Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

kwa kuongezea sayansi kwa mara ya kwanza inakubali inferantion conclusion hii n kwenye gravitional force only tunaona effect yake tu vitu vikirushwa juu vinarudi chini beyond that hakuna prove yeyote.
Hiyo bahari ya vacuum unaongelea dual-particle nature ambayo ndio basis ya law energy cannot be created no destroyed but can change from one state to another.
Hiyo walikuwa wanafanya maabara kuobserve hiyo particle baada ya mda ilipotea afu ikarejea ndio wakaja na hiyo law .
 
Maswali yaliyoshindwa sayansi vitabu vya dini haviwezi yapatia majibu. Vitabu hivyo ni hadithi tuu
 
Mzee unatoa dozi sana wanabisha bure tuu
 
Mungu YUPO.

Kama unasema hayupo Mimi NAKURUHUSU utumie hizo principal zako ZOTE toka kwa wanadamu wote.. ILA, Niruhusu na Mimi nitumie Neno Lake Tu kutoka kwenye Biblia Takatifu.

Only a word..
 
Hizi ni hekaya
 
Hapa mkuu nilikuwa nafanya utangulizi tu sio kama nilitaka kusema Mungu anachangamana na uovu

Ukwel ni kuwa nilitaka kutumia njia ya chanzo cha wema na uovu kuprove the existence of God beyond religion lakini baada ya debate kupamba moto nimebaini nina kazi nyingine ya ziada na nimeona bado kuna kitu hakijakaa sawa but I promise ntalitimiza hili na ntarudi na majibu ya kila hoja ambayo inaquestion uwepo wa Mungu
 
Maswali yaliyoshindwa sayansi vitabu vya dini haviwezi yapatia majibu. Vitabu hivyo ni hadithi tuu
Ukweli mwingine ni kuwa ata sayansi haiwezi kutoa maelezo ya ambacho umekipa tafsiri ya hadithi

Sema ningeomba unipe ufafanuzi kidogo wa hili jambo.Umeongelea kitu sayansi sio? sasa unaweza kunipa ufafanuzi wa hiki unachokipa jina sayansi chimbuko lake ni nini
 
Kwa hiyo hata hoja yako kuhusu uthibitisho wa kuonesha Mungu yupo ulikua based kwenye imani?
Ukweli ni kuwa anayeweza kuprove existence of God bila kuhusisha imani sidhani kama yupo.

Mitume na Manabii waliweza kuprove bila kutumia vitabu vya dini lakini hawakuwahi kukosa imani katika kueleza uwepo wa Mungu kwa maana imani ni nguzo muhimu katika kueleza uwepo wa Mungu

Binafsi naweza kuprove kwako bila kutumia vitabu vya dini ila naona kama kuna vitu inabidi nivikamilishe kwanza. Nkuombe tu subira mkuu,hoja zote nazisoma nadhani zitaniongoza kipindi nakamalisha maelezo yangu
 
Mkuu nitakujibu bila kutumia reference ya vitabu vya dini kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu muweza wa yote,Wakati nasoma kiswahili enzi zile nilifundishwa kuwa uwepo wa neno katika Lugha fulani unathibitisha uwepo wa kitu/Hali hiyo katika jamii ya watu wa lugha husika.

Mfano neno Kijiko Ni neno la kiswahili,ukija katika Lugha ya kisukuma ,kimakonde au kijita huwezi pata neno Kijiko kwa lugha hiyo,hii imamaanisha kuwa makabila niliyoyataja hayakuwa na utamaduni wa kutumia vijiko enzi zao,ndo maana lugha hizo hazina neno sahihi la Kijiko tofauti na kutumia lugha ya kiswahili ili kupata neno husika katika Lugha hizo.

Ukija kwenye neno God kwa kingereza,kwa kiswahili ni Mungu,kwa kihaya/kijita/kizinza ni Mukama na kwa wasukuma ni Lyuba/seba/Mulungu, hivyo maneno haya yanathibitisha uwepo wa Mungu katika jamii nilizozitaja kutokana na kuwepo kwa maneno hayo,ingekuwa kwamba jamii za kiafrika zilipokea tu habari za Mungu toka kwa wazungu Basi neno God/Mungu lingetamkika kwa namna moja katika jamii husika kwani Ni lugha ya kupokea.

Chukulia neno gari au neno simu,kwa jamii za Tanzania sote katika Lugha zetu tunayatamuka maneno hayo Kama yalivyo isipokuwa tunaongeza tu viambishi awali katika mizizi ya maneno husika,hii Ni kutokana na ukweli kwamba watanzania hatukuwahi kuwa na utamaduni wa kutumia simu au gari ndo maana tunakosa maneno sahihi kurejelea vitu hivyo.

Mungu yupo mkuu! Unapokula ukashiba unaweza sema Tanzania hii hakuna watu wanalala njaa,just because wewe unasaza!! Be watchiful mpendwa.
 
Huoni kama umekosa hata staha?
Mwombe basi huyo Mungu unayemuamini akufundishe hata adabu na jinsi gani ya kujenga hoja kisomi mbele za watu

Sio unaanza kuita watu wapumbavu bila kujenga, watu wanao fatilia huu uzi wata ku discredit tu

Kama wewe umeaminishwa wewe ni takataka, kondoo au bibi harusi amini wewe tu

Sio unaanza kuita kila mtu takataka

Kama mpumbavu humu ndani ni wewe. Huna hoja umetumia mihemko

Na hio ndiyo final attempt ya mtu aliyeshindwa kujadili kisomi
 
Fact kuwa kuna neno linatumika katika jamii nyingi halina maana kuwa kitu kinacho wakilishwa na hilo neno kina ishi in reality

Neno Mungu ni tofauti na neno maji, neno maji linawakilisha kitu halisi kilichopo

Kuwepo kwa hicho kitu, kinafanya dunia nzima tukubaliane kuwa neno maji lina maana gani,

Lakini neno Mungu ni tofauti, neno Mungu lipo katika kundi ambalo wanasaikolojia na wanafalsafa wanali term kama Essentially contested concept au ECC

Ni aina ya maneno yenye sifa hizi
1.Wote tunakubaliana kuwe hilo neno lipo
2.Lakini hatukubaliani kuwa hilo neno lina maana gani

In short ECC ni neno ambalo halina Universal meaning

Mfano wa ECC ni maneno kama 'Maadili', 'uraia', 'utawala wa sheria', 'uhuru', 'vita' , 'mapenzi'

Tunafahamu hayo maneno yapo na kila jamii ina neno hilo katika lugha yake lakini sote hatukubaliani juu ya maana hio

Neno 'uhuru' lina maana tofauti tofauti nchi hadi nchi, neno 'uhuru' kwa mmarekani halina maana na neno 'uhuru' kwa mchina, na wetu wanakubaliana kuwa neno uhuru lipo

Sawa sawa kabisa na neno Mungu, sote tunakubaliana neno Mungu lipo kama concept, lakini hatuwezi kubaliana lina maana gani na hatutaweza

Mu hindu ana maana yake, muislamu ana maana yake, Spinoza alikua na maana yake, kwa imani za africa ya kale kulikua na maana yake

Sasa kutaka kuamini hili neno ambalo hatukubaliani lina maana gani linawakilisha kitu kimoja kinacho ishi haiwezekani

Ku sum up, fact kuwa kuna neno Mungu katika kila jamii halina maana kuwa kuna kitu halisi kinachowakilishwa na hilo neno, na hicho kitu kinaishi na kinajitambua

Utanioni wa ajabu nikikwambia nimetoka kupiga story na vita au nimekorofishana na amani

Ni concept tu, haziwakilishi kitu chochote tangible
 
Hoja ya kuwa hakuna mungu duniani ni unaprovable concept...kwa sababu sayansi Hadi leo haitoi majini yanaeleweka kuhusiana na asili ya ulimwengu huu ukisoma geography utakuta nadharia nyingi ambazo ziko weak na hazijitoshelezi....hata Darwin na nadharia yake ya evolution bado inamapungufu juu ya asili ya viumbe na ulimwengu...na pia inasemekana kabla hajafa alitubu...hata ukiangalia wanafalsafa wanakubali kuwa Kuna natural power which create the universe...lakini kwa kumalizia ushaidi mkubwa zaidi juu ya uwepo wa mungu ni kuwa ukiangalia nature ya miili ya yetu sisi wanadamu na viumbe vingine utaona kuwa mtu katudesign mfano miili yetu iko full mechanized mfano utoaji na uingizaji wa hewa ...mfumo wa chakula kuanzia kwenye meno kisagwa kwa chakula na utolewaji wa taka mwili...ukitafakari kwa undani utagundua tumeumbwa coz tunascientific bodies ambayo inaonyesha dhairi shairi kuwa tumeumbwa na mtu mwingine mwenye nguvu zaidi yetu.....so mungu yupo hata habari za mitume Kama yesu ni real story ...
 
Now umenielewa, time si kitu halisi ni illusion tu kama concept ya uwepo wa Mungu tu
 
Mkuu unaaelewa juu ya uwepo wa nomino za zahania(uzanifu) maana yake hizo Ni nomino zinazotaja vitu vya kufikirika lakini himaanishi kuwa vitu hivyo havipo,kutokuviona haimaanishi kuwa havipo.

Mfano wa maneno Mungu,uchoyo ,njaa,urafi ,malaika ,furaha,chuki,urafiki nk. Haya Ni maneno zahania,je unataka kuniambia kuwa hakuna furaha Kati ya wanadamu,au chuki ?Maana furaha,chuki ,uchoyo Ni maneno yasiyo na umbo la kitu,maana yake hatuwezi kuona kwa macho kitu kinaitwa chuki,furaha au uchoyo,lakini vipo!!

Kutokuonekana kwa kitu haimaniishi hakipo mkuu!!!
 
Ukinijibu haya maswali vizuri na nikakuelewa basii nitaamini Mungu hayupo kweli..

1)Kwanini binadamu anakufa?

2)Ni nini kinamfanya binadamu afe?

3)Binadamu akifa anaenda wapi?

4)Kwann binadamu awezi ishi milele?
 
Mkuu imani ni ku accept jambo bila uthibitisho, kilichothibitishwa hakipo kwenye imani. Kusema mitume wamethibitisha mungu yupo kwa imani ni contradiction
 
Now umenielewa, time si kitu halisi ni illusion tu kama concept ya uwepo wa Mungu tu
Sijawah pingana na wew kuhus mda kuhusu Mungu sijawahi kubaliana na wew
Japo sio katika Mungu aliye be proclaimed na vitabu vya dini
 
ndio maana nikakwambia yana exist kama dhana tu
dhana ni human construction
na ndio key point ya hii mada

Chuki, furaha, uhuru, kuchoka na maneno mengine yana exist kwenye akili ya binadamu tu

Kwa viumbe vingine havipo
The same goes with God, ni neno dhahania kali ulivyosema

Lina maana tu kweli akili yetu kama kuchoka kulivyo na maana kwetu na sio kwa machine

Nje ya akili ya binadamu hakuna Uhuru wala demokrasi, ni human imagination inayofanya vionekane kuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…