio key point ya hii mada

Chuki, furaha, uhuru, kuchoka na maneno mengine yana exist kwenye akili ya binadamu tu

Kwa viumbe vingine havipo
The same goes with God, ni neno dhahania kali ulivyosema

Lina maana tu kweli akili yetu kama kuchoka kulivyo na maana kwetu na sio kwa machine

Nje ya akili ya binadamu hakuna Uhuru wala demokrasi, ni human imagination inayofanya vionekane kuwepo
 
Back
Top Bottom